Waislamu mliofanikiwa kwa Elimu ya Shule za Mission badala ya Madrasa kuweni na Shukrani kwa Wakristo waliowafikisha hapo mlipo

Alone yule mzee wa kutetea wazee wake wa Kariakoo Mohamed Said
Stux...
Mimi sitetei.

Utetezi unakuja kwenye shutuma.

Nimeandika kitabu cha historia.
Huu si utetezi.

Mimi nimeandika historia ya wazee wangu katika juhudi za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wengi wa wazee hawa wanatoka Kariakoo na baadhi Gerezani.

Lakini kitabu cha Abdul Sykes ambacho ndiyo msingi wa mjadala hapa JF kimeeleza historia ya wazalendo wengine kutoka majimboni mfano wa Ali Juma Ponda, Hassan Suleiman, Haruna Iddi Taratibu kwa kuwataja wachache kutoka Central Province, Dodoma.

Kwa hali ya kawaida haiwi mtu aandike maisha ya wazee wake atoke mtu apinge.

Hili si jambo la kawaida.

Hili limekuwa hivi kwa watu kujitokeza na kutaka kukipinga kitabu changu kwa sababu moja tu.

Historia ya wazee wangu imemuhusu Julius Nyerere.

Hili limewachoma moyo wengi.

Sababu ya kuwachoma moyo ni ule mshtuko walioupata baada ya kusoma historia iliyokuwa na mvuto wa kipekee ikieleza mchango mkubwa wa wazee hawa kwa Nyerere binafsi na katika harakati za kupigania uhuru.

Vinginevyo kitabu cha Abdul Sykes kingekuwa kitabu kama vitabu vingine.

Kitabu kingesomwa na baada ya muda kusahaulika.

Huu ni mwaka wa 25 kitabu cha Abdul Sykes kinapata wasomaji wapya kila uchao na kila akisomae kinamsisimua.
 
Huyu ni mzee Mohamed Said , ana jukwaa lake rasmi la kupiga propaganda za kijahidina
Stux...
Mimi si mtu wa propaganda.

Nimo katika Dictionary of African Biography kama mwandishi (2011).

Nimo katika Nyerere Biography (2020).

Niko kwingi.

Nimezungumza kwenye vyuo vikuu ndani na nje ya mipaka yetu kuhusu historia ya Tanganyika.

Hivi si viwanja vya propaganda.

Kinachokuumiza wewe ni kusoma historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
P,
Hii ni makala ndefu lakini ina vitu viwili muhimu kwa wasomaji na kwa swali lako kama nashukuru kwa elimu niliyopata katika shule za Misheni.

Makala hii yumo mwalimu wangu aliyenifunza lugha ya Kiingereza St. Joseph's Convent School, Dar es Salaam.

Nimemtaja.

Makala hii inanieleza mimi na dunia yangu:

MAHOJIANO NA MOHAMED VALL WA AL JEZEERA 2007

Jana nilikuwa naangalia Al Jazeera yanayotokea Gaza mara nikamuona mtangazaji wa Al Jazeera, Mohamed Vall anatangaza habari za vita hivi.

Mohamed Vall akanikumbusha mahojiano tuliyofanya nyumbani kwangu Dar es Salaam na Tanga kati ya mwaka wa 2007 na 2008.

Hiki ni kisa cha kipekee katika maisha yangu ya kuhojiwa na vyombo vya habari.

Al Jazeera ilituma waandishi wake wakiongozwa na Mohamed Vall kuja Tanzania kufanya naamini ''documentary.''

Walinipigia simu Tanga na kuniuliza kama naweza kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano au wao wanifate Tanga.

Nilikuja Dar es Salaam na wakafika nyumbani kwangu asubuhi kwa kuangalia mandhari ya nyumba yangu na kuipanga kwa namna waitakayo wao kwa ajili ya kufanya kipindi.

Kwa ufupi walibadilisha muonekano wa ukumbi wangu waliporidhika wakanifahamisha kuwa watarejea usiku kwa ajili ya mahojiano.

Mohamed Vall ndiye aliyenihoji na tulifanya kipindi cha takriban saa moja.

Tulizungumza kitu gani?
Al Jazeera walitaka kujua historia ya Waislam wa Tanzania.

Katika team yao kulikuwa na kijana mmoja yeye aliniambia kuwa ni Mtanzania na akinifahamu kwa miaka mingi sote tukiwa watoto Kinondoni.

Kwa hakika sura yake haikuwa si ngeni na alikuwa na muonekana wa Kisomali.

Nakumbuka kipindi kizima nilichokuwa nahojiwa mwanangu wa kwanza alikuwa kasimama mbele yangu sawasawa na mimi akiniangalia.

Sijui nani alimtuma kunikalia mbele yangu lakini kwa namna ya ajabu sana yeye akawa kama kioo cha mimi kujiangalia na kujitathmini.

Kila nilivyokuwa nikizungumza nilikuwa namuona kwa jicho langu la pembeni akitabasamu na wakati mwingine akitingisha kichwa kama kusema, ''Ahsante,'' au ''Hakika,'' nk.

Sura ya mwanangu ilikuwa kama vile inaniambia kuwa maneno yangu niliyokuwa nasema yalikuwa mazuri yamamfurahisha.

Mwanangu alinikumbusha siku nafanya mtihani wa English Oral, Mtihani wa Cambridge 1970.

Siku zile tulikuwa tukitihaniwa Kiingereza kwa kuzungumza mbali na mtihani wa kawaida wa kujibu maswali kwa kuandika.

