Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Vyombo vya Kamati ya Usalama Wilaya ya Rombo vimewakamata wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya Kenya ambao wameingia Nchini bila kufuata utaratibu kwa maana ya hawakupitia boda iliyo rasmi na hawakuwa na nyaraka zozote za kiuhamiaji
Wamekamatwa kupitia msako halali, na imeelezwa walikuwa watu 26 ambapo kati yao wanaume ni watatu na wanawake ishirini na tatu
Baada ya kukamatwa, wahamiaji hao walifikishwa kituo kikuu cha Polisi cha Rombo. Wakiwa hapo wamefanyiwa upekuzi pamoja na kuhojiwa
Pia wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Rombo na wamekutwa na hatia baada ya kukiri makosa yao. Wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya 500,000
======
MYTAKE
Hii wanalipa gharama za wale wa Bodaboda! next watalipa gharama ya kuzuia Mahindi!
CC: Tony254