Nadhani ni suala zima la mazingira zaidi Kwa maana kinachofanya watu wa maeneo Fulani waonekane wana akili kuliko Kanda zingine
Nimesoma na wamakaonde, wayao, wazaramo, wachaga ,wahaya ,wanyakyusa, wamburu, wamasai ,wangoni na makabila mengine
Kidato cha kwanza mpaka nne nimesoma na wamakaonde,wamwera,wayao ,wanyakyusa , na makabila mengine ya kusini pamoja na ukanda wa pwani nikiwemo mm mwenyewe, shule ya sekondari chidya ,
Advance nimesoma na wachaga wengi, wamburu, wajita na wasukuma wengi pamoja na wamasai huko kaskazini
Chuoni nimesoma na wakerewe,wahaya ,wachaga ,wapemba ,wahindi ,wakenya ,wabotswana na wamakaonde
Kwa experience niliyoipata, ishu kubwa ni mazingira Wala hawana upekee wa akili
Kuanzia advance mpaka chuoni nimeona wachaga na wahaya ,wasukuma,wakurya,wajita na wengineo wakifeli na wengine wakifanya vizuri
Hili suala wanaojadili hua wanakwepa sana kipengele cha athari ya ukoloni na wamisonari , kua walijenga shule maeneo hayo Kwa wingi hivyo kuwapelekea wenyeji wa maeneo husika kua na access elimu ambayo ndio inatumika kama kigezo cha kupima akili za watu.
Overall, uwezo wa akili za watanzania unakaribiana Wala haujaachana sana