TAARIFA HII IMEKANUSHWA NA TEF. Zaidi soma Jukwaa la Wahariri Tanzania lakanusha kutoa tamko dhidi ya CHADEMA
----
Katika hatua isiyo ya kawaida, wahariri na waandishi wa habari wamesusia shughuli zote za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kauli tata ya Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Tundu Lissu.
Akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Lissu aliwataja waandishi wa habari kama "watu wasio na akili" na kuwaita "maadui wakubwa wa maendeleo," jambo lililosababisha hasira na taharuki miongoni mwa wadau wa tasnia ya habari.
Kutokana na kauli hiyo, waandishi wa habari na wahariri wameeleza kusikitishwa kwao, wakisema matamshi hayo ni kudhalilisha taaluma yao na kuhatarisha uhuru wa vyombo vya habari.
Hatua yao ya kususia shughuli za CHADEMA inaashiria msimamo thabiti wa kutetea heshima na uhuru wa vyombo vya habari nchini.