MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Nimeangalia kwa makini sana huu mjadala na kama mtu niliyewahi kufundisha chuo nimeshangazwa sana na uwezo wa hawa wanafunzi wa Kiafrika. Kipindi wanafanya huu mjadala walikuwa ni wenye umri mdogo sana, lakini uwezo wao wa kujenga na kujibu hoja, kuzungumza lugha ngeni kwa ufasaha, ujasiri, pamoja na uwezo wa kumheshimu mzungumzaji mwingine umenishangaza.
Nafahamu fika kwamba hizo hoja zao walizijadili vizuri kabla ya mjadala, lakini kilichonifurahisha ni uwezo wao wa kuvaa vizuri uhusika na kuzijenga hoja ipasavyo. Nasikitika kusema kwamba wahitimu wetu wengi wa vyuo vikuu wanashindwa kujenga hoja kwa namna hii na kuzungumza lugha kwa ufasaha: Iwe ni Kiingereza au Kiswahili.
Kuna sehemu kubwa sana, sisi kama taifa tunakwama: Nasikika zaidi kusema kwamba hawa ndugu wa mwaka 1957, waliweza kufanya mjadala mzuri unaoeleweka kuliko wabunge wengi wa Tanzania wa mwaka 2021. Kibaya na kinachosikitisha ni kwamba wanasiasa wetu wamekuwa ni watu wanaoogopa mno mijadala, tena hadi wengine ni PhD....
Tuna kazi ya ziada kama taifa....