Wahhab kundi lenye itikadi kali ndani ya uislamu

Wahhab kundi lenye itikadi kali ndani ya uislamu

Hao wanaonekana kuwa Wana msimamo wa kati, wenyewe kwa hiari yao wameamua kuacha mafundisho ya Quran na kuendana na mifumo iliopoa kwa maana wamegive it up

Hao ndio masheikh waokoteza aya nyepesi nyepesi wakiacha zile ngumu ili kuendana na mfumo

Kwenye jamii maovu ni mengi sana na Vita ni kubwa katika kuhakikisha maovu hayo yasitendeke na watenda maovu sio tu wa dini zingine hata wenye majina ya kiislam hutenda maovu ambayo ukiyakanya kwa kutumia mfumo wa dini utaonekanwa mwenye msimamo mkali wa kidini

Hivyo masheikh wameamua kwa hiari yao kuacha kukanya maovu yanayotendeka kwa kuacha mafundisho ya Quran Bali kutafuta zile aya nyepesi nyepesi ili kuendana na kinachofanyika

Wasunni au wahab ndio walioshika dini kisawa sawa na ukitekeleza kwa vitendo changamoto ni kuwa nchi kama Tanzania yenye jamii mchanganyiko na nchi zingine zenye mfanano huo lazima wakuite gaidi na majina mengine yasiyofaa kwakuwa mifumo ya nchi haiongozwi kidini
Abood Rogo.
Nimekumbuka mbali sana.
 
Muhamad aliwapotosha Waarabu kwamba yeye na Uislamu wameandikwa katika Biblia. Wakamuamini. Wafuasi wake baada yake walipomtafuta Muhamad na Uislamu katika Biblia na kumkosa, wakaja na lawama kwamba Wayahudi na Wakristo wamebadilisha maandiko. Mpaka leo waislamu wanatusumbua huku na huku kwamba tumebadilisha maandiko na ndio maana Muhamad haonekani ndani yake.

Muislamu akiisoma Biblia jua hapo anasaka makosa tu na si ujuzi. Na ndio maana mtoto wa kislamu yoyote akiisoma Biblia kwa minajiri ya kutafuta wokovu, moyo wake taratibu utahama toka kwa Muhamad hadi kwa Yesu. Na ndio maana Biblia huko Arabuni ni maarufuku, na muislamu akishikwa nayo anauawa. Dini ya kibabe.

No maridhiano
Jikite Kumuhudumia Mumeo Aziz ki.
Haya unayojadili huna ujuzi nayo.
 
Endelea na usufi wako
Sheikh, haya ni masuala ya kidini na ni ibada.

Umetoa hukumu ya maneno yako na wapo waislamu wamesoma andiko lako na kwa msingi huo upo baina ya vizito viwili.

Imma kama ulichokiandika ni kweli uwagawie pepo. Na kama ulichokiandika si sahihi basi umeenda kinyume chake.

Hivyo kwa namna moja ama nyengine hukumu yako itabeba hukumu ya wengine siku ya kiyama, unapaswa kulitafakari hili kwa kina zaidi.

"eti wasunni wanaofuata usufi yaani awe Suni alafu afuate usufi, kichekesho"

Nimekuuliza swali kwa kusema mimi mababu zangu ni sunni na wanafuta usufi.

Nikamalizia swali, kwani usufi ni nini?

Nakuuliza tena, usufi ni nini?
 
Sasa wewe, utaratibu wako wa maisha unaengemeza wapi? Labda nikuulize kama ni mwanaume umetahiriwa? Na kama ni ndio umepata wapi huo utaratibu? Kuna mengine mengi kama kuona, kuzikakana, majina tuliyo nayo n.k. yameegemea kwenye dini fulani. Ukisema huamini katika dini unakuwa unatudanganya.
Hee yaani kutahiriwa nako ni mpaka ufuate maandiko ya dini? Kutahiri kulikuwepo toka enzi za mababu. Na ilikuwa ni sherehe kabisa na vijana wanapelekwa sehemu kwa ajili ya mafunzo maalum.
 
Wahhabi ni wafuasi wa harakati ya Wahhabism, ambayo ni mtazamo wa Uislamu wa Sunni ulioanzishwa na Muhammad ibn Abd al-Wahhab mnamo karne ya 18 katika eneo la Najd, Saudi Arabia. Harakati hii ilisisitiza kurudi kwenye Uislamu wa mwanzo, ikiwa na msimamo mkali dhidi ya kile walichokiona kama uzushi (bid'ah) na ushirikina (shirk).


