Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukisha maliza kutafakari haya na kutambua kwamba hizi ni peremende tu kwa watoto watukutu wanaojiliza kila mara; tafuta nafasi utuletee taarifa kuhusu uhujumu mkubwa anao wafanyia waTanzania na mali za taifa hili.
Kwa mfano: msihi atambue kuwa waTanzania wanao uwezo mkubwa zaidi wa kufanya mambo yao ya maendeleo bila ya kutegemea waletewe maendeleo na watu wake toka huko Arabuni. Misitu na mapori waTanzania wanayamudu vizuri sana, hakuna sababu ya kugawa raslimali kama hizo kwa hao anaoamini watatuletea maendeleo.

Kwa ufupi tu ni hivi: Mwambie kuwa waTanzania siyo wavivu, siyo wezi, n.k..; wanachotaka ni uongozi tu mzuri wa kusimami shughuli zao za maendeleo, basi.
 
Hongera Sana
Wakandarasi kwa Jambo hli kubwa,

Kama nawaona wafuasi wa chadema wanavyotoa macho, Mimi nakwambia nyie michadema hata kura mia tano nchi nzima hampati mwakani tutawanyoosha na siasa zenu za KIBAGUZI hzo.
 
Mbona umekasirika " Wahandisi" fani ya Shujaa Magufuli kumnunulia Chopa Mpendwa Wetu Mh Rais Samia?
Wewe nyakati nyingi huwa ni kinyago sana. Kama umeona "nimekasirika", ni sawa kwani hakuna cha kufurahisha katika maswala ya namna hii yanayohusu nchi yetu. Unakwenda vitani huku ukichekacheka?
 


Kiusalama hili jambo halikubaliki, ni hatari, hao wakandarasi hawajui kabisa wanaongea nini, huwezi mnunulia chombo cha usafiri atumie, iwe chombo cha usafiri majini au ardhini au angani, Mh. Rais ana vigezo vikubwa ya ulinzi na usalama wakati wa kununua vyombo hivyo vya usafiri..!!

Kwanza ni hatari sana kwa mtu au taasisi binafsi au kikundi cha watu kumnunulia Rais wa nchi chombo cha usafiri alafu unamwambia atumie, una nia au lengo gani, nani kakutuma, uliona nani kafanya jambo hilo duniani kote Rais anunuliwe chombo cha usafiri atumie? Urais ni taasisi kuu ya nchi, sio jambo la kukurupuka sbb unampenda au kumuunga mkono unaweza mnunulia hadi gari au helikopta au ndege alafu umwambie itumie, chukua, unaleta mashaka makubwa tena ya hatari sana kiusalama.

Hawa wakandarasi wanaweza changia labda kampeni ya Mh. Rais kwa namna nyingine, ila sio hili la kununua chombo cha usafiri kwa Mh. Rais, najua hili watapigwa stop haraka sana na hawatarudia kuongelea tena na nina uhakika hakuna mtu kawatuma wafanye hivi, na wao wameamua tu bila kufikiri kiundani zaidi.
 
Wewe nyakati nyingi huwa ni kinyago sana. Kama umeona "nimekasirika", ni sawa kwani hakuna cha kufurahisha katika maswala ya namna hii yanayohusu nchi yetu. Unakwenda vitani huku ukichekacheka?
Kwani hao Wahandisi nchi hii siyo yao?

Acheni Demokrasia ichukue mkondo wake🐼
 
Waarabu wamekuwepo hapa siku nyingi kabla ya Samia na ndio wamewajengea bwawa la Nyerere.

Maneno Yako meengi hayasiadiii wanavujiji kuondokana na umaskini ila hao hao unowaita Waarabu wake ndio wanakuletea pesa.

Maendeleo uliyojiletea wewe Yako wapi?
 
Wewe ni underage? Huu ni ujinga wenyewe tulionao kama nchi. Hata Gen Z nyuma Yao Kuna organizers ambao ni watu wazima kabisa. Hawajiendei hivi hivi.
Hivi hela za hayati sabodo ndo zliliwa na top layer wa chadema duh
 
Unataka kujuwa maendeleo yangu...? Nikuhakikishie tu kwamba sina tatizo kwa upande huo.

Waarabu sasa wanahaha sana kwa kutambua kwamba nchi zao ziko mashakani sana baada ya mafuta. Ndiyo maana wanawatafuta kwa kila njia, watu vilaza kama 'Chura Kiziwi', viongozi wasiokuwa na uchungu wowote juu ya nchi wanazo ziongoza. Huyu hana lolote linalo muumiza akilini kuhusu maisha duni anayo pambana nayo mTanzania, na hasa mTanganyika huko vijijini. Ndiyo maana yuko tayari kunadisha kila raslimali ambayo ingeweza kuwasaidia watu hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…