Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Vp Kiboko ya wachawi ,mwenye kanisa Buza

Jamaa namskilizaga Furaha FM 90.9
 
Wapo pia mapadre wa kanisa katoliki na maaskofu walio wazuri sana katika kufundisha neno la Mungu ila kwa vile sio popular hawawezi kutajwa hapa .
Hawa ndio mkuu wao wa kanisa kasema ruksa jinsia moja kutinduana?.
 
Pastor Chris ndio Baba wa kiroho wa huyu tapeli na gold smuggler. Yeye nae akawa na kina Bushiri, makandiwa, mtalemwa, tonny na wengine kibao. Huyo jamaa ni charlatan wa kutupwa.
Baba wa kiroho wa Makandiwa sio huyo yuko Ghana na mwanzo walipoanza huduma walikuwa wanashare ila baadae mambo yaka badilika juu kwa juu...Ukiwa unawafuatilia utawaelewa tu.

Leo hii issue ya Fatherhood imenikumbusha jambo..Hivi unajia watumishi wengi wanasomeka sana katika ulimwengu wa roho kirahisi depending na Mababa wa Kiroho? Hata kushambiliwa hutegemea weakness za hao Mababa wa Kiroho..Choose your spiritual Father with full directives of Holy Spirit ukichagua kisa anafundisha na anawatu wengi au anawatoto wengi wa Kiroho inaweza kukupa shida mbeleni.

Hongera sana kwa vitabu ulivo visoma mtoa mada.Kuna njia nzuri sana kupitia hivi vitabu na mafundisho eidha ya audio au video vikiwa kwa uthabiti na kweli vimevuviwa na Master(Holy Spirit) kuwa imparted ndani ya spirit yamfuatiliaji ni kwa urahisi sana kama vile mapepo mengine yanavyo attack watu kupitia novels movies hata musics.

Hope namna yako ya kuamini sio ya kawaida maana watumishi hawa uliowataja wako deep mno katika issue za Faith.Hongera sana.
 
hakuna kupepesa macho kwa matapeli, wenyewe wanajijua. injili yao hata kwenye Biblia haipo. huyo kuhani mtoto wa yesu wa mkombo aliyefukuziwa congo huyo, na mwamposa anajua alikotoka. washindwe kwa Jina la Yesu.
Matapeli yamekuwa mengi sana. Waumini maamuma lazima wanaswe kwenye hizo vilinge vyao. Shetani naye anayo Mazingaombwe yake wengi wamekufa kwa kutafuta miujiza fake.
 
Baba wa kiroho wa Makandiwa sio huyo yuko Ghana
Oh its true, anaitwa prophet Victor kussi Boateng nimekumbuka.Hizi ni nyakati za mwisho. Bibilia inasema nyakati za mwisho zitakuwa za hatari, maana watu watayakataa mafundisho yenye uzima na kugeukia mafundisho ya mashetani na maagizo ya kibinadamu nao watajipatia waalimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti. Siku hizo ndo siku hizi sasa
 
Hapo Kenyon ndio namuelewa kuliko list yote. Sio kwa kumsikiliza bali kwa kusoma vitabu vyake.
Wengine wote wale wazungu huwa wanatuhumiwa kuwa ni Fmasons 33Β° hivyo huwa nawasilikiza kwa umakini sana au nawaacha kabisa.
Uchumi nje namsikiliza mzee Myron Golden. Namuelewa maana hapayuki anaongea vitu kiakili alafu hatafuti sadaka ya mtu. Nikiona mtumishi anatafuta sadakasadaka sana kuliko kufukua neno huwa namkwepa. Sadaka ni matokeo ya mtu kushiba neno sio mkakati wa injili.

Kwa Bongo, namkubali Pr. Mbaga Mwakasefe kidogo ila vitabu sio kumsikiliza tena eneo la uchumi tu sio kiroho.
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 

Huyu ni mchungaji kweli ila hana Injili, huwezi kumweka kundi moja na Kulola aisee, Huyu, Mitimingi na Toni Kapola hawana tofauti

Pr Mbaga wa Adventista ni far better kuliko huyu

Haya ni maoni Yangu
 
Z. Kakobe
 
Pastor Carlos Kirimbai ni wa wapi?
Pastor Carlos Kirimbai wa Tanzania, yuko hapo Dar, miaka mingi ya nyuma alikuwa akifanya kazi ya ukalimani katika mikutano ya Injili iliyokuwa inawaleta wahubiri mbali mbali wa kimaitafa hapa Tanzania mfano akina Bhonke. Kwa sasa muda mwingi anakuwa anafundisha na kuhubiri hapo Dar akitumia madarasa ya shule ya sekondari ya Kisutu, mjini kati na akishare free mafundisho yake kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp. Ni jamaa fulani hivi hana makuu lakini anapeo fresh wa bible na jamii.
 
Mwamba huyu mchambuzi wa Bible na misimamo mikali

Unaitwa FULL GOSPAL
. Z.Kakobe
 
Mzee Mabondo umenikumbusha mbali sana mkuu, Mungu ampumzishe salama. [emoji120]
Unamfahamu Aaron B. C. Mabondo? Hebu dadavua kidogo mkuu! Ni kati ya watumishi wa Mungu niliowakubali sana.

~ Alimpenda sana Mungu

~ Aliwaheshimu watumishi wenzake bila kujali utofauti wa madhehebu yao

~ Alikuwa mnyenyekevu sana

~ Alikuwa na imani katika NENO la Mungu. Japo hakuwa mtu wa media na hakupenda kujitangaza, kuna watu wengi walisaidika sana kupitia huduma yake, mfano:
1. Kumfufua Kanali wa JWTZ mkoani Arusha. Siku hiyo alikuwa Arusha katika Kanisa la KLPT Kaloleni alipopigiwa simu na mke wa marehemu ili akamsaidie kuupeleka mwili mochwari. Lakini alipofika, alimwamuru ainuke na ikawa hivyo, tena, akiwa hana hata chembe ya maumivu.

2. Dar Es Salaam nako pia alimfufua mtu.

3. Alipopelekwa hospitalini baada ya kivunjika mguu kwa ajali ya gari, daktari alipomwambia atakaa hospitalini mwezi mmoja alikataa. Alisema ana kazi nyingi hivyo atatoka baada ya siku tatu. Na kweli, siku ya tatu iligundulilka kuwa mguu ulishaunga na akaruhusiwa kwenda nyumbani.

Alikuwa ni mtu wa imani hasa. Alimwombea mwanamke aliyekuwa katolewa kizazi na hatimaye akaweza kubeba mimba, alimwombea muathirika wa VVU akapona, n.k.

Ukiweza, soma kitabu cha Historia yake, kinaitwa A WALK OF FAITH.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…