Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Ukitaka kuvuta watu popote pale
  1. Kata viuno
  2. Zungumzia mahusiano au mapenzi
Waimbaji siku hizi wananengua kwa mashindano si kwamba wanapeleka ujumbe wa Mungu ila wanawatega watu

Wahubiri wanaofuatiliwa na watazamaji au wasikilizaji wengi ni wale wanaozungumzia sana ndoa, mahusiano, tabia za mabinti nk

Wabunge nao wanapenda sana kuvuta attention za watu kwa kukatika kwenye mikutano ya kisiasa na kuzungumzia mapenzi bungeni

Viongozi wa kisiasa kadhalika ...rejea ukatikaji wa Kangi Lug mbele ya mkubwa wake wa kazi nk

Hospitali nako unakuta TV ikionyesha nyimbo za vitovu nje wagonjwa wanafunua blanket, wengine wanasukumia net pembeni
ila tuache utan mapenz matamu nyiny
 
Ambao hawachezi kanisani wana hoja ya msingi.

Ila nyinyi ambao mnaanza kulalama mtu akicheza akapitiliza nashindwa kuwaelewa kabisa.
Kuna tofauti na kumchezea Mungu na kumchezea shetani
 
Dansi na mavazi ya hovyo makanisani sio mafundisho ya UKRISTO wala hayapo kwenye biblia, sema mitume na manabii feki wanaogopa kusema ukweli hofu ya kukimbiwa sadaka zikapungua
 
Hapana awamsifu Mungu bali shetani, pili sio makanisa yote ni Mungu siri anajua mmiliki wa kanisa husika.
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Dah Sasa mbona hawatuvulii na sisi tuone bana kumbe nabii alicheza hadi akavua nguo waambie watuvulie na sisi tudindishe vizur sio wanatukatikia tu hatuoni vizur tena mm napenda miuno ya waimbaji mabonge [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Kucheza kwa Mfalme Daudi hadi nguo kumvuka haina maana na sisi Waleo tucheze kihuni.
Inawezekana zilimvuka kwa bahati mbaya , Je tuige hiyo bahati mbaya yake?

Pia haijaandikwa kama agizo kwa watu wote kuwa kwamba tuwe tunacheza kama yeye alivyocheza.

Msichanganye Habari!
 
Only Christian na hawataki kurekebishwa na vimini vyenye mpasuko.
 
Ila ukweli tuseme, wakata mauno na wale wavaa vimini wanachangamsha mazingira, Hata waumini huengezeka.

mrangi
 
Kama huyo
 
Kwani kiuno si kimeumbwa na Mungu, acha kinenguliwe tu...
Mungu hawezi kukereka na mauno ya watu. Binadamu wenyewe ndio wanajitengezea vya kupenda na kuvichukia halafu wanamsingizia Mungu.
 
Ibada za pasaka zinaendelea; kwaya mbalimbali zinatumbuiza. Nimeenda kwenye kanisa mojawapo kusali naomba nisilitaje jina.

Waimbaji wananengua na kucheza mithili ya ngoma za kienyeji na kidunia.

Wengine wananengua miuno kabisa.

Sasa huku ni kumsifu Mungu kweli?
Wameshukiwa na upako
 
Ibada za pasaka zinaendelea; kwaya mbalimbali zinatumbuiza. Nimeenda kwenye kanisa mojawapo kusali naomba nisilitaje jina.

Waimbaji wananengua na kucheza mithili ya ngoma za kienyeji na kidunia.

Wengine wananengua miuno kabisa.

Sasa huku ni kumsifu Mungu kweli?
Pole kwa kubanwa na nguo!
Ila ni kweli inatia kichefuchefu!
 
Kukata viuno ni tamaduni Za mahali.... Congo kukata viuno ni kama zanzibar kuomba taarabu.....
Sis ndo tunaona ni dhambi.... Kuna makabila mengine kusalimia a wanasalimiana kwa kujamba.... Sis sio rahisi mtu kujamba hadharan
 
Mathayo 15: 8-9

“ watu hawa huniheshimu kwa midomo,
Ila mioyo yao iko mbali nami”

Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu.


Wanakwaya wakata viuno mioyo yao huwa mbali na Bwana Mungu.
 
Back
Top Bottom