Wairan 8000 ni Wayahudi

Uyahudi ni dini pia!!??
Haya maneno ukiyaweka katika kiswahili yatakuchanganya maana utaona yana maana moja.

Jewish ni myahudi.
Judaism ni uyahudi.
Hii ni dini ambayo wameiingiza kwenye sheria yao kwamba mtu aki convert kuwa Judaism tayari ana sifa ya kuitwa Jewish.
 
Hao siyo wayahudi bali ni wa Iran pure kabisa, vizazi vyao vimekaa huko zaidi ya miaka 7000 halafu waseme ni waisraeli kweli? Wayahudi nao wanakwama
Wakati serikali ya israel inawashawishi wahamie israel ila wewe unasema sio wanapewa hadi ofa za 60,000usd ili wahame .
 
Mimi sio mjuzi sana wa historia lakini kama kuna ushahidi wa wazungu kukubali utumwa Misri basi hoja ya wayahudi wazungu itakuwa ina make sense
Hiyo ya waisrael kuwa watumwa nadhani ni kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Lakini mwaka 70 BK waisrael walitoka Israel na kusambaa kwenye nchi mbali mbali zilizo jirani na Israel ya sasa. Kumbuka hii mipaka ya utambuzi wa nchi iliyopo sasa haikuwepo zama hizo.

Pia taratibu za kuhamia toka sehemu moja kwenda nyingine hazikuitaji taratibu zinazotumika hivi sasa. Kwa ivo mambo ya utumwa na Israel ya sasa ni historia iliyokaa mbali kwa mbali.

Unajua waisrael kabla ya mwaka 1948 walikaa nje ya eneo hilo la Palestina kwa zaidi ya miaka 2,000?
 
Kama unaamini Biblia basi Wayahudi ni ndugu moja na watu wa Iraq kwa sababu inasemwa huko ndiko baba yao Ibrahim alipotoka, watakuwa ndugu mmoja na Ishmael pia.
Inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.Wayahudi wanasemwa ni watoto wa Judah tu na si vinginevyo.Ibrahim kamzaa Isaac na Ishmael na wototo wengine(possibly japo bible imeandika kuhusu Isaac ,na Ishmael kwa kifupi sana)

Isaac ndio kamzaa Jacob na Essau(Biblia ikaendelea kuandika zaidi kuhusu Jacob)

Jacob akapewa miliki(ardhi) na jina Isreal.Akapata watoto kumi na wawili ambao Judah ni miongoni(hawa ndio wayahudi sasa).Sasa ukisema kuanzia kwa Ibrahim mpaka umpate Judah then utoe hitimisho kwamba wote ni wayahudi kwa sababu ya kuwa na babu mmoja ntapinga ndio maana kuna Levites(kutoka kwa mtoto wa Jacob Levi na wengineo)
 
Unafahamu kuwa kuna waarabu pale shinyanga na tabora ambao ni wasukuma?
Muingiliano wa hao watu ndio unaleta huo utofauti. Ukihamia Saudi Arabia, ukaoa na kuzaa hapo na kizazi cha 4 toka wewe kitaitwa ni cha asili gani? Je rangi yao ya ngozi itakuwa black kama wewe au itabadilika,?
 
Uki track kizazi cha Esau kinakuleta Africa. Ndio hapo mkanganyiko unaanza.

Israel ni watoto wa kizazi cha Jacob.
 
Ndio nafahamu lakini huoni unajikanganya yani ni msukuma then ni mwarabu sio? ebu eleza vizuri sema ni mwarabu anayeishi na wasukuma au ni mwarabu anayefata tamaduni za kisukuma hapo ntaelewa lakini utambulisho wake ni mwarabu

Anyway,hoja yako ilikuwa ni hipi sijaelewa kiongozi au ulikuwa unatoa maelezo ya ziada.

Mimi nikihamia Saudia leo hii nkapata mtoto wa kiarabu tukazaa uzao wangu wote watahesabika weusi na watu kutoka taifa la Tanzania ata wangekuwa weupe kupita huo weupe
 
Huu mjadala utatusaidia sana...

Wale wa kulia au kushoto wameukimbia mjadala...

Israel inatokana na kizazi cha Yakobo, kizazi cha Esau kiko wapi?

Yakobo alikuwa na vijana 12 ambao walitengeneza kabila 12 za Israel, Watoto wa Esau hawapo.

Katika watoto 12 wa Jacob, amechaguliwa Judah. Wale 11 wako wapi?
 
Hivi Mfalme Abdullah II wa Jordan ni muarabu au mzungu?
 
Umejibu vizuri. Kama kizazi chako kitaendelea kuitwa watanzania japo ki muonekano ni waarabu basi hao wanaosema kuna waisrael wazungu wana maanisha rangi.
 
Seth saint huo mti wa familia uliouweka hapo ni mahsusi kwa ajili mwisho wa siku kufika kwa Yesu Kristo. Essau uzao wake haufiki kwa Kristo.

Jee Ishmael ambaye Yoda alimtaja hapo awali hakuwa na watoto? Kufupisha maneno ni kwamba tunajadili wayahudi na uyuda kwa wakati mmoja.

Jee kila Myahudi anatokana na Israel na kama Israel ni taifa la watoto 12 kutokutajwa kwa hao wengine kunawatoa kwenye orodha ya watoto wa Israel??
 
Aaaa you wish! Ni sawa na kusema wakristo wa zenj,saudia,misri wanajivunia kuwa na uraia wa nchi zao!we know better Madame!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…