Wahudumu wa Shishi Food Dodoma wajifunze kauli nzuri kwa wateja

Uzi umejaa mapovu ya kutosha😂😂😂hadi Raha Yani, mtoa mada usirudi Tena hapo shishi food, hela ya kwako wasikusumbue kuitumia, mie ningeinuka muda huo huo na wasingeniona tena hapo, sinaga kuremba
 
Uzi umejaa mapovu ya kutosha[emoji23][emoji23][emoji23]hadi Raha Yani, mtoa mada usirudi Tena hapo shishi food, hela ya kwako wasikusumbue kuitumia, mie ningeinuka muda huo huo na wasingeniona tena hapo, sinaga kuremba
[emoji23][emoji23][emoji23] nilihamia Upande Wa Pili, Maana pembeni yake Kuna Bar
 
Kwakweli hata Hawa watu wa MPESA, TIGO PESA and the like, unaenda unamsalimia haitiki anakuangalia tu, unamuuliza unataka kuweka fedha anakujibu baada ya dakika 2. Duu huwa naondoka aise. Naheshimu sana fedha yangu and huwa sikubali kabisa kubagazwa(in kabudi' voice) wakati fedha ni yangu.
 
Lakini kuna wateja hawo, wasikie tu kwa jirani...wateja wengine wanapenda kuhangaisha wahudumu kisa tu wanalipia huduma fulani basi watawahangaisha mpaka muhudumu anabadili mtizamo kuhusu hio huduma.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wewe hamnazo kweli nakuja kufata huduma unachukua mda mrefu huji then mteja msumbufu una mlaumu kumbe na wewe uko hovyo hivo aisee. Nadhani hata genge huna unabisha kufuraisha waja humu jf.
 
Ila kuna watu wakishapata wateja wanajisahau sana na kuamini kila siku wapo. Akija kufungua mwingine pembeni akawa na lugha nzuri na mshap unaanza kusema kakuloga, kumbe kakuloga kwa customer care nzuri na ushap kwa wateja.

Kaeni mkijua biashara yoyote isiyokuwa na upinzani mteja huwa anaonekana fala sababu hana pa kwenda.

Angalieni mfano wa TANESCO,



Kuna watu wanaitumia vibaya ile slogan ya Mteja ni mfalme.
 
Low thinking capacity
 
Sahihi kabisa Mkuu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa niaba ya shishi food nimesoma comment zenu zote nyingine za kutia moyo nyingine za kuvunja moyo ila nimeshalifanyia kazi hapa nilipo naelekea babati haidom kuchukua wahudumu wapya naimani ukija tena hutokutana na ile kero ya mwanzo na pia jumapili hii uje ule biriani bure kwa umbea wako
 
ndio maujinga ya wahudumu wa dodoma anazoea wateja shish alete wat kutok mikoa mibgine sio wa hapo hao watoto wajibga sana
 
😀 😀 😀 😀
Gerara here.
 
Huko Babati unakoenda kuchukua wafanyakazi usitusahau na sisi wateja wenu tunaopenda kuhudumiwa na Wanawake bikra.!
 
Niliwahi kuagiza chakula nikiwa hotelini Dar es salaam, hoteli yenyewe hawapiki ila wanakupa namba ya Hawa watoa huduma ya vyakula vya take way and delivering! nikapewa number ya shish food na nilikuwa na hamu sana nionje chaula chake.
Kiukweli mpokeaji simu hakuwa na majibu mazuri, pili chakula kilifika cha baridi sana, tatu usumbufu wa mletaji mara aseme kudeliver bei ni hii lakini alipofika akanichaji bei kubwa Zaidi ya chakula nilichoagiza!
Nimshauri dada shilole - Epuka kuajiri washikaji, Ili biashara yako idumu usichekecheke na kujenga mazoea na staff wako, weka managent strong na staff wenye wito na kazi hiyo!
Wish all the best Shilole!
 
Kauli ya mteja ni mfalme inatafsiriwa vibaya kwetu sisi watanzania kiasi kwamba mteja wa aina yetu akiwa na pesa zake nyingi za kutumia atawapelekesha wahudumu kisa tu yeye analipia. Kwa wale wenye biashara zao hapa Tanzania wanaelewa nini namaanisha.

Mfano mzuri ni madereva na mkondakta wa dala dala, tabia zao zinafanana na Watu aina ya changumi, matusi mengi tu mdomoni yanasubiri mteja amchanganye yaanze kutoka wangu wangu.. ukweli ni kuwa wanageuka kuwa watata kwa sababu ya kauli za wateja.... Kuna mahali niliwahi kwenda kwenye hotel moja, langoni yuko baunza anayechuja wateja, akikuotea huruhusiwi kuingia.....atasingizia kitu kama mavazi kuwa hairuhusiwi.
 
Tatizo lenu mmawatongoza!! Mbona mi nikifika wananihudumia chap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…