Waha /Abaha ni Wanyarwanda?

Waha /Abaha ni Wanyarwanda?

Me kama Muha wa kigoma naomba Paul Kagame atuchukue tu[emoji855],,CCM wakitoka madarakan aturudishe TZ.

Unaruhusiwa kwenda uone kama utaweza hata kutoka ukiingia humo
 
Ndio maana mr slim mizuka yake ikipanda huwa anapiga mkwara kigoma ni sehemu yao na ipo siku akiamua kuliamsha dude hatasita kufanya hivyo kuichukua sehemu hiyo.

Unaweza ukatupatia ushahidi kama kuna siku alidai eneo la kigoma ni lake??

Kigoma iko karibu na burundi kuliko rwanda
IMG_1251.jpg
 
Waha na Wahutu ni wale wale tu. Migawanyiko ya ukoloni ndio imesababisha yote hayo. Ni sawa na Watusi na Wahangaza wa Ngara.

Wahangaza wa ngala si watusi

Watusi walio wengi ni warefu
Wahangaza wengi n wafupi

Yawezekana walitoka rwanda lakini si kutoka kabila la watusi
 
Hiki ni kilugha gan mkuu,,, mbona lugha hii unaielewa ww na wenzio tu
Nafikiri hayo ni majina ya maeneo. Mfano, Omurshaka ni kituo cha daladala ya magari ya kwenda, sijui Benaco? Nakumbuka, miaka ya hivi karibuni nilipokuwa Karagwe, nilipandia gari hapo stendi ya Omurshaka hadi Benaco (kama sijakosea), kisha gari jingine hadi Ngara.

Ni majina ya maeneo.
 
Ignorance ni kubwa Sana Tz..
Ina maana hakuna anaejua kuwa wakati Ujerumani wanatawala Tanganyika...Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanganyika??
Waliposhindwa vita Ujerumani ndo Waingereza wakawapa Belgium...Rwanda na Burundi...

Halafu kulikuwa na kambi za wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi miaka ya 60...hivi ambapo karibu wakimbizi wote walihamia Tz kimoja..
 
Sasa kwanini watu wa kigoma utasikia
Wanaambiwa nyie ni warundi tu
[emoji1] huoni kama tunaitoa kigoma wenyewe

Ova

kwasababu wako karibu na nchi yenye machafuko ! Lakin huwezi kusikia tukiwambia wajaruo ni watu wa kenya au wamakonde ni watu wa msumbiji.

Ni rahisi kumtolea mtu mfano mbaya kuliko mzuri hasa kwene malumbano
 
Ni ujinga wa waafrika kugombania makabila. Haya makabila yapo kote na yana muingiliano sana. Wamasai wapo Kenya na TZ. Waha, warundi na wanyarwanda ni kitu kimoja. Waluo wapo Kenya na TZ, Wanyakyusa wapo Malawi na TZ. Wangoni wametoka kusini. Kuna jamii kama wameru/wairaq huko Eritrea na Ethiopia. Jina lenyewe Tanganyika chanzo chake ni Congo yani TZ yote ilibidi iwe Congo. The list is endless. Hamna kipya hapa.
 
warundi pia wanaongea lugha ileile ya rwanda. hivyo inawezekana ni kweli, watu wote wa burundi, rwanda, kigoma ni walewale tu ila hiyo haimaanishi kwamba ni wanyarwanda, kwasababu makabila yote ya mipakani yapo pande zote mbili za nchi zilizoko mipakani. hao wameru wa arusha na wamasai hata kenya wapo hivyo hivyo, hao kina mwita hata kenya wapo kwa majina na tamaduni hizo hizo, hao wajaluo, hao wahaya na uganda wanaendana vilevile, hao wanyasa wa malawi na wanyasa wa tanzania ni wale wale hadi kuna kipindi wanyasa wa malawi walikuwa wanataka kujitoa malawi wawe watanzania kwa sababu wanatengwa, wamakonde wapo msumbiji na mtwara, na wayao pia, wazigua wapo tanga na kenya pia. wachaga na wakenya wametenganishwa na mlima tu. kwahiyo kama yeye anasema kigoma ni rwanda hata sisi tuna haki kusema Rwanda ilikuwa Tanzania na tunaweza kuichukua kama vipi.

Word.
 
Back
Top Bottom