Status
Not open for further replies.
Kinachofanya tuwafatilie ni habari zao Chadema,Leo hii wakigoma habari zao zitadoda.Nani asiejua waandishi wengi wa habari hawaandiki habari za CHADEMA?Media zinazojitambua kwa sasa ni JF na JAMBO TV ONLINE na kwa mbaaali Mwananchi.na sidhani kama hawa wanaweza kugoma
 
Waandishi hao,wamekuwa na njaa Kali sana.
Wengi mfano Mbeya wamefia kwenye magari ya STK , wakitoka kufanya kazi za CCM bila ujira,na kuacha wajane na yatima,
 
Hao waandishi wa habari wanasusia nini wakati hawjahi hata siku moja kuandika au kutangaza habari za CHADEMA? Ungesema wamesusia tena ningekuelewa. Mara ya mwisho kuona habari ya CHADEMA kwenye TV au gazeti ilikuwa lini?
 
Lissu hafai kuwa kiongozi hata wa nyumba kumi. Yule anafaa kuwa Mwanaharakati wakujitegemea akiwa chini ya Mabeberu.
Wewe ndiye unafaaa inatosha.
 
Reactions: UCD
Wanajitekenya tuu. Utandawazi haujitaji hayoo makaratasi
Hivi nani ananunua magazeti zama hizi? Kwanza ni lini hao wahariri wameripoti mazuri ya CHADEMA Hilo la kususia halina impact yoyote kwasababu walikuwa wanaandika mabaya tu hivyo hata wakikusia wasusie tu maana tunajua mabaya watayaandika Yale mazuri wataendelea kuyaacha kama kawaida.
 
Wahariri Wamechelewa kutoa tamko

Siku Lisu alipokutana na wahariri alitukana waziwazi mmoja wa wahariri alipomuuliza swali

Ilitakiwa toka siku ile watoe tamko la kutompa ushirikiano

..bora wahariri wasusie.

..kwasababu huwa wanawaandika vibaya Chadema.
 
Huo ndiyo ukweli.


Kwa ujumla hatuna waandishi wala vyombo vya habari Tanzania, bali vinavyoitwa vyombo vya habari, vimejaa machawa wanafiki ambao wanasubiria kujazwa matumbo yao na mafisadi ya CCM.


Hakuna haja ya kuwaomba radhi. Kuacha kuripoti mambo ya CHADEMA litakuwa ni jambo la heri, maana wao huwa wanaripoti negatively, na siyo kufikisha ujumbe wa CHADEMA kwa umma.

Mitandao ya kijamii kama JF, online TV kama Jambo TV, wanachosha.
 
Balile hamna kitu.
TEF inatakiwa kuongozwa na watu aina ya mzee Makunga (chief editor mstaafu wa Mwananchi), Jesse Kwayu. watu smart. TEF wana mamlaka yapi kwa wanahabari.
 
Mkiacha kutumika kama chawa au mtakapo kataa kufanya majukumu yenu kwa maelekezo kutoka juu na kwa upendeleo kupendelea mamlaka yenye kukamatia makali mtaistahili heshima mnayoililia hapa na Watanzania watawathamini.Na hili mtafanikiwa tuu,kwa kukataa miongoni mwenu kutumiwa kama chawa wa wanasiasa ama chawa wa watawala.
 
Balile mtu mjinga sana huyu, aliwahi kutaka kuniharibia kibarua changu kupitia gazeti lake kwa kupewa 500K na mtu aliyekuwa na personal issue na mimi. Nimeweka nadhiri ipo siku kama siyo yeye basi kizazi chake, nitawalipa inkind.
Unakosea sana kizazi chake kuwa inclusive.
Kuna mambo mengi tunafanya for personal benefit & not family benefit even scriptures teach us to be harmony & dispair dignity for generations.

Malizana na Balile achana na generation yake maana hata hiyo 500k possibly ilifanya asilale nyumbani na kuleta taharuki ndani ya family, it was a loss. Tupendane tuache tabia ya visasi & good enough unaendelea vizuri, you're thoroughly enjoy the life with your good family.
Mungu akutunze na Daima uwe na Neema ya kusamehe ( forgiveness)
 
Yes, kwa sababu yeye pia aliyaka kuniangamiza mimi ni kizazi chake. Hiyo 500K aliichukua kwa manufaa yake na kizazi chake. Nothing more, nothing less. Hata nikishindwa mimi nitawaeleza wanangu wahakikishe hawalisahau jina la huyu mtu na uzao wake.
 
Watu wengi wenye akili zao hawasomi tena magazeti ya bongo, hawaangalii taarifa za habari kutoka tv za bongo kwani huko kumejaa uchawa na sio habari tena. Habari zemabaki kwenye mitandao tu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