Siku moja mama kaninunulia gauni zuri ila viatu hajanunua.
Ilikuwa IDD nikaenda masjid vizuri nilivyorudi Nimefika mlangoni tu nikaanza kulia kwa sauti[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nililia kama saa moja hivi akaja kunipiga maana pesa hana nikaongeza kilio, nikagoma kunywa chai, kila anachonituma nakataa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ananipiga tena nikalia hadi nikasinzia pale pale mlangoni.
Nikaamka kama saa tano hivi nikaanza kulia tena, akawa kachoka kunipiga akaanza kujifuta machozi na yeye. Akaenda sijui kukopa wapi akanipa pesa nikanunue viatu[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ilibidi pilau lisipikwe na kwangu haikuwa shida ilimradi skuna nimepata[emoji23] [emoji23] [emoji23]