Waislamu Mnafeli wapi?

Kwanza kabisa, mfano wako wa gari si sahihi.

Gari halina uhai, halina maamuzi.

Sasa unalifananishaje gari ambalo halina uhai wala maamuzi na mtu mwenye uhai na maamuzi?

Pili, kunifananisha mimi ambaye ujuzi wangu una mipaka, na huyo Mungu wako ujuzi wake hauna mipaka, ni makosa.

Kama ingekuwa hesabu, umefanya uwiano wa cross multiplication kati ya namba na infinity.

Hapo lazima hesabu zako zilete mauzauza yatakayoharibu number theory.

Utapata jibu kwamba kila namba ni sawa na kila namba nyingine, na hesabu hazina maana.

Unapojaribu kufanya analogy, linganisha vinavyolingana.

Mpaka sasa.

1. Hujathibitusha Mungu yupo.
2. Hujatatua problemnof evil.
3. Hujaeleza kwa nini Mungu hatupi uchaguzi wa kuamua tuishi au tusiishi.
4. Hujathibitisha maisha yajayo yapo.
5.Hujajenga hoja yoyote iliyo logically coherent ya kutetea uwepo wa Mungu.
 
Una matatizo ya kimsingi ya kufikiri kidhahania.

Nakuuliza, je, Mungu alishindwa kuumba dunia ambayo makosa, ubaya, uasi, dhambi etc havijulikani na haviwezi kutokea?

Unanijibu kwamba hakushindwa, ila aliumba ulimwengu halafu Adamu na Hawa wakafanya makosa.

Huelewi hata swali langu.

Unajibu kwa kukariri.

Nakuuliza hivi, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao Adam na Hawa hawawezi kufanya makosa? Ulimwengu usiowezekana kufanyika makosa. Makosa hayapo, hayajulikani. Mabaya hayajulikani kabisa. Hayapo?

Unanijibu, aliweza, ila Adam na Hawa walifanya makosa.

Huelewi hata swali ni nini. Hivyo huwezi kulijibu.

Nakuuliza kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao Adam na Hawa hawawezi kufanya makosa?

Unanijibu aliweza, ila Adam na Hawa walifanya makosa.

Una matatizo ya kufikiri kidhahania. Huwezi kufikiri nje ya kukariri kikichoandikwa kwenye vitabu hata kwenye swali rahisi hili.
 
Unajibu hoja kwa hofu za maandiko ya kidini.Je kwa nini unadhani Atheist hawako sahihi kuamini Mungu hayupo? Unatumia kigezo gani kusema Atheist hawako sahihi kusema Mungu hayupo? Au ni hofu zako na jinsi ulivyofundishwa na Dini yako? Kwa nini unadhani mawazo na maoni yako ya kwamba "Mungu yupo" ndio sahihi tu na ya wengine si sahihi??????...
 

Sayansi imeelezea kuwa dunia ina spin/rotate lakini je sayansi imeelezea nini kinachokufanya ijizungushe tangu kuweko kwake?

Uwepo wa sayari na mpangalio wake na kuelea kwake kutokana na uwepo wa gravitational force,je hiyo system ilijitokeza Tu yenyewe? Hivi mnayafikiria vizur haya mambo?

Kwa mfano kujaa na kupungua Kwa maji ya bahari ( low tide range & high tide range) kutokana na kuspin Kwa dunia na gravitational force toka kwenye jua na Mwezi,,,,,je how does this happen? Unataka kusema haya mambo yamejitikeza Tu Kwa bahati? Kama Kwa bahati basi hata kuacha kutokea inawezekanq pia. Kama ni hivyo kwanini tangu uwepo wa ulimwengu kumekuwa na nidhamu hii Bila longo longo lolote?
Kwasababu kuna Mungu muweza ya yote ambaye ndio designer WA hili
 
Nilichokieleza ni kuonyesha kuwa hayo unayoyasema Kwa Mungu yanawezekana,Kwa maana mwanzoni aliwaweka hao wanadamu wawili Katika sehemu ambayo hakukuwa na dhambi wala mabaya

Na

Baadae akaamua kuwaweka katika ulimwengu huu wenye mabaya na mazuri Kwa kusudio maalumu, hii ndio hoja kubwa.
 
Nasema hivyo kwasababu moja,atheist wamesimamia katika msingi mkuu WA sayansi.

Lakini sayansi haijatoa solution ya kila kitu,kuna mambo ambayo sayansi haina majibu au inafikia ukomo,kama hakuna majibu basi hoja ya atheist kuwa hakuna mungu inakuwa haina mashiko kabisa.

