Jamani tusi walaumu wasanii wetu, kwanza tujiulize je, mifumo yetu ya sanaa na michezo inatoa fursa sahihi ya kuibua na kukuza vipaji vya wasanii na wana michezo wetu?
Pia, tujiulize je, jamii (familia) zetu zina muamko wa kuthubutu kuchukua jitihada binafsi katika kuibua, kukuza, na kulinda vipaji vya wasanii na wana michezo wetu??
Hata Ukidadisi Maisha aliyopitia Lupita NYONG'O yana tofaut kubwa sana na maisha wanayo pitia wasanii wetu, kuanzia ngazi ya familia, jamii, mazingira, na hata muamko wa mambo ya sanaa.
SISEMI LUPITA Haku-struggle Katika Kufika Pale Alipo sasa, bali ni ukweli ulio wazi licha ya juhudi zake binafsi, pia amesaidiwa sana na aina ya maisha aliyopitia, hasa kielimu na kijiografia.
WATU WEUSI WENGI, HASA WAAFRIKA LEO HII TUNAJIVUNIA JINA LA LUPITA NYONG'O KATIKA UWANJA WA FILAMU, Lakini Tujiulize Je, Tunafanya Juhudi gani Katika Kutengeneza Kina NYONG'O Wengine???
TUWALAUMU WASANII WETU KWA LENGO LA KUWAZINDUA KUTOKA USINGIZINI, Na Sio Kuwaponda bila kuwapa msaada.