Historia ya Wahhabi (Wahhabism)


1. Mwanzilishi: Muhammad ibn Abd al-Wahhab (1703–1792)


  • Alizaliwa Najd, katika eneo ambalo sasa ni Saudi Arabia.
  • Alijifunza Uislamu na kuathiriwa na mafundisho ya Ibn Taymiyyah, msomi wa karne ya 13 aliyepinga desturi nyingi zisizo katika Qur’an na Hadith.
  • Alianzisha harakati ya kidini iliyoitwa "Muwahhidun" lakini baadaye ikajulikana kama Wahhabism.

2. Ushirikiano na Familia ya Saud (1744)


  • Muhammad ibn Abd al-Wahhab alifanya makubaliano na Muhammad ibn Saud, kiongozi wa ukoo wa Saud.
  • Ibn Saud alikubali kutekeleza mafundisho ya Wahhabi kwa nguvu ya kijeshi, na kwa pamoja waliasisi dola la kwanza la Saudia.
  • Muungano huu ulisababisha vita vingi dhidi ya tawala za Kiarabu zilizoonekana kuwa na uzushi.

3. Uenezaji na Mapambano (Karne ya 18–19)


  • Wahhabi walifanya mashambulizi na kuchukua miji kama Riyadh na sehemu za Hijaz, ikiwa ni pamoja na Makka na Madina.
  • Mnamo 1802, Wahhabi walishambulia Karbala (mji mtakatifu wa Shia), wakaharibu maeneo matakatifu ya Shia na kuua maelfu ya watu.
  • Mnamo 1818, Dola ya Kiosmani (Ottoman Empire) iliwashinda kwa msaada wa Misri na kuharibu utawala wao wa kwanza.

4. Kurejea kwa Wahhabi na Kuundwa kwa Saudi Arabia (1902–1932)


  • Mwaka 1902, Abdulaziz Ibn Saud, kiongozi wa ukoo wa Saud, alianza tena harakati za Wahhabi.
  • Kufikia 1932, aliunda Ufalme wa Saudi Arabia, na Wahhabism ikawa itikadi rasmi ya nchi hiyo.

5. Athari za Kisasa na Mzozo wa Kimataifa


  • Saudi Arabia imekuwa mfadhili mkubwa wa Wahhabism ulimwenguni, ikijenga misikiti na shule za Kiislamu (madrasa) zinazofuata mafundisho haya.
  • Wahhabism imekuwa na athari kubwa kwa makundi kama Salafism, lakini pia imekosolewa kwa msimamo wake mkali dhidi ya madhehebu mengine ya Kiislamu kama Shia, na hata baadhi ya Waislamu wa Sunni wanaofuata Sufi na desturi za kitamaduni.
  • Harakati za kisasa kama Al-Qaeda na ISIS zimehusishwa na tafsiri kali za Wahhabism, ingawa Saudi Arabia yenyewe inapinga makundi haya.

Sifa Kuu za Wahhabism


✅ Kusisitiza Tawhid (umoja wa Mungu) na kupinga ushirikina.
✅ Kupinga desturi kama kuomba kwa maiti, kuzuru makaburi, na sherehe za kidini.
✅ Kufuata Qur’an na Hadith kwa tafsiri iliyo kinyume na bid’ah (uzushi).
✅ Kuhamasisha sheria kali za Kiislamu (Sharia).
✅ Kuwa na uhusiano wa karibu na ukoo wa Saud tangu kuundwa kwa Saudi Arabia.
Ha
Wahhabism imekuwa harakati yenye mvutano mkubwa ndani ya Uislamu na duniani. Ingawa imechangia kuanzishwa kwa Saudi Arabia, pia imekosolewa kwa msimamo wake mkali unaolenga kurejesha Uislamu wa mwanzo kwa kuondoa desturi ambazo wengi wanaziona kuwa sehemu ya utamaduni wa Kiislamu.
Kumbe wezao walikuwa wanapambana kujijenga kisiasa lakini huku wanatukanana kisa itikadi
 
Hee yaani kutahiriwa nako ni mpaka ufuate maandiko ya dini? Kutahiri kulikuwepo toka enzi za mababu. Na ilikuwa ni sherehe kabisa na vijana wanapelekwa sehemu kwa ajili ya mafunzo maalum.
Wamasai na wamang'ati wanatahiliwa huko maporini na hata dini hawazijui
 
Ndio uislamu unamakundi mengi ya ndani, na makundi mengi yamejipambanua na yanatambulika kwa majina yake.
Ila hili kundi linaloitwa wahhabi halipo, kwa maana 2

1. Hao wanaoitwa mawahab wao wenyewe hawajiiti mawahab
2. Huyo sheikh Muhammad ibn Wahab, wapo wanaokubaliana na mafundisho yake, lakini sio katika kiwango cha kusema ni wafuasi wake, au ni kama kikundi fulani kinachomfuta yeye tu pasi na kumfuata mwingine katika wanachuoni.

