Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Acha kulialia,kati ya dini ambayo ulimwengu unaiogopa na kuichunguza ni uislamu,naungana DC kuwafurusha hao magaidi tarajiwa.

Mbaya zaidi hadi waislamu wengewe wanaigopa,vipi yule DC wa dini yenu aliyebomoa msikiti mwaka jana huko dasilamu!?
 
Mkuu wengine wanafundisha sahihi..shida inakuja kuna wengine sijui wanakuwa na agenda zao.

Wanafundishwa vizuri baada ta hapo sasa kuna kunakuwa na yale mengengine baada ya masomo sumu zinaanza.
Mengine yapi?!
 
Niliwahi jipenyeza kwenye hizi taaluma aisee kuna sumu mno wanalishwa na wasiokuwa na nia njema... Yaani kwa mtoto asiyekuwa na uwezo wa kupembua mambo anaondoka nazo.
Sasa kama hao wengi ni wamefeli darasa la saba tena kwa kizazi hiki.
Wakilishwa stori za kina shehe ilunga kwamba kuna mfumo kristo unatengemea nini?
Au wengine makala za mzee mohamed said kwamba waislamu wanaonewa unategemea nini?
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.


Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Wacheni Serikali ifanye kazi. Watoto ni mali ya Taifa na ni jukumu la serikali kusimamia ustawi wao kijamii na kielimu.

Ni nini unachofundisha watoto 90 kwenye kituo kimoja na wanalala hapo hapo? Mbona mjini kuna madrassa kibao tunaona watoto wanakwenda na kurudi mwakwao?
 
Pamoja mkuu tupinge sote nilienda singida aisee ni hatari..
watoto kama wako jeshini wengine nilikuwa nikikutana nao kitaa nawadodosa ..
Mkuu sumu walizonaso ni hatari.
Aisee mm nngezaliwa kwenye familia ya Kiislamu nisingejutia ila ningefanya namna nihamie Ukristo
 
Karo la choo limefunikwa kwa kitambaa cha kitenge na kikaziwa na mawe.
Shehe anawatunza watoto 97 anashindwa kufunika karo na zege.
Hadi magoti anataka kutumbukia
Kuna shida mahali (kichwani)
Eh hii mbona n kesi nyngn tena ya mauaji, yn Shekhe anataka kumuua bwana magoti kupitia shimo la choo 😂
 
!..nenda ocean road kakague uone,sidhani hata Kama umewahi fika,l
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mpka hapo nitaongea kipi tena mkuu wangu?

ile kanisa pale bandari ulikua msikiti wa wavuvi pale,
Itakuwa Wavuvi waliamua kubadili dini
kumbuka ile bandari Kaanzisha mwarabu,so lazima pawe na msikiti karibu,
Huyu mnamuongelea kama vile ni mzawa na ana stahiki zote katika nchi
mjerumani kachukua nchi kajipa eneo lote la ufukweni,maana wanapenda fukwe
Lakini huyu mnamuongelea kama vile alivyo, yaani mvamizi asiyestahili chochote.
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Tatizo mnataka uislamu uwe na nguvu kuliko serikali,hapo angekuwa kafanya hivyo muislamu mwenzenu mngekaa kimya ila kwakuwa aliyefanya ni mkristo mmeshaiona hiyo ni issue ya kidini....
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mpka hapo nitaongea kipi tena mkuu wangu?


Itakuwa Wavuvi waliamua kubadili dini

Huyu mnamuongelea kama vile ni mzawa na ana stahiki zote katika nchi

Lakini huyu mnamuongelea kama vile alivyo, yaani mvamizi asiyestahili chochote.
Mwarabu alifika siku nyingi kabla ya mngoni,akazaliana na wenyeji
 
Back
Top Bottom