Wahuni waiba engine ya lori lililotumbukia Mto Wami

Usisahau kuwa dereva alinasa ndani ya cabin siku 2 so haikusambaratika
 
Mkuu Tanzania tuna watu wana uwezo wa kuiba kwa ustadi. Nakumbuka miaka ya nyuma kuna Mercedes Benz Actross ilizama mto Kagera.

Wajuba walipoambiwa kuwa spea za Benz ni dili, baada ya muda mfupi sehemu za ile gari zikawa zimefika nchi kavu mpaka gearbox, usiulize watu walizamia muda gani na mamba wa mto kagera walikuwa wapi?
 
Daaahh, usilolijua ni kama usiku wa giza.
Nimesoma kwa sauti kubwa ila nimeambulia patupu mh mjumbe..
 
Isjie ikawa kama ya WEST GATE wale JAMAA WA MABAKA wamefanya yao!!
Watafanyaje yao huku tukio zima likirekodiwa tangia wapewe amri na mkuu wao?

Wa kwanza kuhisiwa kama ni hujuma ni ile timu ya kwanza iliyodai jambo hilo haliwezekani, kumbe linawezekana tena kiurahisi kabisa!

Ndiyo maana wakatoa mkadirio wa mbali kuvuruga ushahidi.

Nilistaajabu sana kwa kada hiyo ya uokoaji kutoa tathimini yao ya kizembe zembe kama hiyo, nikawa najiuliza maswali yasiyo majibu!

Hata kama injini na kebeni viling'oka kwenye msukosuko vingelikutwa jirani na hilo chesesi, maana maiti ilikwama humo na ikaopolewa!

Vyombo vinavyohusika vikifuatilia kuanzia staff waliopo hapo idara ya maji, wakiwemo wavuvi ukweli utajulikana tu na kuna watu wataibeba hiyo kashifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…