Chokochoko mnazitafuta wenyewe, Mambo yakishaharibika mnaanza kuwasingizia WAPINZANI.
Wale wahamiaji haramu wa Ethiopia mbona waliachiwa bila masharti yoyote?
Unadhani Ni taifa lipi litafurahi raia wake wakionewa?
Hao wafugaji bila shaka Ni jamii ya wamasai, wamasai wapo Kenya na TANZANIA miaka na miakaa na hawajuagi kabisa habari za mipaka ya kimataifa.
Na tumekua tukiwachukulia hivyo miaka na miaka, Kwa maana Ni ndugu zetu pia.
Sasa hivi Ni visasi visivyo na msingi,
Mkiendelea hivi na kesho mtakuja kusema na wanyamapori wanaovuka kutokana Kenya kuja Tz wataifishwe au wachomwe Moto kwa kuvuka kinyemela
Kiukweli, watanzania tusifike huko.
Usichopenda ufanyiwe, nawe usimfanyie mwenzio.
Sio tu wee kidogo TU ukiguswa unataka mkae meza ya maridhiano.
Kama mtanzania mzalendo,
Siafikiani kabisa na hizi chokochoko zinazoendelea dhidi ya ndugu zetu wakenya.