Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
Sasa mimi nimekuja kutazama mauno yako au kusikiliza ujumbe wa kuniongoa roho? Ni saikolojia ya kawaida tu, ukichezesha mauno watu wataconcentrate na mauno badala ya ujumbe ulioko kwenye hizo nyimbo. Na nyimbo ni ibada pia. Acheni hizo, halafu anakiri kuwa ulikuwa upuuzi aliyofanya, usisahau kuna mabaya mengi Daudi aliyafanya.
 
Kuna kucheza kwa staha na kucheza kihuni,inawezekanaje binti mwanakwaya kashika kiti anachuma mboga huku anazungusha kiuno?,alafu tukipita nao mnatulaumu.
HAKUNA KUCHEZA KWA STAHA NDUGU.

Daudi hakucheza kanisani (ndani ya ibada) bali alipotoka kuchukua sanduku la BWANA [emoji116].

2 SAMWELI 6:16-20.

SHETANI HUTUMIA NJIA HIZO HIZO KATIKA MAKANISA [emoji116].

2 WAKORINTHO 11:14-15.
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

AGIZO LA MUNGU KANISANI NI KUABUDU KWA UNYENYEKEVU [emoji116].

WAEBRANIA 12:28-29.

HABAKUKI 2:20.
 
Kwan wao wanamchezea Mungu yupi? Labda Wana Mungu wao anayependa hayo.
 
Je haikuandikwa nabii alicheza mpaka mavazi yakamvuka? Na sherehe ilichukua siku 7 au wewe una bible yako ilio tofauti na ninayo isoma Mimi?. Acha mabo ya wajenzi huru Ile ni office kama office zingine zilivyo au hujui makampuni ya ujenzi ya wageni yalio jaa hapa Tz?.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
So mikatiko ya ngono inaruhusiwa kanisani kwenu kisa tu Daudi alicheza akabaki uchi.
Je alidhamiria kubaki uchi? Au ni nguo ilianguka tu
 
Haya mambo ya Daudi alimchezea Bwana hadi akabaki uchi, kesho vigodoro na kanga moja na densi zote za kupromote ushoga au kupromote ngono vitaanza kuchezwa makanisani.
Daud hakudhamiria kubaki uchi ni nguo ilimvuka.
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Soma hapa.

Amos 6: 5 ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;
6 ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu.
7 Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani pamoja na wa kwanza watakaokwenda utumwani, na kelele za machezo za hao waliojinyosha zitakoma.
 
Sasa mimi nimekuja kutazama mauno yako au kusikiliza ujumbe wa kuniongoa roho? Ni saikolojia ya kawaida tu, ukichezesha mauno watu wataconcentrate na mauno badala ya ujumbe ulioko kwenye hizo nyimbo. Na nyimbo ni ibada pia. Acheni hizo, halafu anakiri kuwa ulikuwa upuuzi aliyofanya, usisahau kuna mabaya mengi Daudi aliyafanya.
Si kila kilichoandikwa katika Biblia ni cha kufuata, bali mengine ni lesoni kwetu [emoji116]

1 WAKORINTHO 10:11.
Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

Hao wazee wa mapokeo bila ya kuchunguza Maandiko Matakatifu yanavyotuagiza ni wapumbavu sana [emoji34].

Mbona hawaigi jinsi Daudi alivyotembea na Mke wa Msihiri na alipata adhabu ya kufiwa na Mtoto aliyezaa naye yule Bethsheba [emoji848][emoji38]

Pia hata Absalom alikuja kuzini na Wake za Baba yale Daudi maana ni laana iliyotokana na upumbavu wa Baba yake Daudi.
 
