Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Kiujumla kwa sasa hii huduma ya uimbaji imeingilia sana,watu wako kipesa zaidi kuliko utumishi...mtu anaalikwa kwenye mkutano wa injili anataja na kiwango cha kumpa,bila kujua NENO linasema mmepewa bure toeni bure,leo watu wanauza huduma ya Mungu...Mungu awabariki wale wote wanaofanya hii Huduma ktk Roho na kweli.
 
Wewe humfahamu Jangalasoni...huyu ni mtumishi wa Mungu ambaye ameimba ktk upako kwa miaka mingi kabla hajaondoka nchini,kizazi cha miaka ya 80' mpk 90' +2000 mwanzon kinamjua vzr
Video nilizoona YouTube anaonekana kijana mdogo. Aliimba tangu miaka ya 80? Basi itakuwa nimepishana naye.
 
Aliyoyapitia hayatupi sisi uhalali wa kum'judge..

Kila mtu ana mapito yake...tunaanguka ila Neema ya Mungu inatunyanyua tena....

Kwanza umeshausikiliza au kuuona wimbo wake wa 'Simba'? She is back like nothing happened.
"-Simbaa...anaungurumaaa-"Inasisimua na kufikirisha na kutia ujasiri pia.Kwangu ni gwiji wa Gospel Tanzania hii...

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
1. Nyimbo zinazoendana na neno la Mungu
2. Kuwepo kwenye imani thabiti ndani ya Kristo
3. Kuwa na malezi ya kiroho na kanisa analohudhuria kama mshirika
4. Muendelezo wa ukuaji wa huduma, ujuzi na ubora wa kazi.

Kumbuka, hatulinganishi karama bali namna karama ilivyotumiwa kwa ustadi.

Twende pamoja sasa:

1. Abihudi Misholi
2. Fanuel Sedekia
3. Christina Shusho
4. Ambwene Mwasongwe
5. John Lisu
6. Paul Clement
7. Joel Lwaga
8. Upendo Nkone
9. Martha Mwaipaja
10. Ipyana Kibona

Ambao hawakuingia lakini ni wazuri pia hawa hapa:

Christopher Mwahangila, Ephraim Mwansasu, Beatrice Mwaipaja, Walter Chilambo, Paul Mwangosi, Boaz Danken, Safari Paul, Upendo Kilahiro, Jennifer Mgendi, Edson Mwasabwite, Gwamaka Mwakalinga, Beatrice Muhone, Faustin Munishi, Rehema Simfukwe

Kuna wale maarufu sana ambao hawakuingia kwa kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo hapo juu kama Rose Muhando, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Goodluck Gozbert, Angel Benard, Flora Mbasha, Neema Mwaipopo
Kuwepo kwenye imani thabiti ndani ya Kristo!!! Afu unaleta vituko?

1. Huyo Shusho amekuwa mfano mbovu kwa familia na huduma pia

2. Mwaipaja anaishi na mumewe wa ndoa?

Nadhani wote hawa wana makanisa kwa sasa, nani kamwita mwanamke afungue Kanisa?
 
Kuna waimbaji humo kawataji walishaachika kwenye ndoa za kikristo na wakaolewa tena.
 
Maisha binafsi ya mtu hakuna anayeweza kuyafahamu asilimia mia moja isipokuwa Mungu mwenyewe. Hapa tunaangalia general public life na kufuata maadili ya kikristo.

Kufungua kanisa? Hapa tutaenda kwenye theological arguments ambazo ni nje ya mjadala huu. Ndani ya Kristo hakuna myahudi wala myunani, mwanaume au mwanamke, wote ni mwili wa Kristo.
 
Kuna waimbaji humo kawataji walishaachika kwenye ndoa za kikristo na wakaolewa tena.
Kuachika kwenye ndoa ni jambo pana sana pengine linahitaji mjadala wake. Hata suala la kuoa/kuolewa upya nalo ni pana na lina theological perspectives nyingi hivyo tusiende sana huko.

Kifupi biblia imeruhusu kutengana na ukifanya hivyo ukae kwa kutulia. Na imeruhusu kumwacha yule anayeenda nje ya ndoa. Huyo ukitengana naye unaweza kuoa tena.

Msingi wa kanisa kukataa watu kuacha na kuoa upya upo zaidi kwenye kuelewa maana ya msamaha. Kwamba kama Mungu anatusamehe kila aina ya dhambi (of course isipokuwa kumkufuru Roho Mtakatifu) ni kwanini sisi nasi tusisamehe watu aina zote za dhambi?
 
1.Fanuel Sedekia
2.Cosmas Chidumule
3.Jangala Son
4.Paul Mwangosi
5.Abiudi Misholi.
6.Apostle Kyande(Kenya)
7.Ambwene Mwasongwe
8.Medrick Sanga
9.
10..........
Hao ni among the best!
 
Maisha binafsi ya mtu hakuna anayeweza kuyafahamu asilimia mia moja isipokuwa Mungu mwenyewe. Hapa tunaangalia general public life na kufuata maadili ya kikristo.

Kufungua kanisa? Hapa tutaenda kwenye theological arguments ambazo ni nje ya mjadala huu. Ndani ya Kristo hakuna myahudi wala myunani, mwanaume au mwanamke, wote ni mwili wa Kristo.
Unaposema maisha binafsi unamaanisha nini? Yaani ndoa ni maisha binafsi? Na kama unaangalia maisha ya ujumla kwenye jamii basi hawa wanatakiwa maisha yao YAMHUBIRI KRISTO. Je wanafanya hivyo?

Halafu suala ala wanawake kuwa viongozi wala halihitaji theolojia yoyote, niaandiko tu yapo wazi kabisa. Hata hicho ulicho nukuu wala hakisemi hivyo, kina ujumbe tofauti kabisa. Kama ungependa ningefafanua kidogo lakini kwa kuwa umedai tutabadili mada basi naacha hivyo.
 
Katika ujumla wake ninaona maisha yao yanamhubiri Kristo. Hakuna jambo lolote la wazi ambalo linafahamika kiasi kwamba waweze kuhesabika kuwa hawafuati maadili ya kikristo.

Mkuu concept ya kuwa ndani ya Kristo haijaweza kutafsiriwa vyema na matokeo yake wengi wanaona wanaume na wanawake hawawezi kushika majukumu yanayofanana katika kanisa lakini hili sio sahihi. Pengine unaweza kuuleta huo mjadala tupeane elimu na kujengana.
 
Back
Top Bottom