Mfano kama sayari na nyota vilijitokeza Tu zenyewe,then kwanini kuna gravitational force ambayo inazifanya zikae na kulea katika namna ambayo ina mpangilio mzuri?

Kama vilijitokeza Tu Kwa bahati kwanini zinatofautiana Kwa sifa mbali mbali,kwanini vyote visingekuwa na sifa moja na Tabia moja.

Kwa mfano imekuwaje baadhi ya sayari kama dunia kusapoti Maisha ya viumbe na nyingine hazina,kama vilitokea Kwa bahati either vyote vingesapoti Uhai WA viumbe au vyote visinge sapoti ya viumbe.

Mpangilio huo sayansi imefeli na automatically hoja za atheist zinakuwa hazina mashiko.

Na Mungu ndio designer WA hayo yote.

Tangu nianze mjadala huu sijaweka hata Aya moja ya Kitabu cha Dini,kwakuwa najua naongea na watu ambao hawamuamini Mungu.

Sasa kutokana na swali lako, je kwanini nadhani naamini nipo sahihi,naleta hoja ya Maandiko juu ya uumbaji,ambapo jambo hili lilisemwa na Qur'an toka Karne ya 14 kabla ya modern sayansi kuanza utafiti wao,lakini baadae walikuja kuprove kilichosemwa na Maandiko ni sahihi


Qur'an inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu aliumba ardhi Kwa siku mbili:

"Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote."
41:9

Kisha Mwenyezi Mungu akailekea mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaiita pamoja na ardhi zikaambatana pamoja.

"Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu."
41:11

"Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua."
41:12

Mpaka hapo tunaona kwamba uumbaji WA mbingu na ardhi umefanyika nyakati nne au siku nne.

Qur'an inasema halafu mbingu ambayo ni Moshi ili ambatanishwa na ardhi Kwa pamoja zikawa zimeshikamana,tuangalie Maandiko:


"Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?"
21:30

Kwahiyo mpaka hapa tunaona kwamba,uumbaji WA mbingu na ardhi Kwa mujibu wa Qur'an,ulikuwa kama ifuatavyo;

Mwenyezi Mungu aliumba ardhi kisha akaichukua mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaziambatanisha pamoja zikawa zimeshikana kisha baadae akaziachanisha na kuumbwa Kwa mbingu Saba na viliomo baina ya mbingu na ardhi.

Ukija katika Sayansi inadhibitisha utaratibu ule ule ulio elezwa na Qur'an

Sayansi inasema katika uumbaji, kulikuwa na gaseous mass with fine particles ambazo Kwa kiarabu (dukan) ambao INA maanisha Moshi,ambapo Moshi unaundwa na gaseous substratum na fine particles ambazo zinakuwa katika Hali ya ugumu na Hali ya kimiminika katika high temperature or low temperature.

Halafu baadae zikaachana baada ya kutokea mlipuko mkubwa,ambao ulipelekea kurushwa Kwa materials mbali mbali angani na kuundwa Kwa mbingu na vitu vingine kama sayari na nyota na bodies nyingine mbali mbali,rejea kwenye Bing Bang Theory.
Na kwakuongezea Tu ndio maana ukiangalia sayar kama Jupiter utakuta kuna gaseous kama helium na hydrogen, nyota kama jua ni gaseous tupu,hizo Kwa uchache Tu.

Na vile vile Qur'an imeeleza dunia katika uwingi na hivyo ikamaanisha huenda kukawa na uwezekano WA kuwepo dunia nyingine kama yetu ingawa Sayansi bado haijagundua Hilo swala,ingawa wanasema uwezekano huo upo katika galaxy nyingine ambayo IPO nje ya galaxy yetu,waliosoma au ambao wanapenda kusoma mambo ya anga nadhani wanajua nikisema Milk way galaxy namaanisha nini?

Kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yameelezwa katika Qur'an ambapo bado. Sayansi haija yagundua huenda yakaja kugundulika na vizazi vijavyo huko.


Na hapa tuangalie pia Maandiko yanasemaje kuhusu Human production


Kwanza nianze na mambo machache au utaratibu ambao unahusika moja Kwa moja na uzazi wa binadamu.

