Wahuni wa Kinshasa Julai 17 1997- Desemba 25 2024

Tunaendelea........!!!!
MUNGU NI MWEMA KUKAKUCHA.
AFANDE MONOO............kama kawaida yake akanifuata usiku ule ule tuliokuepo pale KISANGANI na akaanza kunipa maelekezo aliyoyapata kwa LESAPEE MUNDENDE kuhusu harakati za kutafuta mawe......ndani ya maeneo yote ya KIVU KASKAZINI na KIVU KUSINI....na maeneo ya jimbo la Tanganyika.
Tulizungumza mambo mengi na akanipa miiko na nini cha kufanya na nini cha kutokufanya tunapokua na askari wa Mzee Kabila......na nini cha kufanya au kutokufanya tunapokutana na askari wa FDRL au tunapokutana na askari wa RPF......au waasi wa kinyamulenge.
AFANDE MONOO akaniambia kua... kwenye pesa hakuna adui......!!!!
Kila mtu anatafuta pesa.......so tuanze kazi mara moja bila kukawia.

1998.............MWAKA WA NEEMA.
Baada ya Mobutu kuondolewa madarakani na Mzee Kabila kuingia madarakani.....huu ni ulikua mwaka wa NEEMA kwa wadau kujichotea mawe bila bughudha.
Katika maisha yangu sijapata kuona watu wenye uchu wa mali na roho za kibaguzi kama wanyarwanda....iwe wanatokea MULENGE AU RWANDA........kwanza wao kwa wao hawapendani...........na kila kitu wanataka wao.
Wakongomani ni watu wapole na Wana huruma mno......ndio maana watu wanatumia hiyo kama advantage,s.
Plani ikawa tutakua tunaenda sehemu salama na mzigo inaletwa tufanye biashara.... HAIJALISHI kaileta muasi au askari wa jeshi la serikali.
Wakati huo pia Waganda nao walikua wamejaa tele na biashara zao za magendo za KUUZA mawe na silaha.
Unapaswa kujiuliza????
Wakongomani wanatoa silaha wapi??
Kwanini hakuna amani DRC???
Nani alichochea ukabila DRC???
Majibu ya haya yote utayapata wakati naendelea kukuabarisha habari hizi.
Mkumbuke kua ...katika kikao hiki sikuepo peke yangu tulikua watu wengi..........ila kwa sababu mazungumzo yananihusu Mimi...basi nitawahifadhi wezangu kulinda faragha zao.
Unajua baada ya kutokea kwa mauaji ya kimbali nchini RWANDA.....na hayo mauaji ya kimbali kuhamia hapa Zaire...ndio nikajua kumbe siasa ni mchezo wa kuigiza.
Nitayasimulia haya mbele kadri ya uzi unavyoendelea.
TURUDI KWENYE SIMULIZI.
Tukapokea mdau kutoka KABONDO.... ...mtu wa kazi......anaewauzia mawe walebanoni na Waganda na wakenya.
Jina la mdau nalificha sababu hapendi ajulikane mpaka leo.
Jamaa akacheka sana alipotuona sababu kiswahili CHETU lilikua kinamfurahisha.
Katika watu wote pale akatokea kinikubali Mimi na akaomba.........niongozane nae mpaka KABONDO sehemu ya kazi.
Tatizo la maeneo Yale kwa miaka ile usalama ulikua mdogo sana......moyo wangu ukasita nikakataa............ila kwa ushawishi wa jamaa yetu huyu...nikajikuta na Mimi naongozana na ndugu yangu huyu mpaka KABONDO...... kwenye maeneo yasiyo rasmi kunakochimbwa DHAHABU.
Ilituchukua siku tatu kwa njia za kufunga unga mpaka tulipofika kwenye maeneo kunakochimbwa DHAHABU.
Pale nikakutana na watu wamepinda balaa....yaani nikakutana na nchi ndani nchi.
Watu hawana habari na SERIKALI..wao wanachowaza tu......ni kutafuta Hela.
Kwanza wanakaa kwenye vibanda na juu ya miti kama wanyama.
Huko hakuna haki za WATOTO.....
Watoto wanatumikishwa mpaka unawaona huruma.
Kila mbabe pale machimboni ana himaya yake ya kibabe...na ole wako uingie bila RUHUSA.
Itaendelea................!!
 
Watoto wanatumikishwa mpaka unawaonea huruma.
Kila mbabe pale machimboni ana himaya yake ya kibabe...na ole wako uingie bila RUHUSA.
Itaendelea................!!
 
Hapa nitapenda kusikia habari za kisangani, bafaswende, mambasa, niania, bangedaido, butembo, bwera, Kasindi, nitapenda ugusie jinsi waarabu wa taqwa , classic walivyotajirishwa na bangi na dhahabu za magendo, nitapenda kusikia kama makako mlikula, nitapenda kusikia visa vya akina general Salim Saleh wa Uganda mdogo wa muse7 , jinsi walivyo vuna mbao pori kupeleka ulaya na dhahabu za kutosha , nitapenda ugusie vita ya wanajeshi wa Uganda na Rwanda kisangani kugombea maeneo yenye madini mengi , nitapenda ugusie wanajeshi wa Rwanda na Uganda waliojipatia mabilioni ya dollar kwenye dili za magendo ya oral au dhahabu na diama au almasi , nitapenda uelezee biashara ya risasi haramu zilivokua zinaingia Congo kutokea Kenya Mombasa zikitokea Pakistan , umenikumbusha visa vingi pia hapa ngoja nilewe kwanza madogo wa Leo laini Sana , enzi hizo Ajira majeshi ya Congo nanrwanda hata uraia hawaulizi mtaulizana baadae na uraia utapewa baadae , Congo , zairwa Acha wateseke ni shamba la Bibi kitambo
Ila itifaki itazingatiwa...ndio maana naandika kidogo kidogo
 
Back
Top Bottom