there are times tunaongea kama utani, but tukija kwenye point ya kweli, Mungu kaweka siku kila mtu atafanikiwa, shetani ndio huwa anaturudisha nyuma ila kuna siku ikifika Mungu akatibua maji, hata shetani afanyeje mtu huwa anatoboa tu. cha muhimu ni kuendelea kupambana na kutokata tamaa kwasababu anayeanguka mara nyingi akija kusimama huwa haanguki tena. kila tunachopitia hapa duniani ni shule. wengi hata kwa hapa tulipofikia tunashukuru Mungu, ni kwa neema yake tu, kwasababu kama ningesema niandike kitabu cha historia, nilishindwa nikadharauliwa hadi na watoto wadogo, pesa imekata, nikaanza mdogomdogo, siku Mungu alipokuja kufungua mlango shetani anajaribu kufung akila siku anashindwa, amebaki kushambulia matunda tu ila mti ameshindwa kuukata. God's time is better, hii ni kwa kila anayesoma hapa.
there are times unaweza kuwa na mtaji na ujuzi na kila kitu, lakini kwenye ulimwengu wa roho milango haijafunguka, utapoteza tu hela yako. ila Mungu akiweka tiki kwenye ulimwengu wa roho, unateleza tu milango na watu waliofanikiwa wanakutafuta, sio wewe kuwatafuta tena. cha muhimu hapo ni kumtafuta mwenye uwezo kufungua milango, Mungu ndiye anaweza na ana ijara yake, shetani pia ukienda ana ijara/ujira wake (roho yako au za watoto wako), Mungu anasema bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa, wengi tumetafuta sana maisha huko duniani tukapata lakini baadaye shetani akachukua vyake vyote na matatizo juu, tulipokimbilia kwa Mungu kwa principle hii alirudisha miaka yetu yote iliyoliwa na madumadu na parare. nilikuwa siamini hii principle hadi iliponikuta. Asante Yesu.