Jinsi muhamad alipata Utume toka kwa Majini.
itume wa Yesu ndani ya Biblia Takatifu walikwisha kutuonya kuhusu uchafu huo. Katika 2 Kor 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
Miongoni mwa mafundisho ya Muhammad ni kwamba kuna mambo kumi yanayokamilisha Uislamu nayo tunayasoma katika kitabu kiitwacho
Mkweli Mwaminifu , Kilichoandikwa na Sheikh Said Moosa Al-Kindy wa Muscut, Juzuu 3-4 Uk 63.Hadithi Na.880 “ Kasema Mtume (s.a.w) (Mambo) kumi ya Uislamu (yanayokamilisha Uislamu):Kukata masharubu,na kuziweka ndevu,nakuziweka ndevu (kutozinyoa) ndevu,na kupiga mswaki,kusafisha ndani ya pua kwa maji,na kukata kucha,kuosha mikono baina ya vidole,na kung’oa (au kunyoa) nywele za kwapani,na kunyoa nywele za mbeleni (mavuzi),na upungufu wa maji. La kumi,kasema sahaba aliepokea hadithi hii kuwa nimesahau,lakini kasema bila shaka la kumi ni “kutahiriwa.”
Kwa mujibu wa Biblia manabii na mitume wanathibitishwa kwa njia ya miujiza.
Kutoka 14:21” Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari,BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki,usiku kucha,akaifanya bahari kuwa nchi kavu”.
Matendo 19:11-12 “Mungu alifanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida . Hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka”. Tazama pia Matendo 16:16-18, 20:7-12 na Matendo 13:6-12.
Qur’an nayo inathibitisha kuwa manabii na mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini] inasomeka “Na kwa yakini tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”
Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur’an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). “Na walisema “Mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi),nami hakika ni mwonyaji mbainishaji (dhahiri tu).” (Taz. Qur,an 6:35-37 13:7,)
Katika Qur’an iko aya ambayo tunapaswa tuitafakari wote kwa pamoja.Katika Surat An-Nisaa, (wanawake), 4:79 “Wema uliokufikia unatoka kwa Mwenyezi Mungu na ubaya uliokufikia unatoka nafsini mwako, mwenyewe umefanya mambo hata yakakufika hayo. Nasi tumekupeleka kwa watu kuwa mtume na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha (hapaitajiwi shahidi mwingine)”
Aya hii inaonesha kuwa Muhammad mtume wa Waislamu, alipelekwa kwa watu kuwa mtume, huku Mwenyezi Mungu akiwa shahidi tu. Siku zote shahidi si mtendaji bali ni mwonaji tu wa tendo lililotendeka.Hoja yetu tungependa kuwajua hao watu waliompeleka Muhammad kwa watu ni akina nani?. Kwa sababu tumeona kule nyuma baada ya Muhammad kutoka pangoni, mkewe Bi. Khadija anamwambia Muhammad kuwa “utume huo!!!!!!! Na Bwana Waraqah ibn Naufal akimwambia Muhammad kuwa “ basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu” kabla ya Qur’an .Je hao si wale “Nasi tumekupeleka” wanaotajwa kwenye aya hiyo hapo juu? Tafakari!! .
Waislamu hudai kuwa Muhammad ametumwa na Mwenyezi Mungu wao, ambaye ni Mfalme wa Wafalme . Lakini tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha Ufunuo 17:14 “ Hawa watafanya vita na Mwanakondoo, na Mwanakondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; na hao walio pamoja naye ndiyo walioitwa na wateule, na waaminifu”
Katika Ufunuo 19:11-16 “ Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
Yesu Kristo ndiye Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana.Lakini tunaposoma Hadithi sahihi za Kiislamu zinaeleza kuwa adui mkubwa wa Allah (s.w) Mungu wanayemwabudu Waislamu, ni yule anayeitwa Mfalme wa Wafalme.
Sahih Al- Bukhari, Vol.8.Hadithi Na.225, Al-Lu’lu Wal-marjan,Juzuu ya 3,Hadithi Na.1385 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema,Mtume wa Allah (s.a.w) amesema,”Majina yaliyo dhalili mno na mabaya mbele za Allah ni mtu kujiita,Malikil-Amlaak (Mfalme wa Wafalme).”
Hivyo, ufunuo aliopokea Muhammad, ambao anatutaka na sisi Wakristo tuuamini haujatoka kwa Mungu tunayemwamini sisi Wakristo, yaani, Yesu Kristo.Bali kama alivyonukuliwa katika vitabu vya Kiislamu, unatokana na kuchezewa na Shetani, na kwa sababu hiyo kwetu anakuwa nabii na mtume wa uongo’
Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo”
Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo. Hatufai