Wahenga wa kike: Mnakumbuka nguo za redimedi, sare sare, moka bila kisahau fukufuku

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] halafu usikute bazee la blue
Nakumbuka kulikuwa na vitambaa fulani vyepesi, unashona kwa kuchanganya, blauzi ya maua, suruali rangi moja...halafu unaachiwa na kakitambaa kwaajili ya kimtandio πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Yaani kama mhindi vilee.
 
Siku moja mama kaninunulia gauni zuri ila viatu hajanunua.

Ilikuwa IDD nikaenda masjid vizuri nilivyorudi Nimefika mlangoni tu nikaanza kulia kwa sauti[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Nililia kama saa moja hivi akaja kunipiga maana pesa hana nikaongeza kilio, nikagoma kunywa chai, kila anachonituma nakataa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ananipiga tena nikalia hadi nikasinzia pale pale mlangoni.


Nikaamka kama saa tano hivi nikaanza kulia tena, akawa kachoka kunipiga akaanza kujifuta machozi na yeye. Akaenda sijui kukopa wapi akanipa pesa nikanunue viatu[emoji23] [emoji23] [emoji23]


Ilibidi pilau lisipikwe na kwangu haikuwa shida ilimradi skuna nimepata[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nakumbuka kulikuwa na vitambaa fulani vyepesi, unashona kwa kuchanganya, blauzi ya maua, suruali rangi moja...halafu unaachiwa na kakitambaa kwaajili ya kimtandio πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Yaani kama mhindi vilee.
Shifoni au
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Kwako kuvaa ilikuwa bora zaidi kuliko kula.
 
Hahahaha huo sijaushuhudia au uku kwetu dongo teremka haukufika
Hahahahaha! Ungekuwa mpenzi wa nguo za kushona ungeujua.
Yaani mshono ulikuwa ukiingia, mnajikuta karibu watoto wote + wakubwa wameshona, unakuwa kama mshono wa mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…