Waislam tulio wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji n.k

Assalaam alaykum,

Leo bhana wakati nimemaliza kuftari na kushiba basi yakawa yanakuja mawazo kedekede kuhusu mafundisho ya dini....

Nimetafakari nimeona waislam wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji, kuliko kamari na kadhalika! Kitu ambacho binafsi nimegundua sio sahihi kabisa, TUNAKOSEA MNO, hiki ni kiumbe cha Allah mtukufu, na hajatuamrisha tukichukie!

Hiki kiumbe kama vilivyo viumbe vingine kinaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu, "sasaiv" nasikia unaweza kuungwa mguu wake kama wako umekatika🥴 hivyo basi nawasii mno MSIMCHUKIE HANA HATIA KABISA!

Nb:-Allah mtukufu kaharamisha nyama ya nguruwe kuliwa na muumini., kama alivyoharamisha DAMU, NYAMAFU, KAMARI NA ZINAA🙂

Nimeambatanisha na picha ya KIUMBE CHA ALLAH MTUKUFU, kikiwa kimepozi kinakuangalia kwa huruma wewe unaekipiga rungu na kukiua, na wewe unaekichukia bila elimu..! Asanteni kwa kuja🤝

View attachment 3265913
Noah
Meza kubwa
Mbuzi katoliki
Kiti moto
Swine
Mdudu
Kasongo wa kufugwa
 
Kulingana Na Biblia tukiacha Quran (Tuliipumzisha)..

Chuki ya Nguruwe Inatoka Huko..Mnyama aliyeandikwa Ni chukizo kwenu Unamzungumziaje?

1. Mambo ya Walawi 11:7-8
"Nguruwe, kwa kuwa ana kwato, tena kwato zake zimegawanyika katikati, lakini hacheui; yeye ni najisi kwenu. Nyama yao msile, wala mizoga yao msiiguse; hao ni najisi kwenu."

2. Kumbukumbu la Torati 14:8
"Na nguruwe, kwa kuwa ana kwato lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu; msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao."

3. Isaya 65:2-4
"Nimeinyosha mikono yangu mchana kutwa kwa watu waasi, waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe... watu wale wanaokaa katika makaburi, na kulala katika mahali palipofichika; wale walao nyama ya nguruwe, na supu ya vitu vichukizao vi katika vyombo vyao."

4. Isaya 66:17

"Wale wajitakasao na kujisafisha katika bustani, wakimfuata mmoja aliye katikati yao, wakila nyama ya nguruwe yenye machukizo, na panya, wataangamizwa pamoja, asema Bwana."
Maagizo yote haya alikua anapewa nani?
 
Waislamu wanaruhusiwa kula nguruwe hawajakatazwa,ila wale tu kipindi wakikosa chakula kingine.

Ila inavyoonekana majini hayapendi kitimoto.
Mwanadamu ana haki zaidi ya kuishi kuliko kiumbe kingine duniani....hata ikiwa kula mavi itamuongezea uhai mahala pa njaa ANARUHUSIWA
 
Assalaam alaykum,

Leo bhana wakati nimemaliza kuftari na kushiba basi yakawa yanakuja mawazo kedekede kuhusu mafundisho ya dini....

Nimetafakari nimeona waislam wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji, kuliko kamari na kadhalika! Kitu ambacho binafsi nimegundua sio sahihi kabisa, TUNAKOSEA MNO, hiki ni kiumbe cha Allah mtukufu, na hajatuamrisha tukichukie!

Hiki kiumbe kama vilivyo viumbe vingine kinaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu, "sasaiv" nasikia unaweza kuungwa mguu wake kama wako umekatika🥴 hivyo basi nawasii mno MSIMCHUKIE HANA HATIA KABISA!

Nb:-Allah mtukufu kaharamisha nyama ya nguruwe kuliwa na muumini., kama alivyoharamisha DAMU, NYAMAFU, KAMARI NA ZINAA🙂

Nimeambatanisha na picha ya KIUMBE CHA ALLAH MTUKUFU, kikiwa kimepozi kinakuangalia kwa huruma wewe unaekipiga rungu na kukiua, na wewe unaekichukia bila elimu..! Asanteni kwa kuja🤝

View attachment 3265913
Alafu anafanana na nanihii yule wa humu
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Nimetafakari nimeona waislam wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji, kuliko kamari na kadhalika! Kitu ambacho binafsi nimegundua sio sahihi kabisa, TUNAKOSEA MNO, hiki ni kiumbe cha Allah mtukufu, na hajatuamrisha tukichukie!
Kwa bahati Nzuri Mshkaji hanaga baya Na mtu! Yeye na mishe zake Tu za kugawa utamu bila choyo!

Kila siku kashfa dhidi yake haziishi ila Jamaa chati inapanda Tu daily. Long live Kitimoto the Clan
 
Mbona hata kwenye Biblia yenu amekatazwa? Soma
Walawi 11:7-8 Na NGURUWE kwasababu anazo kwato,ni mwenye miguu iliyopasuka kati,lakini hacheui,yeye ni najisi kwenu.Msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.

Au wewe Biblia hausomi? jumapili unaenda tu kuomba toba mbele ya mifuko miwili ya cement na kuondoka kama huyu mwenzako?
downloadfile.png
 
Kulingana Na Biblia tukiacha Quran (Tuliipumzisha)..

Chuki ya Nguruwe Inatoka Huko..Mnyama aliyeandikwa Ni chukizo kwenu Unamzungumziaje?

1. Mambo ya Walawi 11:7-8
"Nguruwe, kwa kuwa ana kwato, tena kwato zake zimegawanyika katikati, lakini hacheui; yeye ni najisi kwenu. Nyama yao msile, wala mizoga yao msiiguse; hao ni najisi kwenu."

2. Kumbukumbu la Torati 14:8
"Na nguruwe, kwa kuwa ana kwato lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu; msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao."

3. Isaya 65:2-4
"Nimeinyosha mikono yangu mchana kutwa kwa watu waasi, waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe... watu wale wanaokaa katika makaburi, na kulala katika mahali palipofichika; wale walao nyama ya nguruwe, na supu ya vitu vichukizao vi katika vyombo vyao."

4. Isaya 66:17

"Wale wajitakasao na kujisafisha katika bustani, wakimfuata mmoja aliye katikati yao, wakila nyama ya nguruwe yenye machukizo, na panya, wataangamizwa pamoja, asema Bwana."
haya makatazo yanahusu nguruwe gani? hawahawa nguruwe wazuri watamu wakuvutia tunaokula kila siku au?
 
Back
Top Bottom