Mfalme Daudi alicheza hadi nguo zake zote zikaanguka, kama watu wanaweza kumsifu shetani hadi wakalala chini huku wanakata mauno sioni vibaya watu wakimsifu Mungu kwa style yoyote ilimradi hizo sifa zinafanyika katika roho na kweli

Mungu anaishi katika sifa
Soma
Amos 6: 5-7
 
Kuna video wanaimba ng'ang'ana na Bwana, huwa namtania wife ang'ang'ane na Bwana. Na Bwana ndiyo miye! Waimbaji wanakata miuno! Hadi unasisimka!
Lazima usisimuke sababu we ni Binadamu una moyo wenye tamaa, pia si taratibu za ibada takatifu mbele za Mungu [emoji16]
 
Kasome tena bible. Yupo nabii mmoja alicheza mpaka nguo zikamvuka na kubaki kama alivyo zaliwa. Isitoshe mbinguni unakufahamu? Je Kuna utaratibu wote unao kuelekea namna ya kucheza? Mwili ni hekalu la mungu cheza itakavyo.
Kwenye Biblia pia kuna Nabii alienda kutafuta malaya anaejiuza, mwisho wa siku akalala na mkwe wake,.na wakapata watoto.
Je na sisi tufanye hivyohvyo.??

Si kila alichofanya nabii ni sahihi. Nao walikuwa ni watu, na kuna wakati walifanya makosa.
 
Huyu sasa umkute anakata kiuno na mchungaji. Mpeleekee moto, moto, moto... Shetani.
Ndiyomaana wachungaji wengi hujikuta wakianguka kiroho na kiimani sababu ya uzinzi na chanzo cha yote hayo ni kutofata maagizo ya Mungu inavyopasa na kujichagulia tunayoona yanatupendeza sisi Binadamu [emoji26]
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mungu anaangalia moyo wako na matendo yako na sio mavazi, angekua anaangalia mavazi basi magaidi wote wangeenda mbinguni maana huwa wanajifunika mpaka uso na macho

Tujitahidi kutenda matendo mema na kuweka mioyo yetu safi, unaweza kuvaa gauni refu panaaa kama gunia halafu usiku ni pakashume unaeruka na ungo...
Aliyekuroga kafa.

Unadhani utajivalia kimini na kuingia ofisi yoyote ile ya serikalini, unadhani kwanini wanakataza [emoji848][emoji19]

Kama serikali tu(ya Kaisari) inayokuongoza kidunia namna ya kuishi, ndiyo ije kuwa Mungu akuruhusu huo upumbavu [emoji848][emoji34]
 
Licha ya kwamba tunamuona Daudi akicheza kwenye matukio mbalimbali, lakini katika suala la uimbaji ndani ya Ibada Daudi alikuwa makini na alipokea maelekezo kutoka kwa Mungu jinsi ya kuongoza kwaya ya Walawi, na hatuoni waimbaji hawa wakicheza kwenye Hema Takatifu wala Hekaluni, bali walisimama wakiwa na vyombo vyao waliimba kwa utulivu nyimbo za kumtukuza Mungu

2 #Mambo ya Nyakati 29:25 Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake.
Hawa waimbaji hawakuimba wakiwa wanacheza viduku au kukatika viuno bali waliimba wakiwa wamesimama 2 #Mambo ya Nyakati 35:15 Nao waimbaji, wana wa Asafu #wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia.

KWANINI HAITAKIWI KUCHEZA NDANI YA MAJENGO YA IBADA?
1. Eneo la ibada sio sehemu ya kurukaruka kama Disko, ni mahali pa unyenyekevu palipotengwa maalumu kwa ajili ya mwanadamu kumuabudu Mungu na ndio maana tunatoka nyumbani kwenda kanisani. Kwa hiyo kinahitajika kicho.
#Waebrania 12:28-29 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;maana Mungu wetu ni moto ulao.
#Habakuki 2:20 Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.

2. Malaika wenyewe ambao ni watakatifu wanamuabudu Mungu kwa kuimba kwa unyenyekevu wakiwa wamefunika nyuso zao, na sio kwa kurukaruka:
#Isaya 6:2-3 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

3. Ikiwa unapoenda kwa Baba yako mzazi au kwa bosi wako kuomba msaada unaenda kwa unyenyekevu na kicho, inakuwaje kwa Mungu uende kwa kucheza viduku na kunengua, ambaye yeye Mungu ni zaidi ya baba yako,na ni zaidi ya boss wako?
#Malaki 1:6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?

