Msuluhishi 1
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 1,318
- 472
Kupeana mikono kwa waislam ni suna, kwa hiyo huwezi ukasema kuwa hupendelei kupeana mikono na wenzio kwa kuwa huo ndio utaratibu wako. Wewe huna ruhusa ya kujitungia utaratibu. wako mwenyewe bali unatakiwa ufuate suna.Sijasema siwapi mkono sababu ya Corona, kutokupeana mikono ni utaratibu wangu nimejiwekea enzi na enzi,
Nimesema sababu ya huu mlipuko wa Corona basi hata Ijumaa siendi kuswali msikitini naswalia nyumbani,
Unatakiwa ufuate utaratibu ule ule aliokuja nao Rasulu Laah sala lahu alaihi wasalam.
Kilichokatazwa ni mwanamke kumpa mkono mwanamume isipokuwa watu maalum.
Pia huwezi ukasema kuwa huendi kwenye sala ya ljumaa eti kwa sababu ya corona.!
Huo utakuwa ni ujuha wa karne. Aliyeleta corona ni Allah. Na Mwenye uwezo wa kuiondosha ni Allah.
Allah akitaka kukuletea madhara, hakuna atayeweza kukunusuru na wala huna hila wala ujanja.
Na Allah akitaka kukuletea neema hakuna wa kuzuia wala kukupinga. Usome Uislamu kijana.
Hata hivyo, mwanamke kwenda kusali sala ya ljumaa sio lazima, kama unaamua kuwa usiende kusali msikitini basi usinde, lakini usiseme kuwa huendi kusali msiikitini eti kwa sababu ya corona.! Huo utakuwa ni unafik.