Mwanzo ni kurutubishwa Kwa Yai kwenye sehemu inaitwa fallopian tube,kinachotumika kurutubisha ni mbegu ya kiume (sperm) au kitalaam spermatozoon,kwahiyo kinachotakiwa ni tone dogo la manii ambalo Lina mbegu kama million 10. Na maji haya au tone hili la manii hutengenezwa na testicles (makende) na kuhifadhiwa hapo,halafu kuna glands ambazo zipo karibu na maeneo hayo ambazo huongeza au kutengeneza maji maji katika sperm.
Kwahiyo upandikizaji wa Yai ambalo tayar limepevuka hufanyika katika system ya uzazi ya mwanamke,na kupitia katika follopiana tube na kuelekea katika uterus na huko hujishikiza na hatimaye placenta inatengenezwa au inajitengeneza, na Kwa mfano kama upandikizaji wa Yai ukifanyika katika follopian tube badala ya uterus basi huo ujauzito utaharibika.

Na baada ya embryo kuweza kuonekana na jicho la kawaida basi huonekana kama muunganiko WA kanyama kadogo ambako si rahisi kujua kama binadamu,na inaendelea kukua katika hatua mbali mbali ambazo hujulikana Leo,na kuwa umbile la mifupa,misuli (muscles), mifumo ya ufahamu na kadhalika.

Sasa tuje katika mkabala au maelezo ya qura'n :

Qur'an katika mfumo mzima wa uzazi inazungumzia katika maeneo yafuatayo;

1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa
2) kuna maji maji ya uzazi
3) kuna Utungwaji WA Yai lililo pevuka
4) mabadiliko ya embryo

1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa

Hapa quran inazungumzia swala hili mara Kumi na moja,nitaandika baadhi ya Aya Tu:

((Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.))
16:4


((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?))
75:37

((Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.))
23:13


2) Maji maji ya Uzazi
Qur'an inazungumzia maji maji ya Uzazi ambayo inafurahisha kuyafanyia uchambuzi hapa;


((Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.))
76:2

((Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,))
86:6

Sasa ebu tuangalie haya maji ambayo huambatana na sperm Yana mchanganyiko upi?

a) secretion of male genital gland contains spermatozoons
b) seminal vesicles - hizi organs zina hifadhi spermatozoons zipo karibu na prostate gland,zinatoa maji maji yake ingawa hazina fertilizing agent
c) prostate gland - maji maji yake inaipa sperm creamy texture and characteristic odour
d) glands annexed to the urinary tract

Na hizi ni Aina za maji maji ambazo Qur'an imezigusia na kudhibitishwa na modern science.

3) Utungwaji WA Yai lililo pevuka
Baada ya Yai kuwa fertilized katika fallopian tube inakwenda kwenye uterus na hapo inasemwa implantation of the egg.
Na Qur'an inasema hivi katika tukio Hilo;

((Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa))
22:5

Na Ile Hali ya Yai kuwa katika uterus na kujishikiza katika ukuta mwembamba Kwa AJILI ya kukua, na huo ndio ugunduzi wa modern time.
Na Hali hii pia imeelezwa katika Qur'an tangu zamani huko;

((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14


((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.))
75:37-38

4) Mabadiliko ya Embryo ndani ya Uterus;
Qur'an imezungumzia mabadiliko ya kiumbe ndani ya uterus kama ambavyo modern science imedhibitisha hivyo, na yanashahabiana Sawa Sawa.

((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14

Modern sayansi inasema Kwanza kunakuwa na umbile kama big g/nyama iliyotafunwa ( chewing gum/chewing fresh) ,katika udogo wake kabisa ambao unaweza kuonekana na jicho la kawaida inakuwa kama nyama iliyotafunwa,halafu umbile la mifupa hujitokeza ( mesenchyma) ,halafu mifupa iliyoundwa hufunikwa na misuli ( muscle), halafu baadae organ za fahamu na kufuatiwa na jinsia za kiumbe.

((Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.))
32:9

((Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike

Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa))
53:45-46

Huyo ndio Mwenyezi Mungu,,hakika tukiacha ushabiki wa Imani zatu na kuziweka pembeni,unaona kabisa elimu hii ni ufunuo wa Mwenyezi Mungu Kwa mja wake Muhammad ( s.a.w).

Na kumbuka katika Karne Ile hakukuwa na maendeleo ya kufahamu nini kinaendelea ndani ya tumbo la mwanadamu kuhusiana na uzazi na kubwa zaidi kila hatua ambayo Qur'an imeeleza hakika haikutofautiana na tafiti zilizo fanywa na wavumbuzi wa Karne ya 20.