Hivyo hiyo itikadi wahabism haipo.
 
W
Kama wanateknolojia kubwa hivi, kwanini hawatengenezi vifaa kama simu, TV, Mitaala ya Elimu, Sabwoofer, Operating System n.k
Pamoja na mchina kucopy vitu vya mzungu ila vifaa ninazotumia humu ndani kwangu 100% havitoki kwenye za nchi kiislamu.
Wabongo ni shida. Badala kujiuliza sisi kama watanzania tunajivunia kwa lipi tuko busy kulinganisha sijui waarabu na wazungu. Ukienda huko kwao wala hawajali kama wewe ni muislam au mkristo, wao wanakuweka kwenye kundi la black african.
 
Sheikh, haya ni masuala ya kidini na ni ibada.

Umetoa hukumu ya maneno yako na wapo waislamu wamesoma andiko lako na kwa msingi huo upo baina ya vizito viwili.

Imma kama ulichokiandika ni kweli uwagawie pepo. Na kama ulichokiandika si sahihi basi umeenda kinyume chake.

Hivyo kwa namna moja ama nyengine hukumu yako itabeba hukumu ya wengine siku ya kiyama, unapaswa kulitafakari hili kwa kina zaidi.

"eti wasunni wanaofuata usufi yaani awe Suni alafu afuate usufi, kichekesho"

Nimekuuliza swali kwa kusema mimi mababu zangu ni sunni na wanafuta usufi.

Nikamalizia swali, kwani usufi ni nini?

Nakuuliza tena, usufi ni nini?
Kwani ushia ni dini? Unajifanya una diniiiiii
 
Abood Rogo.
Nimekumbuka mbali sana.
Wapo wengi tu ambao hatunao tena walijaribu kutekeleza maandiko ya Quran kikawakuta cha kuwakuta

Mifumo ya dini zote hutekelezeka sehemu yenye watu wanaoiamini dini hiyo vinginevyo ni vita
 
Hizi issues za ushia, usuni, udini, ukafiri, ukristo na takataka za aina hii wala hazituhusu waafrika basi tu shobo zetu kufuatilia mambo ya wageni.
Tangu lini mtu mweusi akatambulika katika dini za hawa weupe?, ukristo hauwatambui, uislam vile vile, sasa ninyi shobo za nini kufuatilia mambo yasiyowahusu?.

Kama wao na Miungu yao na dini zao sisi tunahusikaje? Inafika wakati mtu wa Njombe nae anamkosoa muislam wa uarabuni dini ilikoanzia, yani wewe unajiona mjuaji kuliko hao walioanzisha hizo taratibu zao za kijinga.

Bila hizi dini mbili za uislam na ukristo basi dunia ingekuwa sehemu salama sana, tafauti na hivi leo, mambo mengi ya hovyo yanafanywa na hao hao wafuasi wa dini mambo ambayo hata mnaowaita wapagani hawayafanyi mfano ushoga, mauaji, chuki, ubinafsi, wivu, kejeli, rohombaya hivi vyote vinafanywa na wafia dini ambao wanaaminisha ni dhambi,

amkeni jamani mnapoteza muda ktk hizo ngonjera za watu weupe.
 
Kwani ushia ni dini? Unajifanya una diniiiiii
Sheikh, kwa heshima na taadhima fuatilia maneno yangu.

Kutoka kwako uliandika sunni hawezi kuwa sufi.

Nikatoa ushahidi kuwa babu zangu ni sunni na vile vile ni masufi.

Ndipo nikakuuliza kwani usufi ni nini?

Suala si ushia, suala ni baina ya usufi na usunni!

Na by the way, mimi ni sunni.

Na lengo la kukuuliza hivi ni kwa sababu nataka kufananisha baina ya kwao nilichojifunza kuhusiana na usufi baada ya kuwauliza na uthibitisho waliyonifahamisha nilinganishe na ushahidi wako kwa hayo ambayo uliyoyazungumza baina ya usufi na usunni.

Karibu.
 
Back
Top Bottom