Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Fr Titus Amigu, namsikilizaga radio maria Tanzania , jamaa anahubiri na ana logic kubwa sana kwenye mafundisho yake.
 
You are right sir! Wanasema "like the father like the son". Kama niliona mhubiri ananitia mashaka, namfuatilia mentor/ baba yake wa kiroho. Nitakachobaini kwa hiyo ndicho kitskachonofanya niendelee kumfuatilia huyo au la.

Na kuhusu vitabu, they are very powerful. Kama ilivyo kwa maneno ya kutamkwa, ndivyo ilivyo kwa maandishi, ni roho.

Binafsi, nimeathiriwa sana na vitabu vya Kenneth Hagin. Nahisi vimeniambukiza "kitu", lakini kizuri.
 
Huyu ni mchungaji kweli ila hana Injili, huwezi kumweka kundi moja na Kulola aisee, Huyu, Mitimingi na Toni Kapola hawana tofauti

Pr Mbaga wa Adventista ni far better kuliko huyu

Haya ni maoni Yangu
🙏🙏🙏
 
Kimsingi umewataja wa mtandaoni na wanaosikika sana kwenye media ila bado wapo watumishi wazuri tu humu duniani. Kuna mzee mmoja nilimkuta huko Iringa niliendaga na kuiishi kikazi mwezi mmoja huko Vijijini Dabaga nikawa naabudu kanisa la TAG Kilolo Christian Centre lipo pale Kilolo Wilayani Anaitwa Mzee Lucas Mkuye. Huyo ndio Mtume wa kwanza wa kweli kumuona maishani mwangu.

Mzee alianza huduma 1979 kipindi hiko ukanda wote wa Dabaga hauna kanisa lolote la kipentecoste na alikuwa akitembea kwa miguu hadi Mapanda huko Mufindi na akaanzisha na kusimamisha makanisa ya TAG ukanda huo. Zaidi ya makanisa 60 yametokea mikononi mwake.

Kwa Walutheri tunaoishi au kukulia ulutheri Morogoro au kwa wale tuliosoma Lutheran Junior Seminary miaka ya 1990's tuna mkumbuka Marehemu Mchungaji Hebert Hafferman. Huyu ndio Mtume wa Pili wa kweli kumuona kwa macho yangu achana na akina Bashando na Daudi Mashimo.

Mzee yule alikuwa mzungu na alikuja TZ miaka ya 1950's na alisambaza Ulutheri kwa kiasi kikubwa kwenye jamii ya kimasai. Aliwekeza kwenye huduma ya Neno na masuala ya kijamii ikiwemo kuwasomesha wamasai wengi wa Morogoro. Zao lake mmojawapo ni Richard Mameo Askofu wa Lutheran hapa Morogoro. R.I.P HEBERT HAFFERMAN, tutakutana katika pambazuko lile katika siku ile ya kalamu ya mwanakondoo.

Picha ya Marehemu mzee Hebert Hafferman akiwa na mtoto wa mchungaji mmoja wa Kimasai Marehemu Lucas.
 
Huyu ni mchungaji kweli ila hana Injili, huwezi kumweka kundi moja na Kulola aisee, Huyu, Mitimingi na Toni Kapola hawana tofauti

Pr Mbaga wa Adventista ni far better kuliko huyu

Haya ni maoni Yangu
Mkuu, binafsi simfahamu Pr Mbaga. Unaweza ukamwelezea kidogo? Huenda kuna mtu anaweza akawa anahitaji "huduma" yake.
 
Nashukuru mkuu🙏

Kumbe ni huyo! Nilishawahi kumsikiliza kupitia YouTube. Yupo vizuri🙏🙏🙏
 
Huyu TAPELI nae yumo hivi huwa mmefungwa macho? Aljeeriza wameonyesha utapele wa huyu na nia ya kuhubiri bado umemuweka meza moja na Kulola
Mkuu, nilieleza kuwa hao niliowaweka ni ambao kwa namna Moja ama nyingine nimebarikiwa na huduma zao.

Nilivisoma vitabu kadhaa vya Uebert Angel, japo kuna baadhi ya mambo ambayo mwanzoni vilinitia mashaka kuhusu huduma yake, niliamua kupuuzia baada ya kubaini kuwa mentor wake ni Pastor Chris.

Pastor Chris naye nilikuwa nina mashaka naye, lakini mashaka yaliisha nilipogundua kuwa rafiki yake wa karibu ni Benny Hinn.

Hata Benny Hinn, nilikuja kumkubali vilivyo baada ya kugundua ukaribu alikokuwa nao na Reinhard Bonnke.

Unauona mnyororo ulivyo? Bonnke, Benny Hinn, Pastor Chris, Uebert Angel.

Lakini sivyo tu, huwa nina "falsafa" yangu kwa habari ya watumishi. Kwamba, katika mafundisho yao, nitatofautisha chuya na wali. Nikikutana na chuya, nitatema lakini wali nitaumeza.

"Sibugii" kila kitu kisemwacho na mtumishi. Nikijiridhisha kuwa akisemacho kipo nje ya Biblia, nakiweka kando nasubiria kingine.
 
KUNA KAUKOMAVU FULANI NA KAUTUBUZIMA NIMEKAONA NILIPOKUWA NASOMA LINE TO LINE YA HAYO ULIYOANDOKA.WEWE SIYO WALE WA SURIALI NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI .GRAND MALT NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI.
NATAMANI TUNGEKUTANA ANA KWA ANA,NINGETOKA KATIKA MKWAMO.
BE BLESSED.
 
PAST Elingarami Munishi,namuona yuko objective sana.
 
Karibu mkuu, lakini mimi si Mchungaji wala kiongozi wa dini. Lakini ukipenda kunitafuta sitakuzuia.
 
Hao wote hapo juu sina shaka nao,hasa pastor Chris oyakhilome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…