Wafungwa wa kisiasa kutoka jimbo la Ukerewe washinda rufaa yao na kuachiwa huru

Wafungwa wa kisiasa kutoka jimbo la Ukerewe washinda rufaa yao na kuachiwa huru

CHADEMA kanda ya Victoria na taifa inaomba wana CHADEMA na waTanzania kwa ujumla kuwaangalia hawa makamanda ili waweze kupata huduma za kiafya baada ya kutoka gerezani na sasa wapo huru.
Mungu wa Mbinguni ahimidiwe milele amina.

Tutawachangia hawa binadamu wenzetu
 
Mengi sana yamebadilika.
CCM ipo kwenye hali ya umahututi.

CCM yenyewe imepitia katika hali ngumu sana, na bado haijui itatoka vipi.

Kosa litakalofanyika ni kuiruhusu tena ijiimarishe.

Iwapo bado CCM imeshikamana na vyombo vya dola, ni dhahiri itaendelea kujiona ni yenye nguvu. Kama kuna walioumia kwenye CCM, basi jua sio kama chama, bali ni makundi yaliyo ndani ya CCM. Ufahamu kundi lolote litakalokuwa kwenye kiti, litatumia jina la CCM kutawala kwa mabavu. Sasa sijui ni kujiimaeirisha kupi unaongelea.

Ni kweli kuna mabadiliko kadhaa, lakini sio ya kimfumo, bali aliyebadilika ni mwenyekiti wake, na kwakuwa utashi wa mwenyekiti ndio hufuatwa na CCM mzima, unaweza kusema ni mabadiliko. Lakini akitokea kiongozi kama aliyepita, bado CCM itarejea kwenye matendo yale ya kihayawani ya waZi. Na kwa taarifa yako uwezekano wa kupatikana kwa mwenyekiti wa aina ile bado upo sana, kwani kuna waliofaidika na tabia zile.
 
Huo uogo umetengenezwa moja ya strategy ni kufunga watu wanyee debe miaka nenda rudi bila losa lolote, extrem ilifika wakaanza kuteka, kuua na kutesa.

Na kwakuwa mbinu ile imewasaidia CCM kutawala bila rabsha, usitegemee mtindo ule kuondoka kabisa. Kitakachofanyika ni kuchekeana kinafiki wakati uoga bado upo, lakini wananchi wakionekana kusimamia haki zao bila uoga, mbinu zile za kutekana, na kubambikiziana kesi zitarejea.
 
Yaan kila jumapili utamuona makamera yanamuonyesha akiwa kanisani lakin hakua na hofu ya Mungu hata chembe

Mbinu ile ilikuwa ni kuhadaa umma kuwa ni mcha Mungu. Rejea kuwa kipindi hicho ndio viongozi wa dini waligeuzwa kuombea kila hafla ilipokuwa inatokea. Inafahamika bado watanzania ni watu wanaoamini sana mambo ya dini, hivyo dini ilitumika pia kupumbazia watu.
 
Mkuu kushindana na mtu aliyeshikilia bunduki huku ameshaikoki wakati wewe una mikono mitupu ni sawa na kumvimbia Simba dume mwenye hasira kali
Ingekuwa dhana hiyo pekee ndiyo inayofanya kazi dunia hii ingekuwa ni tofauti sana na ilivyo leo!
 
Ni kweli kuna mabadiliko kadhaa, lakini sio ya kimfumo, bali aliyebadilika ni mwenyekiti wake, na kwakuwa utashi wa mwenyekiti ndio hufuatwa na CCM mzima, unaweza kusema ni mabadiliko.
LOoo!
Mkuu 'Tindo', naona hatuelewani kabisa. Mimi sioni "mabadiliko" ya uwepo wa Samia badala ya Magufuli. Hayo siyo mabadiliko ninayolenga mimi.

CCM nzima ni "hollow" ilivyo sasa hivi. Haijalishi kundi lipi lililoshika madaraka.
 
watanzania ni watu wanaoamini sana mambo ya dini, hivyo dini ilitumika pia kupumbazia watu.

Hakika kabisa, viongozi wa dini wasiwe sehemu ya watawala maana ina aminika viongozi wa kiimani wanatakiwa kukemea maovu.

Sasa viongozi wa kiimani wakiwa ni sehemu ya utawala basi watawala wataambiwa vipi kuwa wapi wamekosea au kukiuka haki ikiwa viongozi wa kiimani / dini nao wamemezwa na mfumo wa utawala wa nchi.

