Waislamu Mnafeli wapi?

Waislamu Mnafeli wapi?

Kumekuwa na dhana kwamba waislamu wanafuga majini kitu ambacho si kweli kabisa na hata Dini hairuhusu hivyo.

Mwenyezi Mungu anasema hakuumba majini na watu Ila isipokuwa wamwabudu Mola wao,ebu tuangalie Maandiko;

((Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.))
51:56

Kwahiyo Majini na wanadamu waliumbwa Kwa lengo moja Tu la kumwabudu Mola wao na sio vinginevyo.

Lakini bahati mbaya Sana kuna baadhi ya waislamu ambao hushirikiana na majini katika mambo Yao,na hii sio waislamu Tu hata baadhi ya watu ambao sio waislamu hufanya hivyo pia,iwe Kwa kupiga ramli,kufanya miujiza huko kwenye nyumba za ibada na kadhalika.

Ila mazungumzo yangu Leo hapa nazungumza na waislamu, kuna baadhi ambao huwa na haya maruhani/majini ambayo wenyewe huyaita majini Waziri kwakuwa Tu yanawasaidia katika mambo Yao. Naomba niwaambie kuwa hakuna majini mazuri ambayo yanakaa mwilini mwa mtu hata kidogo,hayo ni mabaya na machafu,jini ambaye ameumbwa ili kumwabudu Mola wake hawezi kuja kufanya makazi katika mwili WA mtu kwakuwa hayo ni makosa na amekiuka sababu ya kuumbwa kwake kabisa.

Wanao mwabudu Mola wao wapo kwenye makazi Yao ya kijini na wanaendesha Maisha Yao huku wanamwabudu Mola wao,kwahiyo acheni kuwa watumwa WA hayo majini,kwani hakika mwisho wenu utakuwa sio mzuri.

Ebu tuangalie maongezi haya ya majini kama yalivyoelezwa katika Qur'an ;

((Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.))
72:6


Haya ni maongezi ya Majini baada ya kusikia Qur'an na kumwamini Mola wao,ndio wanahadithia kuwa kuna wanadamu wanaume ambao walikuwa wanatafuta hifadhi toka Kwa majini lakini matokeo yake wakazidishiwa madhambi. Na huo ndio ukweli kuna watu ambao wanaamini majini kuwa ndio watawalinda hapa duniani,na huwa hawafanyi Jambo lolote mpaka washaurieni na majini wao,hakika hiyo ni kufuru kubwa kumwamini kiumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa ndio anakuwezesha kufanikiwa Kwa mambo hapa duniani.

Na mwisho wa siku shetani/ hayo majini machafu ambayo yameacha kusudio la kuumbwa kwao na kuja kushirikiana na wanadamu,mwisho wa siku yatawakana na kuwaambia ukweli, tuangalie Aya ifuatayo;

(Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu).
14:22


Hakika kuna Aya nyingi Sana juu ya majini kuwapotosha wanadamu na kuwaingiza Motoni,kubwa ni kujua kwamba hakuna majini ambao wanatakiwa kushirikiana na binadamu kwani wao Wana Maisha Yao na wanadamu tuna yetu,ushirikiano wowote baina yetu ni upotovu na mwisho wake ni jehenamu.

Mambo mengi na Mda ni mchache!

Ni hayo Tu!
Majini ni viumbe vyake Mnyaazi.

Na ndiyo viumbe vya kwanza kabisa kusilimu kuwa Waislamu ndo wakafuata Binadamu. Walisema hii ndiyo dini inayomwabudu Mola wao.

Wewe unaleta maandiko gani kutaka kutupotosha?
 
Ah Mzee wa freemasons karibu sana
Hujajibu swali nililouliza na ulilojibu sijauliza.

Hujathibitisha huo moto upo.

Mimi siwezi kuwa freemason. Kuwa freemason ni lazima uamini katika aina fulani ya Mungu. Mimi siamini Mungu yeyote.

Wewe unayeamini moto, presumably na Mungu, uko karibu na Freemasons kuliko mimi nisiyeamini kuwepo kwa moto wala Mungu.

Chukua hili kama somo la leo.
 
Hujajibu swali nililouliza na nililouliza hujajibu.

Hujathibitisha huo moto upo.

Mimi siwezi kuwa freemason. Kuwa freemason ni lazima uamini katika aina fulani ya Mungu. Mimi siamini Mungu yeyote.

Wewe unayeamini moto, presumably na Mungu, uko karibu na Freemasons kuliko mimi nisiyeamini kuwepo kwa moto wala Mungu.

Chukua hili kama somo la leo.
Sawa mkuu

Maoni yako yatazingatiwa!

Karibu sana
 
Mimi huwa mkweli katika Jambo la ukweli,sikatai kwamba hakuna masheikh ambao wanafanya hivyo,wapo na hao ni Wale wanao fanya uganga.

Lakini Dini hairuhusu ushirikina ,kwahiyo hao wahukumiwe Kwa matendo Yao na sio dini
Mwislam asiye mnafiki? Theres hope for mankind
 
Sawa mkuu

Maoni yako yatazingatiwa!

Karibu sana
Haya si maoni, hizi ni facts.

Huwezi kuthibitisha huo moto upo, kwa sababu haupo.

Siwezi kuwa Freemason, kwa sababu siamini uwepo wa Mungu.

Bisha.
 
Back
Top Bottom