4. Je kuna mtu ambaye Alisha wahi kwenda kwa mzazi wake au kwa Boss wake kuomba mahitaji Fulani na akaenda kwa kupiga kelele na kwa kuchezcheza viduku?
Kucheza ndiko kunawafanya watu waimbe nyimbo za matusi na za kipuuzi,kwa sababu asiliia kubwa ya nyimbo za siku hizi hazina ujumbe wowote, bali zinapendwa kwa sababu ya style za kucheza na midundo iliyomo, #Zaburi 47:7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.
Hapa umemaliza... .
 
Yote haya ikiwemo dansi za kukata viuno zimeingizwa makanisani Ili kuwapotosha watu. Viongozi wa dini nao wanaogopa kuongea ukweli juu ya mavazi yasiyostaha kuogopa kuwakwaza waumini watawakimbia sadaka zitapungua. Sketi fupi, suruari, jeans, t shirt, ndala, skuna, car wash, tracksuit,pajama,kofia,nguo za mapicha sio mavazi ya kuvaa ibadani, watu wanachanganya mavazi ya disco, beach , michezo na mavazi ya ibadani.
Hongera waislamu kanzu na baibui ni vazi la ibada.
Mungu anaangalia roho na sio mwili ni fundisho la uongo kabisa na hii ni Kazi ya freemason waipenyeza kwa watumishi wao kupitia mitume na manabii feki Ili kuliangusha kanisa
Umenena vyema kabisa.
 
Ila wafia dini kwa kuhamisha magoli hamjambo.
Mimi nakumbuka miaka ya zamani kidogo ilikuwa hairuhusiwi mwanamke kuvaa suruali au siketi fupi na kwenda nayo kanisani!
Cha ajabu miaka ya hivi karibuni wanawake wanavaa vichupi skin jeans na kwenda nazo kanisani na mmeanza kusema eti "Mungu haangalii mavazi, ila anaangalia roho"
Wazee wa haki sawa hao, wameona ni mbinu sahihi kujiingiza makanisani kutafuta Wanaume wasiojielewa kupitia kukata mauno.

Ni Me mpumbavu tu ndiyo ataendelea kuweweseka nao bali anayejitambua hatataka kuonana nao ana kwa ana hata kwa sekunde 1 tu.
 
Kwenye Biblia pia kuna Nabii alienda kutafuta malaya anaejiuza, mwisho wa siku akalala na mkwe wake,.na wakapata watoto.
Je na sisi tufanye hivyohvyo.??

Si kila alichofanya nabii ni sahihi. Nao walikuwa ni watu, na kuna wakati walifanya makosa.
Mwisho wa siku akijaribiwa na Mchawi atataka kukimbia kama Nabii Eliya alivyomkimbia Mchawi Yezebeli badala ya kukomaa na maombi ya kiimani, kufunga na kusali [emoji1787]
 
Ndiyomaana wachungaji wengi hujikuta wakianguka kiroho na kiimani sababu ya uzinzi na chanzo cha yote hayo ni kutofata maagizo ya Mungu inavyopasa na kujichagulia tunayoona yanatupendeza sisi Binadamu [emoji26]
Wamevutiwa na starehe inayochochea zinaaa halafu wakatafuta kafungu kamoja kanakoendana na hiyo starehe kisha wakahalalisha.

Kama kuna mtu alicheza mpaka akavua nguo ndio maana wanacheza,Elia aliua wale wapagani walipoamini MUNGU yupo baada ya kuhubiriwa na Elia wakathibitisha wakasadiki lakini Elia akawachinja, Kwann na wao wasiue wakishakutubisha sala ya toba kufata aliyofanya elia kama suala ni kufanya yaliyofanyika na watu wa kale?

Suleman alioa wake wengi kwann hawaoi? Kwann huyo aliyecheza mpaka akawa uchi tu ndo sahihi kumuiga?
 
Back
Top Bottom