Na Mwenyezi Mungu alimchagua Mtume ambaye hajui kusoma wala kuandika ili adhibitishe maneno yake kuwa Ni ufunuo usio na Shaka ndani yake na unatoka Kwa Yule ambaye ni mjuzi WA mambo yote,yawe na Siri na yasiyo ya Siri na mambo ya ghaibu
 
Mr kiranga
. Kwaiyo ukiambiwa uthibitishe kuwa hakuna Mungu anaendesha aya mambo yote yanayoendelea unauhakika kabisa utatoa point zilizoshiba kwa mujibu wa akili yako au umeamini ivyo tu na wewe ndo imani yako iyo?
kwasababu kuthibitisha mambo ya imani kwa akili zetu izi zakawaida ni jambo ambalo sio la mchezo mchezo ndo maana kuna mambo mengine tunaamua kuyaamini tu bila kuyajudge sana tunachukulia ni katika mtihani unapaswa uamini ili ubaki kwenye line kwa imani yakufaulu mitihani

Tunaona mifumo mbali mbali inaendeshwa kimitihani mitihani tu hadi unafanikiwa mtu lazima uwe umepita mitihani mbali mbali kuna vitu unakutana navyo kwenye mitihani ukiambiwa uprove huwezi yani haimake sense ila unajibu ivo ivo ili ufaulu mfano mzuri wewe sahiz uambiwe uthibitishe kuwa binadamu wamwanzo walitokana na nyani yani utazunguka sana huwezi kuthibitisha na ulijibu kwenye mitihani yako mpaka umefikia hapo

Kwaiyo inawezekana kabisa yupo anaeongoza izi harakati za kidunia na tupo kwenye mtihani "wabongo wana msemo wao kuwa bora uamini yupo ukienda usimkute kuliko kuamini hayupo alafu ukaenda umkute"

Ila jambo zuri nikuamini tu yupo moja kwa moja achana na ayo mambo ya kuwa smart na kiuhalisia hakuna alikuja na hoja za maana kuthibitisha mambo yametokea tu yenyewe toka miaka iyo sio wanasayansi wala wanafalsafa n.k kuna point wanafika wanajikanyaga tu kama yupo unayemjua tuletee apa mwisho wa siku wamebaki wakiamini tu na hawawezi kuthibitisha chochote ni sawa na wewe Kiranga ukitaka watu wathibitishe mambo kweny imani zao kiufupi hutowaelewa acha watu waamini

Watu wamekufa kwa dhurma kwakuonewa bila haki yoyote kutendeka kuna watu hawajatendewa haki kwenye haya maisha na wamekufa katika hali iyo basi lazima kuna muendelezo wa aya maisha baada ya kufa na haki lazima itendeke~
Ni katika maneno ya mwanafalsafa mmoja kama sio Emmanuel Kant.
 
Nimekueleza kwamba, ukisisitiza sana kwamba hivi vyote vyenye complexity na order ni lazima viwe na muumbaji, na muumbaji ni Mungu, unaweza kujiona unatetea uwepo wa Mungu, lakini, hapo hapo umejiwekea swali la Mungu naye katokeaje?

You can't eat your cake, finish it, and still have it.

Umeielewa hiyo hoja?

Ni hivi.

1. Ama vitu vyote complex na vyenye order vinahitaji muumbaji, na kwa kanuni hii hii Mungu muweza yote hayupo, kwa sababu naye ni complex na ana order na atahitaji muumbaji, na akihitaji muumbaji anakuwa si Mungu muweza yote tena.

2. Ama vitu comolex na vyenye order havihitaji muumbaji, na kwa kanuni hii Mungu hahitaji kuwepo ili kuelezea ulimwengu huu complex.

Either way, 1 Mungu hayupo au 2 Mungu hahitajiki kuelezea ulimwengu huu.

Hizi point unazielewa au unazisoma tu na kurudia ulichokaririshwa kutoka vitabu vya dini?

Unaweza kuzipinga na kuzipangua hoja hizi kimantiki?

Naona hujazielewa na wala hujazipinga.

Nachelea kujadiliana na mtu ambaye hanielewi.

That is a waste of time to me.
 
Hujaelewa swali.

Je, Mungu aliweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani kufanyika?

Ukitoa mfano wa Adam al8umbwa katika ulimwengu ambao haukuwa nandhambi wala mabaya, baadaye wakafanya dhambi, unanieleza kwamba hujaelewa swali. Na una tatizo la kusomankwa ufahamu.

Mimi naukiza kuhusu ulimwengu ambao dhambi haiwezi kufanyika. Wewe unanijibu kwa mfano wa ulimwengu ambao dhambi imefanyika.

