Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Mkuu, ni kwamba ukiwa na matendo ya giza hauwezi kuwa unashuhudia Kristo. Nuru na giza havikai pamoja. Sasa mtu anayeishi maisha ya uzinzi anawezaje kumshuhudia Kristo? Huku ni kujidanganya.Katika ujumla wake ninaona maisha yao yanamhubiri Kristo. Hakuna jambo lolote la wazi ambalo linafahamika kiasi kwamba waweze kuhesabika kuwa hawafuati maadili ya kikristo.
Mkuu concept ya kuwa ndani ya Kristo haijaweza kutafsiriwa vyema na matokeo yake wengi wanaona wanaume na wanawake hawawezi kushika majukumu yanayofanana katika kanisa lakini hili sio sahihi. Pengine unaweza kuuleta huo mjadala tupeane elimu na kujengana.
Naomba tafsiri yako maana halisi ya kuwa ndani ya Kristo. Kuhusu wanawake kuwa viongozi nitaandika kidogo tuelimishane, niko njiani kwa sasa. Ila nikuhakikishie, tena si mimi ila Roho, toka kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana hakuna andiko linaloruhusu mwanamke kumwongoza mwanamume. Hii ni asili ya uumbaji wa Mungu wala theolojia haina nafasi kabisa, pure scriptures.