Waislamu 11 Wakamatwa Nigeria kwa kutokufunga Mfungo wa Ramadhani

Waislamu 11 Wakamatwa Nigeria kwa kutokufunga Mfungo wa Ramadhani

Polisi wa Kidini nchini Nigeria wamekamata watu 11 siku ya Jumanne kwa kuonekana wakila chakula mchana katika mwezi wa Ramadhani.

Watu hao wamekamatwa katika jimbo la kaskazini la Kano.

Kano ina idadi kubwa ya Waislam, ambapo sheria ya kidini – Sharia- inatumika pamoja na sheria za kawaida za nchi.

Polisi wa Kiislam, maarufu kama Hisbah, hufanya misako katika maeneo ya chakula na masoko wakati wa Ramadhani.

Wanaume 10 na mwanamke mmoja waliokamatwa, waliachiliwa huru baada ya kuapa kuwa hawatoacha kufunga bila sababu muhimu.

“Tulikamata watu 11 siku ya Jumanne, akiwemo mwanamke mmoja muuza karanga aliyeonekana akila na watu wakatujulisha,” amesema msemaji wa Hisbah Lawal Fagge, akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC.

“Wengine 10 ambao ni wanaume walikamatwa mjini karibu na masoko ambapo kuna shughuli nyingi.”

Ameongeza kusema msako utaendelea lakini amesema wasio Waislam hawahusiki na msako huo.
Tushukuru kuwa na nchi nzuri km TZ
 
Kama unashindwa kukishinda kishawishi cha jirani yako anapokula utaweza kuvumilia pisi ikikufunulia upaja?!

IKO WAPI IMANI YAKO?
 
Kwamba ukijitangaza huna dini halafu ukala mchana hakuna ataekusumbua? Unataka uwaingize cha kike?
inategemea, ikiwa umekatazwa kula hadharani basi kwani kuna shida gani kama utakula ndani kwako au kwenye hoteli?
 
Sawa, wasio waislam hawahusiki kukamatwa wakila, nigeria kaskazini wana vituko sana vya dini hiyo. Huku kwetu kuna msikiti mkubwa mjini na nje kwenye fremu zake kuna mgahawa mkubwa chakula kinaliwa mchana kama kawaida. Nilikuwa na wasiwasi kwamba mgahawa huo huenda ungefungwa kipindi hiki cha mfungo kutokana na kuwa fremu hiyo ni mali ya msikiti huo. Migahawa mingi ya waislam imefungwa kipindi hiki cha mfungo. Huenda mmiliki wa mgahawa huo si muislam na hajapewa shinikizo la kufunga mgahawa huo hapo msikitini. Waislam wa tanzania bara wameanza kuachana na itikadi kali za kidini
 
Huyu Mungu wa Hawa washkaji kama hajapitia Jkt, basi atakuwa hata Mgambo amecheza. Haiwezekani wafuasi wake wawe na operation za nguvu na lazima kuulazimisha watu wamfuate
 
SAUMU YA RAMADHANI

Kufunga Saumu ni nguzo ya nne ya Kiislamu na hakika ya Kufunga ni kuacha kula na kunywa toka asubuhi mpaka magharibi kama Mungu alivyoamrisha. Na kuacha kila mambo mabaya, kama Qur'an tukufu isemavyo kwamba:-

يٰٓـاَيُّهَا الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡا كُتِبَ عَلَيۡکُمُ الصِّيَامُ کَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِيۡنَ مِنۡ قَبۡلِکُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُوۡنَۙ‏

Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga Saumu kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.

Kusudi la Saumu limeelezwa kuwa ni kupata Taq-waa, yaani, ucha-Mungu. Neno Taq-waa, linatumiwa katika Qur'an kwa maana tatu:
(1) Kuepukana na maumivu,
(2) kuepukana na dhambi,
(3) kufikia utakatifu ulio juu wa mambo ya kiroho.

Kufunga saumu ya Ramadhani ni lazima juu ya kila Mwislam isipokuwa watoto wadogo, wagonjwa, wadhaifu sana, wenye mimba, wanyonyeshao na wasafiri.

Ijapokuwa hakuna adhabu ya kimwili ikiwa mtu ataamua kutofunga, ila Mwenye kuacha kufunga saumu ya Ramadhani bila udhuru wowote anapata dhambi kubwa na mwenye kufunga kisha akafungua bila sababu basi juu yake afunge siku sitini kwa mfululizo, au alishe maskini sitini.

Mwezi wa Ramadhani ni mwezi mtukufu zaidi kwenye kalenda ya mwaka wa kiislamu. Ni mwezi pia unaofahamika kama mwezi wa toba, kipindi ambacho waumini wa dini hiyo wanajisogeza karibu zaidi na Mola wao kwa ibada mbalimbali ili wavune thawabu.

Ni dhahiri pia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kunakuwa na mabadiliko mengi katika mfumo wa maisha na matendo ya watu.

Katika nchi ambazo raia wake ni wa dini mbalimbali kama Afrika Mashariki, maswali mengi huibuka kipindi hiki juu ya nini kinatakiwa kifanyike ama kisifanyike. Wale ambao si waislamu huwa na maswali mengi juu ya nini wanaweza kufanya ama kutofanya mbele ya ndugu, jamaa au marafiki wa kiislamu.