Hujaeleea swali.

Hujaelewa swali kabisa.

Naanza kupata shaka kama una hata uwezo wa kunielewa.
 
Kwa framework ya logic, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote, aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya, anaweza kuthibitishwa kwamba hayupo.

Anaweza kuthibitishwa hayupo kama vile unavyoweza kuthibitisha kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.

Anaweza kuthibitishwa hayupo kama vile unavyoweza kuthibitisha kwamba mtoto mchanga wa miezi sita leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo.

Anaweza kuthibitishwa hayupi kama vule inavyoweza kuthibitishwa kwamba hakuna pembetatu ambayo pia ni duara hapohapi katuka Euclidean plane geometry.

Na zaidi, kimantiki, kati ya wanaosema kitu kipo na wanaopinga, wenye wajibu wa kuthibitisha (the burden of proof) ni wale wanaosema kitu kipo.

Ndiyo maana polisi wakija kwako na kukutuhumu wewe kwamba umeficha madawa ya kulevya nyumbani kwako, wao ndio wanaotakiwa wpige search nyumba, wayapate hayo madawa, na kuyaweka kama ushahidi. Si kazi yako wewe unayesema madawa hayapo ku prove kwamba madawa hayapo.

But I doubt many appreciate these facts.

Mimi nimethibitisha, through the problem of evil, in a logical framework, kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwapo na ulimwengu huu unaoruhusu mabaya uwepo. Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu huu haupo, ama ulimwengu huu upo na Mungu huyo hayupo.

Ulimwengu huu upo, hivyo, Mungu huyo hayupi.

Wanaosema Mungu yupo hawajathibitisha kwa njia yoyote kwamba yupo, wanakwenda kwa imani tupu.

Tatizo najadiliana na watu ambao hata nikielezea "the problem of evil" wengi hawaelewi undani wake.
 

Kwanini unaamini kila kitu chenye complexity lazima kiwe na mwanzo wake?
Je huko si kukariri pia?

Na ukishaanza kuamini au kukariri hivyo ujue hakutakuwa na mwisho wa chanzo cha kitu.


Chanzo ni kimoja Tu Mungu
 
Kama ambavyo unaona it's a wastage of time kuendelea kujadiliana kwakuwa unadhani sikuelewi

Nami pia naona nami hunielewi vile vile

Let's have a time out!
 
Kwanini unaamini kila kitu chenye complex lazima kiwe na mwanzo wake?
Je huko si kukariri pia?

Na ukishaanza kuamini au kukariri hivyo ujue hakutakuwa na mwisho wa chanzo cha kitu.


Chanzo ni kimoja Tu Mungu
Wapi nimesema naamini kila kilicho complex lazima kiwe na mwanzo wake?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Naona najadiliana na mtu ambaye hajui kusoma kwa ufahamu.
 
Kama ambavyo unaona it's a wastage of time kuendelea kujadiliana kwakuwa unadhani sikuelewi

Nami pia naona nami hunielewi vile vile

Let's have a time out!
Nitakuelewa vipi wakati hufuati logic?

Unaleta arguments zinazoonesha Mungu muweza yote hawezi kuwepo, huku ukifikiri hizo ni arguments za kutetea uwepo wa Mungu.

Tutaelewana vipi?
 
Mithali 19:21 Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Hivyo it's true kwamba
Binadamu hawezi kufanya kitu ambacho ni nje ya mipango ya Mungu
Sasa kama binadamu hawezi kufanya kitu chochote kilicho nje ya mipango wa Mungu, kwa nini binadamu anahukumiwa kwa kufanya dhambi?

Yani ikiwa binadamu kufanya dhambi ni mpango wa Mungu (kwa sababu binadamu hawezi kufanya kitu ambacho ni nje ya mipango ya Mungu), sasa inakuwaje Mungu apange binadamu afanye dhambi, halafu amhukumu tena huyo binadamu kwa kufanya dhambi?
 
Zaburi 53:1

Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema.

WAPUMBAVU WAZIDI KUONGEZEKA NA WANA JAZBA KWELI KWELI.
 
Zaburi 53:1

Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema.

WAPUMBAVU WAZIDI KUONGEZEKA NA WANA JAZBA KWELI KWELI.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Umekariri Zaburi.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Umekariri Zaburi.

Thibitisha Mungu yupo.


AKILI ZA WAPUMBAVU ZIMEGOMA KUTAMBUA UWEPO WA MUNGU.
 
2 Wakorintho 4:18

tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…