Waganda watoa sababu zao kwanini watakomaa na SGR ya Kenya na sio ya Tanzania

Waganda watoa sababu zao kwanini watakomaa na SGR ya Kenya na sio ya Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Waganda wametoa sababu zao kwa nini imewalazimu kuegemea upande wa SGR ya Kenya zaidi ya ile ya Tanzania inayotegemewa kujengwa.
Naomba hii mada tuijadili kitaalam kwa kudadavua taarifa neno kwa neno.

Urefu
Kenya - 1,250KM
Tanzania - 1548KM (1228Km kwenye ardhi na 320km kwenye maji)

Uwezo wa mizigo
Kenya - kontena 8640 kwa siku maana ina uwezo wa treni 40 kwa siku kila moja ikiburuza kontena 216
Tanzania - kontena 216 kwa siku kwa ajili ya mapungufu na changamoto nyingi kuanzia bandarini na kwenye ziwa Victoria

Muda wa usafiri
Kenya - masaa 24
Tanzania - siku tatu, masaa 72 kama wakijaribu sana

Vikwazo vya aina ya mizigo
Kenya - Hamna kikwazo, vyote vinaruhusiwa
Tanzania - Kuna aina ya mizigo hairusiwi kupita kwenye ziwa

Upokezaji wa mizigo
Kenya - Hakuna changamoto, ni moja kwa moja
Tanzania - Bandari ya Mwanza na Port Bell, pale inabidi meli zitumike tano kuvusha mizigo ya treni moja

Uwezo wa bandari
Kenya - Bandari ya Mombasa ni kubwa mara tatu zaidi ya Dar, na bado kuna uboreshwaji unaoendelea
Tanzania - Bandari yao bado sana

Mizigo ya sasa
Kenya - Uganda inasafirisha mizigo tani milioni 10 kupitia Mombasa
Tanzania - Uganda inasafirisha tani milioni 0.5 kupitia Tanzania

Ukaribu wa soko kuu
Kenya - Ipo karibu ya Suez Canal
Tanzania - Ipo mbali sana na Suez Canal

Uhakika wa kukamilisha
Kenya - Imekanilisha Nairobi - Mombasa 472KM na tayari ujezi umeanza kwa eneo lililosalia ikiwemo upatikanaji wa pesa
Tanzania - Wametia saini mkataba wa ujenzi wa Dar - Morogoro 205KM, bado wanasaka hela kwa ajili sehemu iliyosalia, na pia bandari za Mwanza na Port Bell itabidi zijengwe upya na ununuzi wa meli aina mpya.

Hizo hapo ni baadhi ya sababu, kuna mengine mengi nikipata fursa nitaendelea kuyajaza humu.

Kwa wasomaji hodari great thinkers naomba muifuate ripoti kamili hapa https://sgr.go.ug/downloads/SGR_comparison_of_Kenya_Tanzania_Ethiopia_Uganda.pdf
 
That's from layman's head mtu kajikalia chini ya mwembe kavimbiwa na githeri na kuja na hizi hekaya,

Sina utamaduni wa kujadili vitu kutoka kwa mtu wa aina hiyo

Taratibu kaka, haya yote yametokana na tovuti ya serikali ya Uganda iliyozinduliwa kwa ajili ya SGR, sio kila kitu ni fadhila, kuna mengine inabidi wazingatie mahesabu ya kitaalam.
 
That's from layman's head mtu kajikalia chini ya mwembe kavimbiwa na githeri na kuja na hizi hekaya,

Sina utamaduni wa kujadili vitu kutoka kwa mtu wa aina hiyo

Hahahaha! Duh!

Mahindi iko wapi kwa sasa ya mtu kupika githeri?
 
Taratibu kaka, haya yote yametokana na tovuti ya serikali ya Uganda iliyozinduliwa kwa ajili ya SGR, sio kila kitu ni fadhila, kuna mengine inabidi wazingatie mahesabu ya kitaalam.
Tokea lini imezinduliwa hiyo ni scam don't take the domain go.ug for granted

You need some security certificates for it to be trustworthy on Internet community and only government could provide such confidentials sasa makanjanja wamejiundika kawebsite uchwara kuja kutishia watu hapa.
 
Mk254 unaanza kuishiwa hoja sasa, hii mada haina mashiko. Kwani Waganda wakipelekewa miundo mbinu mpaka mlangoni kwao (iwe ya Kenya au Tanzania) watakataa?
 
Mk254 unaanza kuishiwa hoja sasa, hii mada haina mashiko. Kwani Waganda wakipelekewa miundo mbinu mpaka mlangoni kwao (iwe ya Kenya au Tanzania) watakataa?

Huko wapi unakwenda kutokea, hamna mlango wa nje, rudi kwenye mada.
 
Taratibu kaka, haya yote yametokana na tovuti ya serikali ya Uganda iliyozinduliwa kwa ajili ya SGR, sio kila kitu ni fadhila, kuna mengine inabidi wazingatie mahesabu ya kitaalam.
Ndugu unapotea sasa. Je, hivi nyie kenya mnamatatizo gani? Yaani mnajiundia domain ya kwenu na kiita ya serikali ya Uganda. Ama kweli Kenya tumewashika pabaya sana.
Wewe jamaa nimeanza kukudharau sasa.
 
Huko wapi unakwenda kutokea, hamna mlango wa nje, rudi kwenye mada.
Ndio hicho najaribu kutafuta sikioni, mada iko wapi hapa? Ikiwa mmeshidwa kuwahakikishia waganda kama kilichotokea 2007-08 mpaka wakapata hasara hakita tokea 2017 unategemea Uganda wata kuja kuwaamini tena? Swali langu lilikuwa dogo tu tena hiyo ndio ingekuwa mada "Waganda wakipelekwa miundo mbinu mpaka mlagoni kwao, iwe kupitia Kenya au Tanzania, wataikataa?"
 
Taratibu kaka, haya yote yametokana na tovuti ya serikali ya Uganda iliyozinduliwa kwa ajili ya SGR, sio kila kitu ni fadhila, kuna mengine inabidi wazingatie mahesabu ya kitaalam.
Mnaongea hata msivyojua. Coalition of the willing [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Ndugu unapotea sasa. Je, hivi nyie kenya mnamatatizo gani? Yaani mnajiundia domain ya kwenu na kiita ya serikali ya Uganda. Ama kweli Kenya tumewashika pabaya sana.
Wewe jamaa nimeanza kukudharau sasa.
It is a genuine Uganda govt Sgr portal...

SGR Uganda
 
Back
Top Bottom