Mwalimu wangu wa English na Literature Miss Menez, msichana wa Kigoa siku ile alikuwa katika chumba cha mtihani na alikuwa kaweka kiti chake sawa na mimi uso kaukunja ananiangalia na kunisikiliza.

Nakumbuka jana yake wanafunzi wa Literature alituita na kutuambia kuwa ikiwa sisi wanafunzi wake hatukupata Merit Pass yaani First Class basi na yeye pia atakuwa kafeli mtihani.

Nilipokuwa najibu maswali nilimuona Miss Menez, wanafunzi sie kwa utundu wetu tulimpa jina, ''Lanky,'' kwa ajili ya urefu na wembamba wake.

Sijua nani alikwenda kumuambia.

Siku moja darasani akatuambia huku akicheka kuwa anajua jina tulilompa.

''So my golden class you have given me a nickname...''

Turejee kwa Al Jazeera.

Kila mazungumzo yalivyokuwa yanasonga mbele nilikuwa nawaona watu wa Al Jazeera ambao kwa hakika ndiyo walikuwa hadhira yangu walikuwa kama vile wanazamishwa na yale niliyokuwa nasema.

Sura zao ukiziangalia walikuwa wanafuatilia kila sentensi niliyokuwa naitoa.

Historia ya Waislam na uhuru wa Tanganyika na yaliyotokea baada ya uhuru siku zote imekuwa kisa cha kupendeza na kuvutia kusikiliza.

Mohamed Vall nakumbuka swali lake la mwisho aliniambia kuwa kesho alikuwa na mahojiano na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu.

Je, anaweza kuninukuu na kumuuliza maswali Rais kutafuta ukweli kwa yale niliyozungumza?

Jibu langu lilikuwa anaweza.

Baada ya kumaliza mahojiano haya wale vijana walinipongeza wakisemea kipindi kilikuwa kizuri sana.

Nilisubiri kwa muda mrefu kipindi kirushwe.

Hakikurushwa.

Baadae zikanifikia taarifa kuwa baada ya kumaliza kufanya vipindi Tanzania Bara walikwenda Zanzibar kwa mahijoano mengine.

Tape zao za vipindi vyote walivyofanya Tanzania Bara na Visiwani vilipotea hotelini Zanzibar.

Baada ya mwaka mmoja hivi Mohamed Vall na wenzake walirudi tena Tanzania na wakaja Tanga kwa mahojiano.

Sijui nini kilitokea safari hii.
Kipindi hakijaenda hewani hadi leo.

Picha ya mwisho ni mahoajiano na Mohamed Vall Tanga, Bombo Area 2008 nyingine ni mahojiano Dar es Salaam, Masaki 2007.


Mahojiano na Al Jazeera Dar es Salaam
2007​
 
Tofauti iliyopo kwenye hizi Dini mbili ni kuwa moja ina uvumilivu wa kidini nyingine haina Kabisa au ni mdogo mno! Mojawapo inafundisha kupendana baina yao ...! Kuna kijana mmoja wa dini mojawapo huwa ananipeleka mahali . Yule kijana alishangaza akawa anasalimias vizuri na mmoja wa wadada wa Dini yake, kama vile wanafahamiana siku nyingi!
Ilibidi nimuulize kama ana mfahamu! Akakana!
Msingi wa hoja ya mleta mada upo ktk Uvumilivu wa kiimani!
 
Tuanze na yule mzee Said,hakika shukrani ya punda ni mateke.
 
Kitu ambacho P hajakielewa ni kuwa Waislam wanatilia mkazo sana suala la Elimu ya Dini kwasababu kupitia Elimu hii unapata MUONGOZO wa Kuishi dunian na ustaarab pia lakn Kwa Wakristo kusoma Bible knowledge sio lazma maana kila ktu wamewaachia Viongozi wa Dini
 
Yani m sijawahi ona mkristo mwenye akili sawasawa

Embu fikiria professor mtu na elimu yake anaenda kudanganywa na standard 7 failure kwa mahubiri ya uongo hlf anaacha millions ety za mchungaji ivi wakristo mna akili kweli nyinyi?

Ukishakua kafiri ww ni wa hapa hapa tu duniani ndo mna mumepewa ufakhari mkubwa hpa duniani makafiri ila mbinguni kma msemavyo hamna lenu jambo

Chuki zenu zimejificha sanaa lkn sasa ona ata huyu alokua mtangazaji maarufu ameshaitokeza chuki yake hadharani
 
Wewe una powers fulani!, baada ya wewe kumuulizia humu ile Alasiri m, leo usiku amenitafuta, she just lost her dear mother!.
P
Pole sana Pascal. Obviously, si unakumbuka mazoezi ya Yuri Gerard (yule Mrusi kama nimepatia spelling), ulikuwa na kitabu chake cha "will power" na mimi baada ya kukisoma nilikuwa najaribu ku'practise'.
 
Miji ipi hiyo iliyoendelea yenye waislamu wengi?mana kama dsm itoe katika hilo.
 
Kwahiyo wanaoenda kumpiga mawe shetani mecca na madina kule wao ndio wana akili kubwa.

Saudia wanazidi kuwa matajiri kwa pesa za wajinga wengi ulimwenguni kwote
 
 
Kwan Uksristo ni din gan? Na umeletwa na nan? Kwa lengo gan? Naona jamaa anamajibuno kwel mda mwengine haitaj uende shule
 
Asante sana mkuu, na hilo ndio lilikuwa lengo haswa la kuwaelimisha wa upande wa pili
Sisi tunafundishwa mengi sana ambayo ni maisha halisi

Tulikatazwa kusema uongo kwa vitendo yaani fimbo
Hata nidhamu na heshima
Sasa wao wengi wamesoma ili waje kuiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…