Wahusika kwenye kadhia ya Mbowe Wawajibishwe

Wahusika kwenye kadhia ya Mbowe Wawajibishwe

Chereko chereko zinapoendelea kufuatia kuachiwa huru Mh. Freeman Mbowe, kadhia hii isiishe bila fidia wala watu fulani fulani kuwajibika au hata kuwajibishwa.

Kwenye kadhia hii kuna watu wamepotezwa, watu wameteswa, utaratibu wa sheria umekiukwa, watu wamedhulumiwa, nk.

Yote haya ikiwa ni ufedhuli mkubwa uliopitiliza usioweza kuvumilika.

Asiachwe awaye yote kwa ukiukwaji wowote uliofanyika.

Kama mamlaka haichukui hatua, waovu hawa na waburuzwe mahakamani wao kama raia.
Mkuu kwanini wawajibishwe?..kwani hukumu imetolewa kuwa mbowe ameshinda kesi?...kumbuka kuna mtego mbowe kawekewa..mahakama ilimkuta na kosa kabla ya leo DPP hajaachia unyoya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni watu wa ajabu sana

Katiba mpya iwe wazi kufurushwa kwa watu kama hawa kutokana na wananchi kutoridhishwa na utendaji wao hasa huu uliojaa dhuluma, yapigiwe msitari.
 
!Aibu Kwa Jaji Kwa maamuzi aliyofanya!Watu wamebumba ushahidi wakaja kuuleta mahakamani,kila mtu akaona ni ushahidi wa mchongo na hakuna kesi!Jaji akasukumwa kuamua kuwa Wana kesi ya kujibu!Kabla hawajaanza kujitetea DPP anasema hana nia ya kuendelea na kesi maana ushahidi alionao ni crap!
Jaji unajisikiaje huko uliko?Ungeyajua haya,Bado uamuzi wako ungekuwa watuhumiwa Wana kesi ya kujibu?
Kesi ya kujibu aliyoona Jaji ambayo DPP hakuiona ni ipi?🤣🤣🤣
 
Mkuu kwanini wawajibishwe?..kwani hukumu imetolewa kuwa mbowe ameshinda kesi?...kumbuka kuna mtego mbowe kawekewa..mahakama ilimkuta na kosa kabla ya leo DPP hajaachia unyoya

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbowe kama kwa Lijenje, hana hatia mkuu.

Yumkini Hangaya, Sirro, DPP, Kingai, majaji wa kesi hii, na bila shaka hata wewe unajua hivyo.

Kwanini Wawajibishwe? Yako mle kwenye mada mjomba:

"Kwenye kadhia hii kuna watu wamepotezwa, watu wameteswa, utaratibu wa sheria umekiukwa, watu wamedhulumiwa, nk."
 
URIO sijui kama jeshi litamuamini tena...

Kina kingai pia nafikiri ndio mwisho wa kupewa Operation za Michongo.. Wameonekana Zero kabisa..

Naamini kesi zote zikifuatiliwa kama ilivofuatiliwa hii ya mbowe,,Mahakama itabaki uchi sana
 
Urio akakubali kununuliwa.

Heko kwao Lembrus Mchome, Komando Mhina na wote waliosimama na haki hadi mwisho.

Mola atawalipa.
 
Hoja nzito iko hapa kama mshtaki anasema anaona hana kosa la kuendelea kushtaki, je mhukumu aliyetangulia mbele kwa kusema mshtakiwa ana jambo la kujibu ana hali gani? Mahakama imeachwa na harufu mbaya sana! Inanuka!!!
Mkuu kwanini wawajibishwe?..kwani hukumu imetolewa kuwa mbowe ameshinda kesi?...kumbuka kuna mtego mbowe kawekewa..mahakama ilimkuta na kosa kabla ya leo DPP hajaachia unyoya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule jamaa aliyekuwa akitajwa kama Kakobe, sijui hatma yake itakuwaje
 
Kwa hyo mnafurahia mbowe" kufika Bei"
Kale malimao. Maganda yake yatakufaa sana. Kila mlichotaka kimekwama. Kesi ya mchongo imeangukia pua.

Wekeni matanga - mna msiba mzito!
 
Back
Top Bottom