Waislamu Mnafeli wapi?

Mfano wako wa mtu shambani uko very clear
 
Na hujajibu swali langu
Kwamba kabla hujazaliwa ulikuwa hai?
Nakuja kukujibu
 
"Mtu mtumwa shambani mwako"

Ni wapi niliposema kwamba mwenyezi Mungu akampa huyo mtu aliyemuumba jembe na zana za kilimo akamwambia kuwa lima na mazao yote nayahitaji mimi nitakupa chakula tu??

Wewe ulihitaji uhuru upi? Uwe na mbawa?

Unataka uwe na uhuru wa kuchagua mahali pa kuzaliwa

Rejea
Kutoka 20:12
Na jibu hili swali kwamba ulikuwa hai kabla hujazaliwa??
 
Mfano wako wa mtu shambani uko very clear
Nashangaa wanaojifanya hawaelewi hawaelewi nini.

Ukweli kwamba watu hatupewi uchaguzi wa kuamua tuzaliwe au tusizaliwe, kabla ya kuzaliwa, unaondoa kabisa hoja ya kwamba tuna uhuru wa uchaguzi.

Hatuna hata uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, hatuna uhuru wa kuchagua tunazaliwa wapi, na wazazi gani, na vinasaba gani, mwaka gani etc.

Haya ni mambo yanayokuja kuathiri maisha yetu sana.

Sasa kwa nini tunajidanganya kwamba tuna uwezo mkubwa wa kuchagua mambo ikiwa hata hatuna uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa, kuzaliwa wapi, kuzaliwa lini, kuzaliwa na wazazi gani etc?
 
Kwa hivyo uhuru wa kuzaliwa ndio unaouhitaji??

Na je uhuru a kuishi?
Kupumua?
Kufanya yale utakayo katika ardhi uliyopo?

Kama unahitaji uhuru hup jibu kwanza swali hili

Ulikuwa hai kabla ya kuzaliwa??
Namalizia ka kusema kwamba

Mwanao hawezi kuwa na sauti zaidi yako kama anaishi kwako bado
 
Mungu wako anawalazimisha watu wafanye kazi bila ya watu kusaini contract ya kukubali hiyo kazi. Halafu unasema huyu Mungu kawapa watu uhuru wa kuchagua.

Wewe unaona hili jambo limekaa sawa?
 
Kwani ni wapi walipoandika kamba mwenyezi mungu alimuagiza mtu huyo afanye kazi katika shamba lake??
Kwa ajili yake??
Wewe hata hujaelewa analogy.

Inawezekana ndiyo sababu hatuelewani.
 
Mungu wako anawalazimisha watu wafanye kazi bila ya watu kusaini contract ya kukubali hiyo kazi. Halafu unasema huyu Mungu kawapa watu uhuru wa kuchagua.

Wewe unaona hili jambo limekaa sawa?
Ulipozaliwa ulisaini Contract?

*Rum 1: 28
 
Ulipozaliwa ulisaini Contract?

*Rum 1: 28
Hivi mpaka sasa hujaelewa swali langu?

Sijasaini.

Kwa nini Mungu wako hakunipa nafasi ya kusaini contract niingie katika maisha haya kwa kukubali mwenyewe?

Kwa nini nimejikuta nimezaliwa tu bila mimi mwenyewe kukubali kuzaliwa?

Hujajibu swali hili.

Na kama sikuwa na uchaguzi wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe, utasemaje nina uchaguzi baada ya kuzaliwa?
 
Yohana 1:13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Hakuna aliyejichagulia kuzaliwa hapa alipo leo kwa maana n Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo kwa maana anafahamu toka mimba zetu hzijatungwa mpaka siku zinakufa sisi tutakuwa watu wa aina gani.

Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake lakini huzaliwa kiroho kwa mapenzi yake. Na huo ndio uhuru uliokuwa unauhitaji
Naona hizi reference nazoweka huzisomi.
 
Nakuuliza, kwa nini Mungu hatupi nafasi ya kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe?

Unaandika, Mungu hatupi nafasi ya kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Hapo hujajibu swali, umekubali tu Mungu hatupi nafasi ya kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Na kama hajatupa nafasi ya kuchagua katika hili, huwezi kusema katupa nafasi ya kuchagua.
 
Mkuu una hoja za msingi sana unafafanua kwa lugha inayoeleweka.

Sema mara nyingi mnaojadiliana nao hawataki kukubali kuelewa
 
Mungu hatupi nafasi hiyo kwa sababu
Yeye ndio mpangaji wa kila kitu na ndio muamuzi wa kila kitu katika dunia hii
 
Kwani ni wapi walipoandika kamba mwenyezi mungu alimuagiza mtu huyo afanye kazi katika shamba lake??
Kwa ajili yake??
Huo ni mfano kuhusu hoja ya kuwa huru kuchagua mkuu. Si mstari wa biblia wala maagizo ya mungu
 
Wewe nani kakutuma kusema haya hivi kwa Wakristo Lucifer mnamtaja sana ni shetani mkuu mnawasingizia waislam sana.
Hivi unaijua Freemason na siri ya msururu wa madhehebu ya wakristo
Katoliki, Lutheran,presbyterian,wasabato, Anglican,Menonite,Living water n.k
Hivi unajua kwenye mlima wa Zayuni shetani alisema nitawaingilia huko kwenye makanisa Yao?
Hivi unajua madhehebu ya wakristo ya walokole yalianzia marekani mji wa Kansas city mwaka 1904 kama watu wanao rap kwa kuamini ili umuabudu mungu unatakiwa kupiga makelele usikike wakati ukweli ni kwamba unaweza muabudu mungu kimya kimya.
Wakristo msiwasingizie waislam issue za majini wakati freemason ipo.
Uislam ni dini ya amani.
Kula ugali wako lala abudu mungu wetu mmoja usihoji vingine
 
Kwani mkuu unadhani Mimi nipo upande gani
 
Umekuwa unaikumbatia Sana hoja ya Uhuru WA kuchagua kuzaliwa,naona hii ndo inakubeba Sana

Naomba unijibu swali hili!

Je unakuwa hai Kwanza kabla ya kuzaliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…