Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Kuna Ka historia wamekatengeneza siku hizi wanakazungusha mitandaoni kuhusiana na Ikulu na Ocean road hospital wakiaminishana vilikuwa ni vya Waislam na vilijengwa na wai, wakati lile jengo pale lilikuwa disigned na John Sinclair, na ndiye aliyesimamia ujenzi wake na ujenzi huo ulifanywa Waingereza mwaka 1922 baada ya jengo la awali lilikuwa limejengwa na wajerumani kuharibiwa na majeshi ya Uingereza.
German ndiyo walianza kuijenga Ikulu baada ya kuamua kuhamisha makao kutoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam, walichofanya ni kununua ardhi kutoka kwa Sultan basi na si majengo
Yaani sultan alikua na ardhi tu hapo bila jengo!?..pale ocean road Kuna msikiti,Kuna kibla,vimetoka wapi!?.. unadhani watu hawajui walikotoka!?..mjerumani alipora ikulu, ikulu ndiyo darulssalaam yenyewe,yaani nyuma ya amani,huku kwingine ni mzizima
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Kwani sheria za nchi hii zinazuia Waislamu kutembelewa usiku na pamoja na vyombo vya habari? Kuna kitu mnakuwa mnafanya usiku mpaka useme mnadharirishwa na hamtaki ushahidi wa media?

Ni kitu gani????
 
Kwani sheria za nchi hii zinazuia Waislamu kutembelewa usiku na pamoja na vyombo vya habari? Kuna kitu mnakuwa mnafanya usiku mpaka useme mnadharirishwa na hamtaki ushahidi wa media?

Ni kitu gani????
Watu walalapo hupunguza mavazi,ni vizuri mkuu wa wilaya kukuvamia saa Tisa usiku kwako na vyombo vya habari?..huyo magoti anatakiwa kunyooshwa
 
Kiongozi lazima uwe na hekima na busara kwa wale unaowaongoza. Petro anaweza kuwa sawa ila njia aliyoitumia kutatua hilo tatizo sio sawa. Ni njia ya kuzua taharuki na kumchonganisha Rais Samia dhidi ya waumini wa kiislam.
Hivi unadhan petro alikurupuka? Unadhani hakuwa na taarifa za nini kinafundishwa pale? Tabu mnafundisha watoto kupigana sasa sijui ili waje kupigana na nani
 
Mkuu wa wilaya ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani,ana vyombo vya kumpa taarifa,hakuota Bali vyombo vilimpa taarifa ndiyo akavamia usiku,yaani kiki kupitia dini ya watu,ajirekebishe
Amevamia usiku? Waislamu bhana 😂
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.


Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Safi sana, Petro Magoti ni kiongozi bora, anastahili kuwa mkuu wa mkoa.
 
Walikua wanasoma shule gani kabla ya kwenda hapo?
Mheshimiwa kasema ni watoto....kwani watoto wanapaswa kuwa shule gani???

Hzo tahfidhu ni kichaka cha kuwanyima watoto haki zao (nazijua vzr) ......heri ungenambia taalim...kule angalau wamekuwa kdg.
 
Yaani sultan alikua na ardhi tu hapo bila jengo!?..pale ocean road Kuna msikiti,Kuna kibla,vimetoka wapi!?.. unadhani watu hawajui walikotoka!?..mjerumani alipora ikulu, ikulu ndiyo darulssalaam yenyewe,yaani nyuma ya amani,huku kwingine ni mzizima
Acheni story, hakuna kitu kama hicho mkuu. Ramani zote za yale majengo designing zipi na history zote zipo zinasema wazi kuhusiana na hayo. Inawezekana majengo yalikuwepo lakini siyo pale. Kumbuka, Sultani aliwekeza zaidi Bagamoyo huko Dar es salaam ilikuwa ni extension tu
 
Kwa mfano hilo lingekuwa kanisa watoto wanafundishwa mazingira mabovu je DC Magoti angelifunga? Je wakristo wangelalamika?Hata kama DC kakosea sawa lakini uongozi wa msikiti ulitakiwa ukamilishe miundombinu kabla ya masomo kuanza.Lililofanyika ni jambo jema Kwa hata wazazi wa watoto wamejua watoto wao wanaishi kwenye mazingira gani
Mm n mkiristo na angefanya hvy kwa Wakristo nngeunga mkono
 
Karo la choo limefunikwa kwa kitambaa cha kitenge na kikaziwa na mawe.
Shehe anawatunza watoto 97 anashindwa kufunika karo na zege.
Hadi magoti anataka kutumbukia
Kuna shida mahali (kichwani)
 
Mkuu wa wilaya ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani,ana vyombo vya kumpa taarifa,hakuota Bali vyombo vilimpa taarifa ndiyo akavamia usiku,yaani kiki kupitia dini ya watu,ajirekebishe
Ndo hivyo.mojawapo ya taarifa aliyopewa ni hiyo kua kuna sehemu watoto wanalazwa kwakulundikwa kama mawe ndo ikabidi aende mwenyewe akashuhudie.Akili zako ni ndogo ndomaana unawaza mambo ya kiki wakati ilo swala linahihusu jamii na lina faida kwenu wenyewe.Labda useme hampendani kwahiyo ata mtoto wa mwenzako akiwa analala pabovu kwako sio shida.
 
Back
Top Bottom