Waislamu Mnafeli wapi?

Waislamu Mnafeli wapi?

Shida ipo sehemu moja tu wakristo wengi hawana elimu juu ya uislam kwaiyo wanamezeshana propaganda sana juu ya uislam.

Lakini bado sioni tatizo kuitwa wafuga majini kama ufugi uwezi chukia kitu ukiona unakasilika ujue unayafuga.
Swadakta Al habib
 
Kumekuwa na dhana kwamba waislamu wanafuga majini kitu ambacho si kweli kabisa na hata Dini hairuhusu hivyo.

Mwenyezi Mungu anasema hakuumba majini na watu Ila isipokuwa wamwabudu Mola wao,ebu tuangalie Maandiko;

((Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.))
51:56

Kwahiyo Majini na wanadamu waliumbwa Kwa lengo moja Tu la kumwabudu Mola wao na sio vinginevyo.

Lakini bahati mbaya Sana kuna baadhi ya waislamu ambao hushirikiana na majini katika mambo Yao,na hii sio waislamu Tu hata baadhi ya watu ambao sio waislamu hufanya hivyo pia,iwe Kwa kupiga ramli,kufanya miujiza huko kwenye nyumba za ibada na kadhalika.

Ila mazungumzo yangu Leo hapa nazungumza na waislamu, kuna baadhi ambao huwa na haya maruhani/majini ambayo wenyewe huyaita majini Waziri kwakuwa Tu yanawasaidia katika mambo Yao. Naomba niwaambie kuwa hakuna majini mazuri ambayo yanakaa mwilini mwa mtu hata kidogo,hayo ni mabaya na machafu,jini ambaye ameumbwa ili kumwabudu Mola wake hawezi kuja kufanya makazi katika mwili WA mtu kwakuwa hayo ni makosa na amekiuka sababu ya kuumbwa kwake kabisa.

Wanao mwabudu Mola wao wapo kwenye makazi Yao ya kijini na wanaendesha Maisha Yao huku wanamwabudu Mola wao,kwahiyo acheni kuwa watumwa WA hayo majini,kwani hakika mwisho wenu utakuwa sio mzuri.

Ebu tuangalie maongezi haya ya majini kama yalivyoelezwa katika Qur'an ;

((Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.))
72:6


Haya ni maongezi ya Majini baada ya kusikia Qur'an na kumwamini Mola wao,ndio wanahadithia kuwa kuna wanadamu wanaume ambao walikuwa wanatafuta hifadhi toka Kwa majini lakini matokeo yake wakazidishiwa madhambi. Na huo ndio ukweli kuna watu ambao wanaamini majini kuwa ndio watawalinda hapa duniani,na huwa hawafanyi Jambo lolote mpaka washaurieni na majini wao,hakika hiyo ni kufuru kubwa kumwamini kiumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa ndio anakuwezesha kufanikiwa Kwa mambo hapa duniani.

Na mwisho wa siku shetani/ hayo majini machafu ambayo yameacha kusudio la kuumbwa kwao na kuja kushirikiana na wanadamu,mwisho wa siku yatawakana na kuwaambia ukweli, tuangalie Aya ifuatayo;

((Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu.))
14:22


Hakika kuna Aya nyingi Sana juu ya majini kuwapotosha wanadamu na kuwaingiza Motoni,kubwa ni kujua kwamba hakuna majini ambao wanatakiwa kushirikiana na binadamu kwani wao Wana Maisha Yao na wanadamu tuna yetu,ushirikiano wowote baina yetu ni upotovu na mwisho wake ni jehenamu.

Mambo mengi na Mda ni mchache!

Ni hayo Tu!
Shukrani kwa darsa👏
 
mwenyezi mungu anasema anayetaka maisha ya dunia atampa na atakuacha ujilie raha ya mchongo ya dunia ila tambua ahera huna chako..kupanga ni kuchagua mkuu
Aaah kasema wapi hii?
Kwahyo nisifuge kuku ili nipate hela nikala raha za dunia kwasababu ntakosa ahera?
 
