Wafugaji wa kuku wa nyama na mayai wasiosajiliwa kuchukuliwa hatua

Wafugaji wa kuku wa nyama na mayai wasiosajiliwa kuchukuliwa hatua

View attachment 1039167

Wafugaji wa kuku wa nyama na mayai wametakiwa kujisajili kisheria ili waweze kutambulika na kufanya kazi ya ufugaji kwa ufuata sheria zilizowekwa.

Imeelezwa kuwa wote ambao hawajasajiliwa lakini wanafanya kazi ya ufugaji kuku , hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mpaka sasa takwimu zinaonyesha ni wafugaji 41 tu ndio wameshasajiliwa.
Mamlaka zinazohusika zimesema ni lazima kila mfugaji kuku kuwa na kitambulisho, na asiye nacho atachukuliwa hatua za kisheria.

Taarifa hio pia imedai kuwa hata wauzaji pia wa kuku na mayai ni lazima kuwa na vitambulisho hivyo.
Halafu bata je? Na kanga, njiwa, sungura, kitimoto, bt mzinga, kwale, somba, mchicha, kisamvu, spinachi, minazi, miembe, michungwa, matango, na mlenda je?
 
Wasiwasahau wafugaji wa ndevu nao, wameongezeka sana hasa maeneo ya Kinondoni!
 
"Tunanunua drim laina kwa fedha zetu za ndani"
 
Aisee Tunakoenda siko. Ebu fikiria Nmemaliza kozi ya IT sina kazi, nkaona bora nijiajiri nitengeneze kablog kangu au website yangu baada ya kulipia domain name naambiwa inabidi nilipie usajili wa wesite millioni moja kwa serikali. Okaay nkaona hio milioni sina nkaamua niachane kwanza na mambo ya website na blog yangu nkaanza kufuga kuku, Punde si punde naambiwa na ufugaji wa kuku inabidi nijisajili na nilipe kodi. Nkaona niachane na hio tena, Nkafikiria kile kisima nlichoachiwa na bibi mzaa mama, Nkasema yeees acha nianze kuuza maji mtaani kwenye kile kisima, napo nkaja kuambiwa inabidi nilipe kodi. Aiseee Kwa namna hii sie tuliopo kwenye 'Jobless Corner' Tutatokaje kimaisha. sasa kila startup itakua inafeli kutokana na hizi kodi zisizoeleweka. Whyyy!!!!!!!
Malaya na matapeli ni wengi sana kodi hawalipi
 
Hii ni habari iliyoripotiwa katika gazeti moja na ambayo pia inasambaa mitandaoni.

Kwa kifupi, wanatakiwa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria na sio kufuga hivi hivi. Taarifa hii imetolewa na Dr. John Kaijage ambae ni Mtafiti Mkuu na Mratibu wa ufugaji wa kuku katika Wizara ya Kilimo na Mifugo.

Habari ndio hio.
 
Hii hapa
IMG-20201230-WA0008.jpg
 
Shida ni hii miradi mikubwa inayo endeshwa ambayo inahitaji pesa nyingi kupita uwezo wetu,

Kwa namna hali ilivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kutafuta namna ya kuwekeza nje ya nchi walau nusu ya mitaji yetu maana wakikumata umefuga kuku na haujasajiliwa basi ujue mbio zao moja kwa moja ni kwenye account za benki na kuzu ia hela ndio story nyingine zitaanza kusikilizwa huku ukipigwa danadana

SHAME ON THIS COUNTRY
 
Mbona imeanza muda mrefu huko vijijini, hauwezi kumtoa kuku sehemu 1 kwenda nyingine mpaka uripoti kwa mtendaji wa kijiji hata kama unaazima hilo jogoo kwa ajiri ya mbegu tu.
 
Back
Top Bottom