The symbiotic relationship between the General Francisco Franco regime and the Church depended on both parties retaining a shared vision of each other’s role in the destiny of Spain. Each was happy to cocoon the country in a nostalgic, imperial and Catholic past.

But Franco did not let the church dictate the terms of their relationship, and Spain was in no danger of becoming a theocracy. The same Cardinal Gomá –who had favoured “divine totalitarianism“– was shocked when a pastoral letter of his, which questioned unlimited state power and favoured monitoring the regime’s religious orthodoxy, was banned. It was a sharp reminder that the Church enjoyed its privileges by the grace of Franco! ..........

READ MORE: Source : The Catholic Church after the Spanish Civil War.
 
Mpaka leo najiuliza magufuli alikuwa mtu wa aina gani? Naomba mnisaidie who was this person really?
 
LOoo!
Mkuu 'Tindo', naona hatuelewani kabisa. Mimi sioni "mabadiliko" ya uwepo wa Samia badala ya Magufuli. Hayo siyo mabadiliko ninayolenga mimi.

CCM nzima ni "hollow" ilivyo sasa hivi. Haijalishi kundi lipi lililoshika madaraka.

Unatumia kipimo gani kujua kuwa ni hollow, wakati imeendelea kushikamana na vyombo vya dola?
 
Unatumia kipimo gani kujua kuwa ni hollow, wakati imeendelea kushikamana na vyombo vya dola?
Mkuu 'Tindo', naona una maswali mengi ya udadisi tu huku ukweli ukiujua mwenyewe.

Huko "...kushikamana na vyombo vya dola" kusikutishe hata kidogo.
Leo hii CCM ikifurumishwa utaona vyombo hivyo hivyo ndio vitakuwa mbele kuinanga CCM.

CHADEMA ingeendeleza ilipokuwa imefikia na Magufuli (sina maana ya siasa za uanaharakati); ungeona jinsi nchi hii ilivyobadilika. CHADEMA wanakosea sasa hivi kuwapa CCM nafasi ya kujipanga upya. Kinana akiwa kinara wa kazi hiyo.
 
Kalamu bwana
 
Katiba ya kukaa mezani na CCM bila kutokea machafuko, usitegemee kuheshimiwa.

Katiba bora hupatikana baada ya machafuko, au nchi kupinduliwa.

Hilo ni angalizo nakupa ndugu yangu.
Mbona Zanzibar walipata katiba Yao Mkuu kwa maridhiano, nadhani watu wa Pwani Wana busara sana tatizo huwa wahafidhina ambao huogopa maslahi Yao kutapanywa.

Hata JK naamini alikua na Nia njema kuleta katiba mpya shida ni wahafidhina kama kina Wassira, Lukuvi, Sitta n.k wakateka mjadala na kutaka kupindisha mambo Ili walinde maslahi Yao!!

Maadam Nia njema ipo basi tuwe na subira kunaweza patikana suluhu kwenye mchakato huu mpya wa katiba
 
Mkuu 'Tindo', naona una maswali mengi ya udadisi tu huku ukweli ukiujua mwenyewe.

Huko "...kushikamana na vyombo vya dola" kusikutishe hata kidogo.
Leo hii CCM ikifurumishwa utaona vyombo hivyo hivyo ndio vitakuwa mbele kuinanga CCM.

CHADEMA ingeendeleza ilipokuwa imefikia na Magufuli (sina maana ya siasa za uanaharakati); ungeona jinsi nchi hii ilivyobadilika. CHADEMA wanakosea sasa hivi kuwapa CCM nafasi ya kujipanga upya. Kinana akiwa kinara wa kazi hiyo.
Iliendeleza ila Mbowe mkatishia kumfunga kwa kesi ya ugaidi, Mimi nadhani Rais akiwa diplomat hakuna haja ya kutunishiana misuli ila kwa type ya JPM kweli Mtu wa siasa za Lissu was a better fit yaani jino kwa jino.

Having said that, CHADEMA na Samia wamechagua meza kama suluhu. Kuanza kuinanga serikali wakati meza ipo wazi ni siasa za kizamani ngoja wamalizane na mambo ya tume huru na katiba utaona moto unavyowaka tena.

Hata kule Kenya unaona Odinga Yuko kimya kwa madhaifu ya Kenyatta maana ndio anamsafishia njia ya Ikulu, ila akiingia wote mtashangaa atakvyowasha moto kwa mafisadi akiwemo Kenyatta mwenyewe!!

Siasa ni kama karata Kila move inahesabiwa, hivyo ukikosea timing tu hii chance ya tume huru haitarudi milele
 
Back
Top Bottom