Uchaguzi 2020 Wagombea CCM wakwama kufanya kampeni

Uchaguzi 2020 Wagombea CCM wakwama kufanya kampeni

Mimi sina chama ila nikiangalia Ccm inapendwa sana na Magufuli huyu Watanzania wanampenda sana

Kila nikiuliza mtu anasema atapigia Magufuli kura
Kama unaishi Tunduru nategemea kupata jibu gani?
 
Mimi sina chama ila naona wagombea wa CCM wana nafasi kubwa ya kushinda
hata wasipopiga kampeni kutokana na kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli
Wanaweza kupita bila kupiga kampeni kwa kubebwa na DEDCCM, TUMECCM, POLICCM N.K
 
Mimi sina chama ila nikiangalia CCM inapendwa sana na Magufuli anapendwa sana na Watanzania
Kuna kila dalili kuwa CCM itashinda sana
 
Mimi sipo kwenye mambo ya siasa kaka yangu
Ila Rais Magufuli anapendwa sana na Watanzania
 
Hivi kuna nchi nyingine duniani ambako mmoja wa wagombea wa urais anateua tume ya uchaguzi? Hiki ni kitu kinafanya tudharauliwe sana duniani.

Uhuru maana yake ni nini? Sio uwezo wa kujiamulia mambo yetu wenyewe? Mbona hatuna uwezo wa kuamua ni nini ndiyo kiwe katiba yetu? Watanzania tumeporwa uhuru wetu?

Tulidharauliwa sana wakati tunatawaliwa na Waingereza. Na sasa tunadharauliwa sana wakati tunatawaliwa na ccm. Bado sisi siyo watu huru. Tunaweza kujikomboa, itabidi tujikomboe. Tukatae ccm na wanyapara wake
 
Kama ndivyo kulikuwa kuna haja gani ya kutumia fedha za umma kuwakodisha Wasani lukuki? Watadai ni fedha za chama lkn si kweli.

Ukweli uko wazi maendeleo ni ya watu siyo ya vitu. CCM imechokwa na hata yenyewe imejichokea kwa sasa ni nguvu ya Dola na Tume ya Uchaguzi ndiyo tegemeo lao kuu.
Acha sound wewe, ccm watumie hela za umma kufund kampeni zao bwana lissu mtaalam wa sheria kuliko watu wote duniani awe hajalisemea. Huenda inauma lakini ccm wana hela aisee. Niko msalala kabla ya kampeni kuanza ccm walitangaza kuhitaji milion 250 kama fund za kuendesha mchakato wa kampeni ndani ya wiki mzigo ulikuwa umechangwa na wadau na wengine wanaomba kuongezea hapo ni wilaya moja tu kama ilikuwa program ya nchi nzima unadhani walikusanya kiasi gani? Jumlisha vitega uchumi vyao, michango ya wapenzi na wanachama mmoja mmoja nk.. Tusiwe tunapenda kujiliwaza, ccm ina pesa
 
Duu! Your statement is a serious parradox! Hapa unasema wamekatishwa tamaa kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura inayojitokeza, Lakini tena unasema wana uhakika wa kushinda uchaguzi! Hapa lazima kuna walakini!
 
Back
Top Bottom