Wafungwa wa kisiasa kutoka jimbo la Ukerewe washinda rufaa yao na kuachiwa huru

Wafungwa wa kisiasa kutoka jimbo la Ukerewe washinda rufaa yao na kuachiwa huru

Mkuu 'Tindo', naona una maswali mengi ya udadisi tu huku ukweli ukiujua mwenyewe.

Huko "...kushikamana na vyombo vya dola" kusikutishe hata kidogo.
Leo hii CCM ikifurumishwa utaona vyombo hivyo hivyo ndio vitakuwa mbele kuinanga CCM.

CHADEMA ingeendeleza ilipokuwa imefikia na Magufuli (sina maana ya siasa za uanaharakati); ungeona jinsi nchi hii ilivyobadilika. CHADEMA wanakosea sasa hivi kuwapa CCM nafasi ya kujipanga upya. Kinana akiwa kinara wa kazi hiyo.

CDM wafanyeje labda, au wamzuie Kinana kuzunguka nchi nzima?
 
Uk̸i̸i̸s̸h̸i̸ k̸w̸a̸ u̸p̸a̸n̸g̸a̸ u̸t̸a̸k̸u̸f̸a̸ k̸w̸a̸ u̸p̸a̸n̸g̸a̸
 
Iliendeleza ila Mbowe mkatishia kumfunga kwa kesi ya ugaidi, Mimi nadhani Rais akiwa diplomat hakuna haja ya kutunishiana misuli ila kwa type ya JPM kweli Mtu wa siasa za Lissu was a better fit yaani jino kwa jino.

Having said that, CHADEMA na Samia wamechagua meza kama suluhu. Kuanza kuinanga serikali wakati meza ipo wazi ni siasa za kizamani ngoja wamalizane na mambo ya tume huru na katiba utaona moto unavyowaka tena.

Hata kule Kenya unaona Odinga Yuko kimya kwa madhaifu ya Kenyatta maana ndio anamsafishia njia ya Ikulu, ila akiingia wote mtashangaa atakvyowasha moto kwa mafisadi akiwemo Kenyatta mwenyewe!!

Siasa ni kama karata Kila move inahesabiwa, hivyo ukikosea timing tu hii chance ya tume huru haitarudi milele
EeeenHeee,

Mkuu 'zitto junior', kwanza kabla ya yote, naona jinsi lugha inavyobadilika, bila shaka kuna mambo huko yanapikwa kama tulivyohisi wengi wetu.

Haya uliyoandika hapa, ngoja niyape tafakuri, kwa maana naona makisio yetu juu ya CHADEMA na Samia yalikuwa sahihi.
Nitatafuta muda mzuri knirudi kwenye bandiko hili kwa utulivu wa akili.

Lakini tafadhari, naomba tusikoseane heshima mara hii ,kwa kutumia maneno kama haya ""iliendeleza ila Mbowe 'mkatishia'kumfunga kwa kesi ya ugaidi"
Sikumbuki ni lini hasa nilijihusisha katika jambo la namna hii!
 
CDM wafanyeje labda, au wamzuie Kinana kuzunguka nchi nzima?
Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.

Nadhani tumeelewana, mkuu wangu 'Tindo'.
 
"Nia njema" umeipima kwa kipimo gani ukajua ipo?
1. Fidia kwa Lissu na Mbowe.
2. Kuachiwa wafungwa wa kisiasa
3. Kuunda tume ya kuchukua maoni juu ya reforms za kisiasa.

Hayo yote yanaonyesha kuna Nia njema ya negotiations hizi kuzaa matunda.
 
Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.

Nadhani tumeelewana, mkuu wangu 'Tindo'.
Mbona wanazunguka, last week walikua Mbagala kusajili kidijitali na kugawa kadi za kielektroniki.

Mabaraza ya katiba yanaendelea nchi nzima wote mnaona. Sasa sijui kuzunguka kupi huko unamaanisha
 
EeeenHeee,

Mkuu 'zitto junior', kwanza kabla ya yote, naona jinsi lugha inavyobadilika, bila shaka kuna mambo huko yanapikwa kama tulivyohisi wengi wetu.

Haya uliyoandika hapa, ngoja niyape tafakuri, kwa maana naona makisio yetu juu ya CHADEMA na Samia yalikuwa sahihi.
Nitatafuta muda mzuri knirudi kwenye bandiko hili kwa utulivu wa akili.

