Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Vigezo vilivyotumika:

1. Nyimbo zinazoendana na neno la Mungu
2. Kuwepo kwenye imani thabiti ndani ya Kristo
3. Kuwa na malezi ya kiroho na kanisa analohudhuria kama mshirika
4. Muendelezo wa ukuaji wa huduma, ujuzi na ubora wa kazi.

Kumbuka, hatulinganishi karama bali namna karama ilivyotumiwa kwa ustadi.

Twende pamoja sasa:

1. Abihudi Misholi
2. Fanuel Sedekia
3. Christina Shusho
4. Ambwene Mwasongwe
5. John Lisu
6. Paul Clement
7. Joel Lwaga
8. Upendo Nkone
9. Martha Mwaipaja
10. Ipyana Kibona

Ambao hawakuingia lakini ni wazuri pia hawa hapa:

Christopher Mwahangila, Ephraim Mwansasu, Beatrice Mwaipaja, Walter Chilambo, Paul Mwangosi, Boaz Danken, Safari Paul, Upendo Kilahiro, Jennifer Mgendi, Edson Mwasabwite, Gwamaka Mwakalinga, Beatrice Muhone, Faustin Munishi, Rehema Simfukwe

Kuna wale maarufu sana ambao hawakuingia kwa kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo hapo juu kama Rose Muhando, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Goodluck Gozbert, Angel Benard, Flora Mbasha, Neema Mwaipopo
Nlivyoona kwny top 10 hayupo Rose nkajua tu hauko serious!.
 
Wimbo wake wa:
Ee Mungu wangu mimi nitakushukuru....
Hutumo..
Namtaka Yesu nimuone
Si Salama
Mungu wa Mapendo..
Amina...n.k...

Ile Album Rose alijua kuitendea haki Aiseee....
....nipe moyo wa nyama,uliopondeka,moyo uliyotulia........sikia we kinanda,sikia we kinubi.The best song ever( kwangu lakini).Rose ni level nyingine( kwangu lakini).

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
MUNGU kagawa vipawa tofauti na vyote ni utukufu kwake everyone is perfect for his/her position,kila mtu na Neema yake
 
Mimi namkubali muimbaji chipukizi MARIAM KILYENYI
na wimbo wake HAKIMU WA HAKI, pamoja na ule NATAFUTA MSHAURI!
 
#1AMBWENE
#2AMBWENE
#3AMBWENE.
#4 MWASONGWE
Naunga mkono hoja hapo kwa Ambwene, Huyu mtumishi analiimba neno la Mungu, natumai kabla ya kutoa wimbo hua anafunga na kuomba kwanza, Ukiwa mpenzi wa "gospel-bongofleva "zile za kuchambana, kusimangana na kusemana huwezi msikiliza Ambwene. Ambwene anahubiri kupitia wimbo, Anahubiri kwa unyenyekevu na upole, hakika Mungu ambariki na kumsamehe dhambi zake.

Japo kwa kutenda haki nakuzingatia ulegend list yangu ni hii
1.Sedeki
2.Abiud
3. Ambwene.

Tukirudi kwenye amsha amsha hakuna kama Rose Muhando.
 
Kuna kwaya fulani miaka ya 2002 inatokea mkoa wa tanga sijui inaitwaje ile naitafuta kweli.
Ni kwaya ya KKKT, kwenye kasha la kanda walijipanga mstari halafu wa mbele wamechuchumaa.

moja ya kipande cha wimbo kinasema
Bwana yesu anasemaaa yeye yu ndani ya babaa
sisi tuwe ndani yake ili tupate uzima.

Naomba msaada kwa anayeijua hiyo kanda maana kipindi hicho nilikuwa bado sijui kusoma.
 
Sisi watu wa mziki mzuri hatuna baya
Screenshot_20220910_190411.jpg
 
Back
Top Bottom