Unajibu hoja kwa hofu za maandiko ya kidini.Je kwa nini unadhani Atheist hawako sahihi kuamini Mungu hayupo? Unatumia kigezo gani kusema Atheist hawako sahihi kusema Mungu hayupo? Au ni hofu zako na jinsi ulivyofundishwa na Dini yako? Kwa nini unadhani mawazo na maoni yako ya kwamba "Mungu yupo" ndio sahihi tu na ya wengine si sahihi??????...
Nasema hivyo kwasababu moja,atheist wamesimamia katika msingi mkuu WA sayansi.
Lakini sayansi haijatoa solution ya kila kitu,kuna mambo ambayo sayansi haina majibu au inafikia ukomo,kama hakuna majibu basi hoja ya atheist kuwa hakuna mungu inakuwa haina mashiko kabisa.
Mfano kama sayari na nyota vilijitokeza Tu zenyewe,then kwanini kuna gravitational force ambayo inazifanya zikae na kulea katika namna ambayo ina mpangilio mzuri?
Kama vilijitokeza Tu Kwa bahati kwanini zinatofautiana Kwa sifa mbali mbali,kwanini vyote visingekuwa na sifa moja na Tabia moja.
Kwa mfano imekuwaje baadhi ya sayari kama dunia kusapoti Maisha ya viumbe na nyingine hazina,kama vilitokea Kwa bahati either vyote vingesapoti Uhai WA viumbe au vyote visinge sapoti ya viumbe.
Mpangilio huo sayansi imefeli na automatically hoja za atheist zinakuwa hazina mashiko.
Na Mungu ndio designer WA hayo yote.
Tangu nianze mjadala huu sijaweka hata Aya moja ya Kitabu cha Dini,kwakuwa najua naongea na watu ambao hawamuamini Mungu.
Sasa kutokana na swali lako, je kwanini nadhani naamini nipo sahihi,naleta hoja ya Maandiko juu ya uumbaji,ambapo jambo hili lilisemwa na Qur'an toka Karne ya 14 kabla ya modern sayansi kuanza utafiti wao,lakini baadae walikuja kuprove kilichosemwa na Maandiko ni sahihi
Qur'an inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu aliumba ardhi Kwa siku mbili:
"Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote."
41:9
Kisha Mwenyezi Mungu akailekea mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaiita pamoja na ardhi zikaambatana pamoja.
"Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu."
41:11
"Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua."
41:12
Mpaka hapo tunaona kwamba uumbaji WA mbingu na ardhi umefanyika nyakati nne au siku nne.
Qur'an inasema halafu mbingu ambayo ni Moshi ili ambatanishwa na ardhi Kwa pamoja zikawa zimeshikamana,tuangalie Maandiko:
"Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?"
21:30
Kwahiyo mpaka hapa tunaona kwamba,uumbaji WA mbingu na ardhi Kwa mujibu wa Qur'an,ulikuwa kama ifuatavyo;
Mwenyezi Mungu aliumba ardhi kisha akaichukua mbingu ambayo ilikuwa Moshi akaziambatanisha pamoja zikawa zimeshikana kisha baadae akaziachanisha na kuumbwa Kwa mbingu Saba na viliomo baina ya mbingu na ardhi.
Ukija katika Sayansi inadhibitisha utaratibu ule ule ulio elezwa na Qur'an
Sayansi inasema katika uumbaji, kulikuwa na gaseous mass with fine particles ambazo Kwa kiarabu (dukan) ambao INA maanisha Moshi,ambapo Moshi unaundwa na gaseous substratum na fine particles ambazo zinakuwa katika Hali ya ugumu na Hali ya kimiminika katika high temperature or low temperature.
Halafu baadae zikaachana baada ya kutokea mlipuko mkubwa,ambao ulipelekea kurushwa Kwa materials mbali mbali angani na kuundwa Kwa mbingu na vitu vingine kama sayari na nyota na bodies nyingine mbali mbali,rejea kwenye Bing Bang Theory.
Na kwakuongezea Tu ndio maana ukiangalia sayar kama Jupiter utakuta kuna gaseous kama helium na hydrogen, nyota kama jua ni gaseous tupu,hizo Kwa uchache Tu.
Na vile vile Qur'an imeeleza dunia katika uwingi na hivyo ikamaanisha huenda kukawa na uwezekano WA kuwepo dunia nyingine kama yetu ingawa Sayansi bado haijagundua Hilo swala,ingawa wanasema uwezekano huo upo katika galaxy nyingine ambayo IPO nje ya galaxy yetu,waliosoma au ambao wanapenda kusoma mambo ya anga nadhani wanajua nikisema Milk way galaxy namaanisha nini?
Kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yameelezwa katika Qur'an ambapo bado. Sayansi haija yagundua huenda yakaja kugundulika na vizazi vijavyo huko.
Na hapa tuangalie pia Maandiko yanasemaje kuhusu Human production
Kwanza nianze na mambo machache au utaratibu ambao unahusika moja Kwa moja na uzazi wa binadamu.
