Asante kwa neno, nimebarikiwa sana
Licha ya kwamba tunamuona Daudi akicheza kwenye matukio mbalimbali, lakini katika suala la uimbaji ndani ya Ibada Daudi alikuwa makini na alipokea maelekezo kutoka kwa Mungu jinsi ya kuongoza kwaya ya Walawi, na hatuoni waimbaji hawa wakicheza kwenye Hema Takatifu wala Hekaluni, bali walisimama wakiwa na vyombo vyao waliimba kwa utulivu nyimbo za kumtukuza Mungu
2
#Mambo ya Nyakati 29:25 Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake.
Hawa waimbaji hawakuimba wakiwa wanacheza viduku au kukatika viuno bali waliimba wakiwa wamesimama 2
#Mambo ya Nyakati 35:15 Nao waimbaji, wana wa Asafu
#wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia.
KWANINI HAITAKIWI KUCHEZA NDANI YA MAJENGO YA IBADA?
1. Eneo la ibada sio sehemu ya kurukaruka kama Disko, ni mahali pa unyenyekevu palipotengwa maalumu kwa ajili ya mwanadamu kumuabudu Mungu na ndio maana tunatoka nyumbani kwenda kanisani. Kwa hiyo kinahitajika kicho.
#Waebrania 12:28-29 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;maana Mungu wetu ni moto ulao.
#Habakuki 2:20 Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.
2. Malaika wenyewe ambao ni watakatifu wanamuabudu Mungu kwa kuimba kwa unyenyekevu wakiwa wamefunika nyuso zao, na sio kwa kurukaruka:
#Isaya 6:2-3 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
3. Ikiwa unapoenda kwa Baba yako mzazi au kwa bosi wako kuomba msaada unaenda kwa unyenyekevu na kicho, inakuwaje kwa Mungu uende kwa kucheza viduku na kunengua, ambaye yeye Mungu ni zaidi ya baba yako,na ni zaidi ya boss wako?
#Malaki 1:6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?
4. Je kuna mtu ambaye Alisha wahi kwenda kwa mzazi wake au kwa Boss wake kuomba mahitaji Fulani na akaenda kwa kupiga kelele na kwa kuchezcheza viduku?
Kucheza ndiko kunawafanya watu waimbe nyimbo za matusi na za kipuuzi,kwa sababu asiliia kubwa ya nyimbo za siku hizi hazina ujumbe wowote, bali zinapendwa kwa sababu ya style za kucheza na midundo iliyomo, #Zaburi 47:7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili.