Special schools ilikuwa zamani, siku hizi hazivumi tena, hata watoto wanaomaliza hizo shule, wakija vyuoni wako kawaida sana, hata reasoning ability, IQ level zao hakuna kabisa tofauti na shule za kawaida, hivyo special schools ilikuwa zamani.
Unajua kinachofanya ivyo. Hapo Kuna ego na envy zinafanya kazi,yaani hutaki ego yako iwe down,ama yao iwe juu. Umecheki matokeo ya mwaka huu fomu walioenda huko wana ufaulu gani.
Kiufupi tu elewa binadamu Ni Yule Yule Jana Leo na hata kesho. Hata hii kauli yako imeshaongewa kitambo kabla Yesu hajaja.
Sema bana nafurahi kusoma humans emotions.
Hapo subconscious iko kazini inakutuma unaongea vitu ambavyo vinafanya unafarijika.
Ndio Mana ukipita shule za kawaida mfano day ukasoma ukapata kitengo kikubwa kazini ama usisome ukaja ukapata pesa lazima utakuja kutoa maumivu yako hapa kuwa wale waliosoma Sana wako waapi siku hizi Mara nimekutana naye akachoka.
Ukipita kawaida ama kayumba ukifanikiwa ukubwani utayatoa ya moyoni mwako maumivu kuwa waliosoma vipaji wako wapi ama waliosoma private schools hawana kitu kazi ilikuwa Ni spoon-feeding.
Ni sawa na mtu Hana smart phone anayo kitochi anajitetea kuwa mie smart ya Nini Kama kupiga na kutuma sms nafanya so hayo mengine hayana umuhimu. Na wakati huyo mtu ukimpatia chaguo la zawadi la simu mbili atachagua smart na kuacha kitochi.
Ni sawa masikini akishindwa kupata hela utamsikia hela za ndagu,Mara Freemason,Mara fisadi akaiba,aliyesoma akizipata hela ambaye hajasoma anakimbilia kujifariji kuwa nyie mmesoma bana. Aliye Soma akipata hela anavimba anatukana kuwa nimeajiri wasomi wenye digrii mie Ni la Saba na hawana kitu kichwani yaani full kutoa uchafu wake kichwani wa yeye kukosa kichwani.
Hata Elon musk ameshaongea kuwa sijasoma havard Ila nimeajiri havard graduate so ni Kama anatoa emotional pain trauma mkuu.
Yaani brain zetu huwa Zina mechanism ya kutuficha tusiuone ukweli upende usipende.
Ukiwa huna hela ya daladala nafanya mazoezi.
Ukiwa nazo maisha haya mafupi nijitese na Nini kwani mazoezi sitakufa acha Nile zangu nyama hapa Ila Kama Hakuna acha Nile dagaa na mboga za majani kwanza Zina afya.
Hii sio kuwa Ni wewe hata mie Mana Ni mechanism fulani ya brain ya kutuepusha na mental and physical pains. Kama vile ukikanyaga msumari ama Moto unatupa ama kutoa mguu fasta mno kuliko uwezo wa kawaida wa kuwaza.
So huwa nafurahia kukiona practically ninachosoma.