Wahuni waiba engine ya lori lililotumbukia Mto Wami

Wahuni waiba engine ya lori lililotumbukia Mto Wami

Nachojiuliza, uyo mmama ameweza kununua scania mpya zaid ya million 100 ila alishindwa kupata m2 kuokoa lori lake.

Kuna kitu kinatakiwa kifatliwe hapa. Ilo lori lina comprehensive insurance au ni la mkopo bank?
 
Naona maswali yote unayojiuliza hayana mashiko.

Enhe, likifuatiliwa halafu?

Unajiuliza maswali ya mtu kukosa mil2 katika kadhia kama hiyo na kisa chote mbona alikiweka wazi kwamba hiyo ilikuwa ni trip ya kwanza!

Kununua kitu chenye thamani na kuishiwa pesa mbona ni jambo la kawaida kabisa ili mradi mhusika alikuwa na lengo lake na mahesabu yake namna ya 'kutoboa' ili kujiendeleza.
 
Baada ya Mkuu wa Majeshi kupeleka kikosi chake kulitoa lori lililo tumbukia mto wami, lori limekutwa halina engine wahuni wamesha fanya mambo yao.

Wabongo sio watu wazuri.

Pongezi wa CDF kwa kufanikisha hilo japo kwa kuchelewa.
Wameiba au imebaki chini kwenye maji wataiba wapeleka wapi sasa maana ujue ile gari kabla ya kudumbukia mtoni iligonga nyuma ya gari nyingine. Halafu je unayajua maji yanayotembea vizuri maana tusiongee
 
Mkuu Tanzania tuna watu wana uwezo wa kuiba kwa ustadi. Nakumbuka miaka ya nyuma kuna Mercedes Benz Actross ilizama mto Kagera.

Wajuba walipoambiwa kuwa spea za Benz ni dili, baada ya muda mfupi sehemu za ile gari zikawa zimefika nchi kavu mpaka gearbox, usiulize watu walizamia muda gani na mamba wa mto kagera walikuwa wapi?
Duh, Kuna watu mamaster wa uwizi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ukisikiliza hiyo video unawasikia waliolitoa wenyewe wanasema hapa hakuna gari tena
 
Mimi nitakua wa mwisho kuamini hili kwasabu.... Ebu kwa akili ya kawaida jaribu kifikiria uzito wa Geabox na Engine. Kisha jiulize Cabin mbona haijatoka na chassis??
Kisha nikujibu tu kwamba bolts zinazo kamata Engine mauntain ni nne pekee zenye unene wa 16 millimeters.
Gearbox inaunganishwa na bolts 10 zenye unene wa 10 millimeters kutoka kwenye flyn wheel pamoja na pressure, inayo ungana na bell housing ya aluminum.
Sasa.....
Ile impact ya force plus weight kutoka kule juu darajani ingeweza kuhimili kuto kusambaa kwa gari lile...??
Upo sahihi lakini bado watu wanaweza fanya hii michezo

Hiyo link hapo juu ni toyota hiace ilitumbukia baharini kigamboni ikitokea kwenye kivuko lkn baada ya wiki moja ilitolewa huku ikiwa haina baadhi ya vitu muhimu hadi power windows, ni ajali ya april 20, 2016
 
Nachojiuliza, uyo mmama ameweza kununua scania mpya zaid ya million 100 ila alishindwa kupata m2 kuokoa lori lake.

Kuna kitu kinatakiwa kifatliwe hapa. Ilo lori lina comprehensive insurance au ni la mkopo bank?
MI nimeshindwa kuelewa
 
Back
Top Bottom