Tendo kubwa ambalo linaonekana moja kwa moja kufanywa na waislamu katika kipindi hiki cha mfungo ni kujizuia kunywa na kula kutoka alfajiri (kuchomoza kwa jua) mpaka magharibi (kuzama kwa jua).

Haijalishi, mtu awe masikini ama tajiri, awe na chakula ndani ama asiwenacho, madhali wanakiri kwa yakini kuwa ni waislamu basi hujizuia kula na kunywa.

Katika mazingira yenye watu wa imani tofauti, mathalani mtaani, shuleni au hata kazini sio wote wanaofunga, na wengine hutembea na vyakula vyao.

SWALI HUWA, JE, NAWEZA KULA MBELE YAKO AU MBELE YA WATU WENGINE?

Jibu lake hutegemeana na mtu na mazingira husika. Kuna wale ambao hawana tatizo lolote kwa mtu kula mbele yake anapokuwa amefunga, ila wengine wanatafsiri ukifanya kitendo hicho kama kutowaheshimu na kuwapa majaribio ya kiimani kwa makusudi. Kama upo kazini ama shuleni, ni vyema zaidi ukatumia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa chakula.

Mazingira ya eneo pia huchangia katika hili. Katika nchi nyingi ambazo zinafuata sheria za kiislamu, kula hadharani wakati wa mchana wa mwezi wa Ramadhani huwa ni kosa. Na ukifanya hivyo unaweza kujipata mikononi mwa vyombo vya usalama, Ambapo jambo hili sio sheria wala sio Fundisho la Islam sawa na Mtukufu Mtume Muhammad saw alivyotuelekeza na Kutufundisha.

Ndiyo maana Ramadhani kwa hakika inahusu kujiboresha katika ngazi zote: kujenga uhusiano wa kina zaidi na Mwenyezi Mungu, kutimiza vyema haki za wanadamu wenzetu, na kurekebisha maadili na matendo yetu wenyewe ili kuwa watu bora zaidi.


RUHUSA ZA MTU KULA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI.

1️⃣ Ugonjwa
Yaruhusiwa kwa mgonjwa kula ndani ya mwezi wa Ramadhani; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

اَيَّامًا مَّعۡدُوۡدٰتٍؕ فَمَنۡ كَانَ مِنۡكُمۡ مَّرِيۡضًا اَوۡ عَلٰى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنۡ اَيَّامٍ اُخَرَؕ وَعَلَى الَّذِيۡنَ يُطِيۡقُوۡنَهٗ فِدۡيَةٌ طَعَامُ مِسۡكِيۡنٍؕ فَمَنۡ تَطَوَّعَ خَيۡرًا فَهُوَ خَيۡرٌ لَّهٗ ؕ وَاَنۡ تَصُوۡمُوۡا خَيۡرٌ لَّـکُمۡ اِنۡ كُنۡتُمۡ تَعۡلَمُوۡنَ‏

Kwa siku zilizohesabiwa. Lakini miongoni mwenu awaye mgonjwa au katika safari, basi atimize hesabu katika siku zingine. Na wale wanaoweza, watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya wema kwa radhi ya nafsi yake, basi ni bora kwake; na kama mkifunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.

2️⃣ Safari
Inaruhusiwa kwa msafiri kula ndani ya Mwezi wa Ramadhani, na inamlazimu kuilipa saumu hiyo baadaye, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

اَيَّامًا مَّعۡدُوۡدٰتٍؕ فَمَنۡ كَانَ مِنۡكُمۡ مَّرِيۡضًا اَوۡ عَلٰى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنۡ اَيَّامٍ اُخَرَ

Kwa siku zilizohesabiwa. Lakini miongoni mwenu awaye mgonjwa au katika safari...

3️⃣ Wajawazito na Wanyonyeshao n.k
 
Polisi wa Kidini nchini Nigeria wamekamata watu 11 siku ya Jumanne kwa kuonekana wakila chakula mchana katika mwezi wa Ramadhani.

Watu hao wamekamatwa katika jimbo la kaskazini la Kano.

Kano ina idadi kubwa ya Waislam, ambapo sheria ya kidini – Sharia- inatumika pamoja na sheria za kawaida za nchi.

Polisi wa Kiislam, maarufu kama Hisbah, hufanya misako katika maeneo ya chakula na masoko wakati wa Ramadhani.

Wanaume 10 na mwanamke mmoja waliokamatwa, waliachiliwa huru baada ya kuapa kuwa hawatoacha kufunga bila sababu muhimu.

“Tulikamata watu 11 siku ya Jumanne, akiwemo mwanamke mmoja muuza karanga aliyeonekana akila na watu wakatujulisha,” amesema msemaji wa Hisbah Lawal Fagge, akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC.

“Wengine 10 ambao ni wanaume walikamatwa mjini karibu na masoko ambapo kuna shughuli nyingi.”

Ameongeza kusema msako utaendelea lakini amesema wasio Waislam hawahusiki na msako huo.
Hawa Waislam ni janga la Dunia. Ona huyu mwingine akimfokea mdada wawatu wakiwa kwenye basi ati kwanini anakula wakati yeye amefunga. Mijinga kweli hii mijitu

View: https://x.com/TheHarrisSultan/status/1773467199975657597?s=20
 
Back
Top Bottom