Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Usifananishe mfumo wa elimu wa ulaya na marekani, huko mfumo wao ni wa elimu bora wakati sisi mfumo wetu ni wa bora elimu. Waliosoma kabla na mpaka miaka michache baada ya uhuru waliuonja mfumo wa elimu ya ulaya ambapo mwanafunzi aliyemaliza darasa la nne alikuwa na uwezo wa kuajiriwa! Hii ilitokana na elimu kuzingatia sana mwanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, bila kujua kimojawapo utarudia darasa, wao wamewekeza sana elimu ya msingi wakati sisi tunawekeza elimu ya sekondari! Ni vigumu mtu mzima kuelewa masomo kuliko mtoto. Kutokana na hali hiyo ya mfumo wa elimu bora mwanafunzi anamaliza kidato cha sita anauwezo mkubwa sana kielimu hivyo anaingia chuo akiwa na uwezo wa kujitawala binafsi kielimu ndiyo maana wenzetu wakotayari kuishi popote duniani ili afanye utafiti hata kusiko na umeme wakati sisi ikifika saa kumi jioni tunaanza kustarehe! Pia hayupo anayeweza kwenda kijijini peke yake kwa ajili ya kufanya utafiti. Nakushauri mleta mada na wenzako wa aina yako kwanza mjue huko ulaya kuna wahadhiri wazee zaidi ya hao mnaowatukana na wanaheshimika sana kuliko nyie vikaragosi vinanyokesha kwenye mitandao vikichati na mademu. Wewe ulidisko sasa unatapatapa kujihami, it is too late, tafuta bodaboda ili maisha yaendelee.Hii naungana nawe. Japo si wote,wengi ni wajinga tena wenye roho mbaya. Nakumbuka wenzetu Makerere huwaita PhD or Pull Him/Her Down profs. Hata hivyo, msikonde, vitakufa kimoja hadi kingine. Hivi ndivyo vinakwamisha vijana wetu. Utajifisiaje kufelisha wakati Ulaya au Marekani ikitokea hivyo unachunguzwa na kupewa onyo. Nadhani vyuo vyetu vijenge utaratibu wa kutathminiana ambapo wanafunzi, anonymously wanamuevaluate prof na prof anawaevaluate.