Mianya ya Rushwa kubwakubwa baina Chawa wasomi na wafanyabiashara wanapojipendekeza katika siasa za Tanzania.
Matokeo yake umoja usio na afya wa kipigaji katika serikali na wakandarasi kuongeza bajeti ya miradi ya ujenzi ili fedha hizo za ziada ziende kugharamia shughuli za kisiasa za chama dola kongwe CCM.
Muungano huu wa TUCASA na CCM haukubaliki kabisa, kwa sababu unatengeneza mianya ya ufisadi, rushwa na matumizi ya ziada kugharamia chama cha kisiasa
TUCASA ni nani ni Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA)
TOKA MAKTABA :
KAZI ZA UJENZI ZIFANYIKE KWA UBORA NA UZALENDO - DKT. BITEKO
28TH JUNE, 2024
KAZI ZA UJENZI ZIFANYIKE KWA UBORA NA UZALENDO - DKT. BITEKO
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amewataka makandarasi nchini kutekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora na uzalendo mkubwa ili wainue uchumi wa nchi na kuhakikisha unashikiliwa na Makandarasi wazawa.
Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 28 Juni, 2024 alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi lililoandaliwa na Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA) jijini Dar es Salaam.
Vile vile, amewataka kuheshimu matumizi ya fedha za miradi, kwa kufanyia shughuli za ujenzi, na faida watakayoipata kuiwekeza na kutunza kampuni zao.
Aidha, ameielekeza Wizara ya Ujenzi kuweka mkakati wa kuwainua makandarasi nchini na kuhakikisha unatekelezwa ipasavyo kuanzia ngazi ya Wizara ya Ujenzi yenyewe pamoja na Wizara ya Fedha kisha kuendelea na mazungumzo na mabenki ili kuja na mpango mzuri wa kuwawezesha makandarasi kimtaji.
Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu itaelekeza sekta zingine zikiwemo Nishati, Maji, Uchukuzi, kuhakikisha zina wabeba wakandarasi wazawa; pamoja na kuziwekea malengo ambayo kila mwaka kwenye mkutano wa makandarasi unapima utekelezaji wa malengo hayo.
Aidha, amewataka kuiga mfano kutoka Wizara ya Kilimo ya BBT, Wizara ya Ujenzi iwasaidie vijana kuanzisha makampuni na kuwapatia kazi ndogo ndogo ili kuwajengea uzoefu.
Dkt. Biteko pia amesisitiza kuwa, serikali imeendelea kuwachukulia hatua watumishi wote wa umma wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Dkt. Biteko amesema, katika mpango mkakati wa kukuza makandarasi wa ndani, kumewekwa kipangele cha kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo kunatengwa asilimia isiyopungua 20 kwa ajili ya makandarasi wa ndani.
Dhamira ya Mhe Rais ni kuwajengea uwezo makandarasi wazawa na ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa Serikali pamoja na watumishi wa ngazi zote kuhahakikisha wanatekeleza agizo lake la kuwakuza na kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza miradi mikubwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza Wizara kupitia Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imefanikiwa kuanzisha mpango mahsusi wa kuwashirikisha Mahandisi vijana kupitia miradi ya ujenzi ili kuwajengea uwezo zaidi katika miradi inayoendelea ya ujenzi ambapo hadi sasa, vijana waliopitia program ya SEAP ni 12,772 na wanao endelea nayo ni 3,317.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara imetenga miradi ya Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 120 za lami ambazo zitashindanishwa kwa Makandarasi wa ndani pekee pamoja na kutoa kipaumbele kwa Makandarasi wanawake ambapo imetenga kilometa 20.
Naye, Mwenyekiti wa TUCASA, Samwel Marwa, ameiomba Serikali iwe mlezi kwa TUCASA ili kuwajengea uwezo wa kufanyakazi na kusimama wenyewe. Pia ameiomba Serikali kuendelea kupambana na rushwa ili kuifanya TUCASA kufanya kazi kwa weledi na kupata faida katika majukumu yao.
14 July 2024
TUCASA CONTRACTORS DAY 2024 - PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY (PPRA) "Bi.Winifrida Samba"
View: https://m.youtube.com/watch?v=k8jHlYQmhGI
In a panel discussion, Ms. Winifrida Samba from the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) elaborated on the significance of the Public Procurement Act of 2023, highlighting new policies implemented by PPRA.
She discussed the enhancement of accountability mechanisms within procurement processes to ensure transparency and responsibility for public officials and service providers.
By implementing an electronic bidding system, PPRA aims to foster greater competition and facilitate the participation of small and medium-sized enterprises (SMEs).Additionally, the evaluation and awarding process of contracts has been streamlined to guarantee fairness and efficiency.
Recognizing the vital role of SMEs in economic growth, PPRA has introduced policies to support their involvement in government procurement, ensuring they have equal access to opportunities.PPRA has established robust quality assurance measures to ensure public projects deliver maximum benefits while maintaining cost-effectiveness.
The authority has also embraced digital transformation by introducing systems that streamline processes and enhance transparency.
To support compliance, PPRA provides online resources and guidance, promoting accessibility and transparency. Training programs and workshops are conducted to enhance stakeholders' understanding of procurement laws and best practices, fostering sustainable strategies to ensure accountability in public services and procurement processes.
Rigorous systems for auditing and controlling public expenditure have been established to maintain efficiency and transparency.Ms. Samba also emphasized the importance of promoting local contractors and suppliers. PPRA has prioritized local contractors in government projects, aiming to boost the local economy.
To help local contractors meet project requirements, PPRA offers capacity-building programs that enhance their technical and managerial skills. Financial support mechanisms, such as favorable financing terms and guarantees, have been introduced to help local contractors secure funding for large-scale projects.
Furthermore, PPRA encourages joint ventures between local and foreign contractors to facilitate knowledge transfer and experience sharing. Robust monitoring and evaluation frameworks have been implemented to ensure local contractors adhere to project specifications and deliver quality work.
By involving local contractors in government projects, PPRA ensures that communities benefit directly from public spending, fostering a sense of ownership and responsibility.
These measures demonstrate PPRA’s commitment to supporting local contractors, fostering economic growth, and ensuring that public procurement contributes to the overall development of the country.For more detailed information on PPRA's initiatives and policies, please visit their official website: PPRA Website