Mwanzo ni kurutubishwa Kwa Yai kwenye sehemu inaitwa fallopian tube,kinachotumika kurutubisha ni mbegu ya kiume (sperm) au kitalaam spermatozoon,kwahiyo kinachotakiwa ni tone dogo la manii ambalo Lina mbegu kama million 10. Na maji haya au tone hili la manii hutengenezwa na testicles (makende) na kuhifadhiwa hapo,halafu kuna glands ambazo zipo karibu na maeneo hayo ambazo huongeza au kutengeneza maji maji katika sperm.
Kwahiyo upandikizaji wa Yai ambalo tayar limepevuka hufanyika katika system ya uzazi ya mwanamke,na kupitia katika follopiana tube na kuelekea katika uterus na huko hujishikiza na hatimaye placenta inatengenezwa au inajitengeneza, na Kwa mfano kama upandikizaji wa Yai ukifanyika katika follopian tube badala ya uterus basi huo ujauzito utaharibika.
Na baada ya embryo kuweza kuonekana na jicho la kawaida basi huonekana kama muunganiko WA kanyama kadogo ambako si rahisi kujua kama binadamu,na inaendelea kukua katika hatua mbali mbali ambazo hujulikana Leo,na kuwa umbile la mifupa,misuli (muscles), mifumo ya ufahamu na kadhalika.
Sasa tuje katika mkabala au maelezo ya qura'n :
Qur'an katika mfumo mzima wa uzazi inazungumzia katika maeneo yafuatayo;
1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa
2) kuna maji maji ya uzazi
3) kuna Utungwaji WA Yai lililo pevuka
4) mabadiliko ya embryo
1) Utungwaji WA mimba unafanywa na kiasi kidogo cha manii/shahawa
Hapa quran inazungumzia swala hili mara Kumi na moja,nitaandika baadhi ya Aya Tu:
((Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.))
16:4
((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?))
75:37
((Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.))
23:13
2) Maji maji ya Uzazi
Qur'an inazungumzia maji maji ya Uzazi ambayo inafurahisha kuyafanyia uchambuzi hapa;
((Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.))
76:2
((Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,))
86:6
Sasa ebu tuangalie haya maji ambayo huambatana na sperm Yana mchanganyiko upi?
a) secretion of male genital gland contains spermatozoons
b) seminal vesicles - hizi organs zina hifadhi spermatozoons zipo karibu na prostate gland,zinatoa maji maji yake ingawa hazina fertilizing agent
c) prostate gland - maji maji yake inaipa sperm creamy texture and characteristic odour
d) glands annexed to the urinary tract
Na hizi ni Aina za maji maji ambazo Qur'an imezigusia na kudhibitishwa na modern science.
3) Utungwaji WA Yai lililo pevuka
Baada ya Yai kuwa fertilized katika fallopian tube inakwenda kwenye uterus na hapo inasemwa implantation of the egg.
Na Qur'an inasema hivi katika tukio Hilo;
((Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa))
22:5
Na Ile Hali ya Yai kuwa katika uterus na kujishikiza katika ukuta mwembamba Kwa AJILI ya kukua, na huo ndio ugunduzi wa modern time.
Na Hali hii pia imeelezwa katika Qur'an tangu zamani huko;
((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14
((Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.))
75:37-38
4) Mabadiliko ya Embryo ndani ya Uterus;
Qur'an imezungumzia mabadiliko ya kiumbe ndani ya uterus kama ambavyo modern science imedhibitisha hivyo, na yanashahabiana Sawa Sawa.
((Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.))
23:14
Modern sayansi inasema Kwanza kunakuwa na umbile kama big g/nyama iliyotafunwa ( chewing gum/chewing fresh) ,katika udogo wake kabisa ambao unaweza kuonekana na jicho la kawaida inakuwa kama nyama iliyotafunwa,halafu umbile la mifupa hujitokeza ( mesenchyma) ,halafu mifupa iliyoundwa hufunikwa na misuli ( muscle), halafu baadae organ za fahamu na kufuatiwa na jinsia za kiumbe.
((Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.))
32:9
((Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa))
53:45-46
Huyo ndio Mwenyezi Mungu,,hakika tukiacha ushabiki wa Imani zatu na kuziweka pembeni,unaona kabisa elimu hii ni ufunuo wa Mwenyezi Mungu Kwa mja wake Muhammad ( s.a.w).
Na kumbuka katika Karne Ile hakukuwa na maendeleo ya kufahamu nini kinaendelea ndani ya tumbo la mwanadamu kuhusiana na uzazi na kubwa zaidi kila hatua ambayo Qur'an imeeleza hakika haikutofautiana na tafiti zilizo fanywa na wavumbuzi wa Karne ya 20.
Na Mwenyezi Mungu alimchagua Mtume ambaye hajui kusoma wala kuandika ili adhibitishe maneno yake kuwa Ni ufunuo usio na Shaka ndani yake na unatoka Kwa Yule ambaye ni mjuzi WA mambo yote,yawe na Siri na yasiyo ya Siri na mambo ya ghaibu