Lakini tafadhari, naomba tusikoseane heshima mara hii ,kwa kutumia maneno kama haya ""iliendeleza ila Mbowe 'mkatishia'kumfunga kwa kesi ya ugaidi"
Sikumbuki ni lini hasa nilijihusisha katika jambo la namna hii!
Hamna lugha ilibadilika ila Hilo Mnyika alisema wazi kabisa, hata issue ya Mdee alisema maamuzi yatatokana na "negotiations" kwa Mama na sio procedure za kimahakama!!

Na alichosema ni wanachama tuwe "watulivu" huku meza ikitumika. So usitegemee Lissu au Mbowe kuanza kufanya mikutano ya kuishambulia CCM na Samia huku unataka wabunge hao hao wa CCM waipitishe sheria bungeni!!

Na hiyo haimaanishi Una surrender kwa CCM ila mnapunguza msuguano kipindi hiki Cha majadiliano maana mnahitaji utulivu na maelewano.
 
Hapana. Wazunguke naye, mlango kwa mlango. Hiyo ndiyo kazi muhimu kwa CHADEMA wakati huu, na siyo kutafuta kumwaga damu za waTanzania.

Nadhani tumeelewana, mkuu wangu 'Tindo'.

CCM wana ruzuku, na hata raslimali za serikali zinatumika kufanikisha ziara za viongozi wa CCM. Je CDM wanatoa wapi hela ya kuweza kumfuatilia Kinana kila apitapo? Vyama vikongwe vilivyo madarakani muda mrefu hasa vyenye vimelea vya kijamaa, havitoki madarakani kwa box la kura. Na ushahidi wa hilo uko wazi peupe.
 
Na alichosema ni wanachama tuwe "watulivu" huku meza ikitumika. So usitegemee Lissu au Mbowe kuanza kufanya mikutano ya kuishambulia CCM na Samia huku unataka wabunge hao hao wa CCM waipitishe sheria bungeni!!
Hivi hili la "kushambulia" linatoka wapi?

Kwani kwa CHADEMA kufanya kazi zake za kisiasa ni lazima ishambulie?

Hapa ndipo penye tatizo, na nadhani hapa ndipo palipowekwa mtego wa kuinasa CHADEMA isifanikiwe katika shughuli zake.

Mbona Kinana anafanya kazi zake vizuri tu, kwani kamshambulia nani?
 
CCM wana ruzuku, na hata raslimali za serikali zinatumika kufanikisha ziara za viongozi wa CCM. Je CDM wanatoa wapi hela ya kuweza kumfuatilia Kinana kila apitapo? Vyama vikongwe vilivyo madarakani muda mrefu hasa vyenye vimelea vya kijamaa, havitoki madarakani kwa box la kura. Na ushahidi wa hilo uko wazi peupe.
Haya sasa.
Sababu juu ya sababu, na visingizio kede wa kede!

Tutakwenda namna hii mpaka wapi, mkuu 'Tindo'!

Kwa nini tusipige vichwa, mimi na wewe kusaidia kifikra kuwawezesha CHADEMA kufanikisha haya tunayowataka wayatimize kwa waTanzania, badala ya kuendelea kutafuta vizingiti tu?

Huku mitaani, CHADEMA ipo sana kama haijasambaratika tena kwa sababu zisizofahamika.
CHADEMA wana muundo wao wa uongozi katika sehemu mbalimbali kote nchini; hawahitaji sana hizo unazozieleza walizonazo CCM kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi kabisa sehemu zote wanakotakiwa kuzifanya.

Makao Makuu pale wapo watendaji wanaoweza kuendesha programu zote nchi nzima kwa mpangilio unaoeleweka kwa kutumia teknologia iliyopo hivi leo.

Sasa naona umenizungusha vya kutosha juu ya hili. Nashawishika sasa kukuhoji wewe pia upande wako huo unaouamini kwamba ndio unaohitajika kufanyika kama Tanzania inataka kuwa na Katiba Mpya.
 
1. Fidia kwa Lissu na Mbowe.
2. Kuachiwa wafungwa wa kisiasa
3. Kuunda tume ya kuchukua maoni juu ya reforms za kisiasa.

Hayo yote yanaonyesha kuna Nia njema ya negotiations hizi kuzaa matunda.
Fair enough.
Lakini sichukulii watu kupewa HAKI wanazostahiri kuwa kama 'favor' kwao; kuwa kama sharti la kuwafunga mnyororo juu yake.
Hakuna ninapopendekeza hao waliopewa haki zao wampopoe kwa njia yoyote aliyetenda haki, lakini hapo hapo kisiwe ndicho kitu cha kuwakumbusha kama walipewa fadhira.
 
Back
Top Bottom