Ni Kama dhambi zingine tu,ukute anayeshitikiana na jinni hanywi pombe,hazini,hachezi kamari...Ila hakuna uchawi usiohusisha jinni,wengine wanaita mizimu,Ila ndiyo jinni haohao
Mimi nna Rafiki yangu wa kijini, ila yeye Ni wa ibada Sana, na hakai mwilini mwangu, ila huwa anakuja kwa umbo la kibidamu baadae anatoweka, Ni mshakaji tunapiga story Sana, kila alhamisi ndio inakuwa siku yake yakuja kibindamu ,na ijumaa, nimeegundua kumbe chakula chao Ni mifupa pia,na mabaki ya vyakula walioacha binadamu baadhi
 
Si tulikubaliana kuna majini wazuri na wabaya..leo wewe unasema majini wote wabaya..utakua muislamu wa mchongo wewe.

#MaendeleoHayanaChama
Majini Kama ilivyo binadamu, Kuna wema na wabaya
 
Mimi nna Rafiki yangu wa kijini, ila yeye Ni wa ibada Sana, na hakai mwilini mwangu, ila huwa anakuja kwa umbo la kibidamu baadae anatoweka, Ni mshakaji tunapiga story Sana, kila alhamisi ndio inakuwa siku yake yakuja kibindamu ,na ijumaa, nimeegundua kumbe chakula chao Ni mifupa pia,na mabaki ya vyakula walioacha binadamu baadhi
Asalam alaykum
 
Si tulikubaliana kuna majini wazuri na wabaya..leo wewe unasema majini wote wabaya..utakua muislamu wa mchongo wewe.

#MaendeleoHayanaChama
Majini wazur na wabaya Kwa matendo Yao ni wao katika Maisha Yao, kuna wema na wabaya kama binadamu.

Lakini akishakuja kuchangamana na mwanadamu huyo tayar ni mbaya Kwa Hicho kitendo

Ngoja nikuongeze ufahamu zaidi Kwa mifano maana akili za watu WA Jf wanazijua wenyewe;

Binadamu katika Maisha Yao kuna wabaya na Wazuri lkn binadamu huyo huyo akienda kufanya mapenzi na mnyama hakika moja Kwa moja anakuwa ni mbaya kwasababu Kwa akili ya kawaida Hilo Jambo sio sawa
 
Mimi nna Rafiki yangu wa kijini, ila yeye Ni wa ibada Sana, na hakai mwilini mwangu, ila huwa anakuja kwa umbo la kibidamu baadae anatoweka, Ni mshakaji tunapiga story Sana, kila alhamisi ndio inakuwa siku yake yakuja kibindamu ,na ijumaa, nimeegundua kumbe chakula chao Ni mifupa pia,na mabaki ya vyakula walioacha binadamu baadhi
Huo mtihani ndugu yangu, lazima mtakuwa na mapatano Fulani

Majini hawashirikiani na wanadamu isipokuwa kuna makubaliano Kati Yao,na mara nyingi ni kumkana Mwenyezi Mungu na KUABUDIWA wao.

Jini hawezi kukufanyia kitu au kukusaidia Jambo Bila na yeye kupata faida.

Hakuna jema utalo pata kutoka Kwa hawa viumbe,Sana Sana utaangamia Tu!
 
Nimekaa tanga, tabora na lindi hivyo nafahamu kazi za mashehe kupunga pepo.
Mimi huwa mkweli katika Jambo la ukweli,sikatai kwamba hakuna masheikh ambao wanafanya hivyo,wapo na hao ni Wale wanao fanya uganga.

Lakini Dini hairuhusu ushirikina ,kwahiyo hao wahukumiwe Kwa matendo Yao na sio dini
 
Back
Top Bottom