Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Mkuu, ni kwamba ukiwa na matendo ya giza hauwezi kuwa unashuhudia Kristo. Nuru na giza havikai pamoja. Sasa mtu anayeishi maisha ya uzinzi anawezaje kumshuhudia Kristo? Huku ni kujidanganya.

Naomba tafsiri yako maana halisi ya kuwa ndani ya Kristo. Kuhusu wanawake kuwa viongozi nitaandika kidogo tuelimishane, niko njiani kwa sasa. Ila nikuhakikishie, tena si mimi ila Roho, toka kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana hakuna andiko linaloruhusu mwanamke kumwongoza mwanamume. Hii ni asili ya uumbaji wa Mungu wala theolojia haina nafasi kabisa, pure scriptures.
 
Mkuu, ni kwamba ukiwa na matendo ya giza hauwezi kuwa unashuhudia Kristo. Nuru na giza havikai pamoja. Sasa mtu anayeishi maisha ya uzinzi anawezaje kumshuhudia Kristo? Huku ni kujidanganya.
Ni kweli anayeishi gizani hawezi kuhubiri ya nuruni wala kuleta nuru. Kukiwa na uthibitisho basi tutamuondoa maana hatuwezi kuwa na icons ambao hawafuati maadili ya kikristo.


Mtu anapokuwa ndani ya Kristo anakuwa kiumbe KIPYA, wote waume kwa wake. Wote ni hali ile ile ya kiroho (similar spiritual being), hakuna tofauti.

Mwanaume ni kiongozi kwenye muktadha wa ndoa. Ndani ya ndoa mke na mume hawapo sawa. Mume ni kichwa. Hili ni jambo muhimu sana kujua.

Nje ya ndoa mwanaume na mwanamke wanafanana kila kitu iwapo wapo ndani ya Kristo. Kulikuwa na situation nyingi tangu enzi za Musa kuhusu sehemu ya mwanamke kwenye mambo kama ya urithi nk

Watu kama Deborah, Esther, Miriam, Rahab, Martha, Phoebe nk walionesha uongozi katika namna mbalimbali ndani ya biblia.

Kukaa kwenye nafasi ya kiuongozi kuliathiriwa zaidi na tamaduni zilizorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine lakini hili halijawahi kuwa agizo la Mungu mahali popote.
 
Debora alifanya kazi gani?
Kuongoza vita haikuwa uongozi katika agano la kale?
 
Hakuna aliyeishika nafasi yake na kwa kizazi hiki cha studio artists na ulokole wa kisasa, sijui kama tutapata wa kariba yake
Tumepoteza lengo la uzi kitambo sana
 
Albam ya Jipange sawasawa kuna ule wimbo Amina hatari....Mtoa mada wewe ni nan mpaka uanze kuwahesabia watu dhambi kwamba unasema Rose mhando sio mcha Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wimbo wake wa:
Ee Mungu wangu mimi nitakushukuru....
Hutumo..
Namtaka Yesu nimuone
Si Salama
Mungu wa Mapendo..
Amina...n.k...

Ile Album Rose alijua kuitendea haki Aiseee....
 
Rahabu yule kahaba(kama alivyotajwa)alikuwa na uongozi gani ndani ya Biblia?
 
Inaonekana nyimbo za injili umeanza kuzisikiliza kwanzia miaka ya 2005 kuja juu, waimbaji wengi uliowaweka kwenye top ten wameibuka katika awamu ya pili ya kutawala kwake JK.

Usiniambie kuwa kabla ya waimbaji hawa tena wengi wakiwa under 40, hapakuwahi kutokea waimbaji wa injili Tanzania waliotikisa Africa Mashariki.

Pata muda, sikiliza nyimbo za kina Jangalason na waimbaji wengine wa wakati wake.

Vinginevyo hiyo orodha ingejikita kuanzia mwaka 2015 kuja leo.
 
Image ya mtu kwenye public inaweza kuwa fabricated,naweza kupika positive image yangu naweza nikaficha behind the scenes ,
Hakuna mtu Yuko na monopoly ya truth , maadam wote tuko kwenye msururu kwenda kwenye mzani wa haki ,huna authority yoyote wala Askofu wako ya kusema huyu ni mbaya huyu ni mwema ,Watu wanaangalia kipawa Cha Mtu ,MUNGU ananyesha mvua Kwa Watu wote hata wachawi always
 
Rahabu yule kahaba(kama alivyotajwa)alikuwa na uongozi gani ndani ya Biblia?
Tafsiri ya uongozi kwenye ulimwengu huu imeathiriwa sana na maoni ya wagiriki katika filosofia yao kiasi kwamba tunaposema uongozi mtu anawaza kisiasa na utawala.

Yule mwanamke aliweza kufanya negotiation iliyopelekea taifa zima la Israel kuwa chini ya kiapo chake na hatimaye akawaokoa ndugu zake wote.

Hatimaye akabadilisha maisha yake na akaja kuolewa na kuwa na familia. Hakuishia hapo, ni miongoni mwa great grandmothers wa Bwana Yesu Kristo.

Kama huu sio uongozi basi nothing else is.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…