Wahubiri wakristo mnaolitaja jina la Yesu bure redioni acheni mara moja!

Wahubiri wakristo mnaolitaja jina la Yesu bure redioni acheni mara moja!

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
2,351
Reaction score
2,255
Huu ni upumbavu na kudhalilisha jina la Yesu. Yesu ni mmoja na jina lake likitajwa mara MOJA linatosha. Upuuzi huu mnaoufanya redioni ni kumdhalilisha Yesu. Kwa jina la Yesu....bla bla bla ×100, kwa damu ya Yesu..... blah blah blah x70, kwa damu ya mwanakondoo.... blah blah blah x 50. Acheni upumbavu na kudhalilisha imani. Huo upuuzi mlifundishwa wapi. Acheni UPESI. Kanisa limejengwa kwenye misingi ya mitume na hakuna kati yao alifanya upumbavu mnaoufanya. ACHENI UPESI before the wrath of God is poured on you. Kama ni pesa mnatafuta katafuteni hata shambani zipo acheni kupotosha watu na kuifanya imani ya kikristo kuwa kituko.
 
Na mkiendelea this time tutamuomba Mungu awaaibishe hadharani. Hamwezi kufanya dhambi kubwa namna hii hhii mkaachwa tu . Kila mhubiri anayetumia jina la Yesu kujipatia manufaa binafsi sasa Mungu amuumbue. Uvumilivu wake umefika mwisho. Mungu si mdoli wa kumchezea. Anastahili heshima ya hali ya juu kwa sababu pamoja na mambo mengine hata elimu yote tuliyo nayo bado maumbile aliyoyaumba tu hatujaweza kuyaelewa vema. Si Quantum Physics wala Molecular Biology wala tawi lolote la sayansi wala hisabati lenye majibu ya FUNDAMENTAL QUESTIONS OF OUR EXISTENCE.
 
Mmefanya huko ni mahali pa kujipatia mapato ya aibu. Na kwa sababu kuna uhuru wa kuabudu basi mmejificha kwenye kichaka hicho maana hamguswi huko. Mungu anawaona kwenye hicho kichaka mlikojificha. Adhabu yenu inakuja. Hamwezi kuliharibu taifa la Mungu na watu ambao wengi wao hawana elimu ya Biblia mkipindosha maandiko na kufundisha uongo kwa manufaa binafsi. Mungu mwenyewe sasa atashuka awashughulikie maana uovu wenu umezidi. Mmeinajisi dunia, you deserve God's punishment. Katika agano jipya nyumba ya Mungu ni KANISA (JAMII YA WAAMINI). Ninyi mmeigeuza kuwa pango la wezi na matapeli. Mungu jawezi kukaa kimya siku zote. Enough is enough.
 
Wamekusikia mkuu
Wamenisikia sana na wasipoacha adhabu iko mlangoni. Uvum8livu wa Mungu umefika mwisho. Hata kabla ya gharika kuu Mungu alikuwa mvumilivu kwa maovu ya kutisha mwisho akasema baaaaasiii......yatosha
 
Wamenisikia sana na wasipoacha adhabu iko mlangoni. Uvum8livu wa Mungu umefika mwisho. Hata kabla ya gharika kuu Mungu alikuwa mvumilivu kwa maovu ya kutisha mwisho akasema baaaaasiii......yatosha
Kati yako wewe na Mungu nani anatoa adhabu mkuu?


Kikubwa ujumbe wako umefika
 
Kati yako wewe na Mungu nani anatoa adhabu mkuu?


Kikubwa ujumbe wako umefika
Ni Mungu ila nimetumwa tu kuleta ujumbe. Wakidharau this time mguu utaota tende. Si wameona hakuna mamlaka inayowakemea. Sasa imani ya kikristo imekuwa HOLELA tu. Mtu anaamka asubuhi na mafundisho yake na kanisa lake . It is enough!
 
Mi mwenyewe maisha yakinipiga sana najiita Nabii naenda kuwapiga hela wafuasi wa yesu
 
Ni Mungu ila nimetumwa tu kuleta ujumbe. Wakidharau this time mguu utaota tende. Si wameona hakuna mamlaka inayowakemea. Sasa imani ya kikristo imekuwa HOLELA tu. Mtu anaamka asubuhi na mafundisho yake na kanisa lake . It is enough!
Sawa
 
Huoni kama unajitengenezea hasira,chuki,hukumu na sonona kwa bei rahisi?
No. Not at all. I am doing it happily for my fellow human beings. Watu hawa wanapotosha ulimwengu. Kama naweza kuuambia ulimwengu uovu wao basi at least my existence has a meaning and will probably be remembered.
 
Mi mwenyewe maisha yakinipiga sana najiita Nabii naenda kuwapiga hela wafuasi wa yesu
Si vizuri. Ni kutengeneza taifa la mataahira kwa,jina la ukristo. Waumini wakristo wengi wao hawaijui imani wala historia ya dini. Hata hiyo biblia tu tafuta ni wakristo wangapi wameisoma hata ROBO tu. Katika wakristo elfu moja ukipata wakristo hamsini sijui. Watu kama hao kutapeliwa rahisi sana maana hawana misingi ya dini yao.
 
na mahubiri yao yanahusu utajiri tu
Lakini wao wwnyewe hawakutajirika kwa kutoa hozo zaka na sadaka maalumu. Kama vitu hivyo ni vya kumtajirisha mtu wangeenda kutoa huko makanisani wapate utajiri. Wanajua utajiri hauji kwa kwa njia hiyo. Wanakuambia mtolee Mungu kumbe zinaingia mifukoni mwao.
 
Ni Kama nakuskia ukisema,njia Bora ya kuishinda malaria ni kuua mbu wote duniani na sio kuelimisha watu namna ya kujikinga na kutunza mazingira.

Adhabu yenu inakuja. Hamwezi kuliharibu taifa la Mungu na watu ambao wengi wao hawana elimu ya Biblia mkipindosha maandiko na kufundisha uongo kwa manufaa binafsi.
Uliposema,watu hawana elimu ya biblia...uko right!hapo ndio tatizo limeanzia,hosea 4:6"my people are destroyed for lack of knowledge"
huwezi kumzuia shetani asidanganye,huwezi kumzuia shetani asipotoshe ila unaweza fundisha watu wakajua namna ya kujilinda na mafundisho potofu
 
Back
Top Bottom