Waislamu Mnafeli wapi?

Ni Kama dhambi zingine tu,ukute anayeshitikiana na jinni hanywi pombe,hazini,hachezi kamari...Ila hakuna uchawi usiohusisha jinni,wengine wanaita mizimu,Ila ndiyo jinni haohao
Exactly Mkuu, uchawi ni Sanaa ya kuwasiliana na majini.

Kafara ni Funguo ya kuwasiliana na majini.

Kutokana na jamii na jamii hao majini wana majina tofauti, Mizimu, demons, devils, Aliens, ghost etc.
 
Na jamaa anaweza kusema kuwa amemtaja Bakhesa kama tajiri sio tajiri aliyetajirika kea makini.
Angalia hiyo sentensi yake,yawezavunjwa vunjwa
Hajathibitisha huko motoni kupo.
 
Nioneshe hao waloelimika hapa?
Nakujibu Tu kwakuwa nakuheshimu

Kwakuwa unaona watu bado wanaonyesha kupinga haina maana kwamba hawajifunzi,kinachobaki hapa ni ushabiki wa Dini Tu.

Na sitarajii wote wataelewa Ila hao wachache watao elewa inatosha,kwani Nabii Nuhu aliwalingania watu Kwa miaka kibao lakini walio mkubali ni 80 Tu. Kwahiyo kwenye kazi ya da'wa kazi yako ni kufikisha Tu na Allah ndio muwezeshaji

Tunaambiwa tufikishe walau Aya moja Tu kuwafahamisha watu ujumbe wa Mwenyezi Mungu,watu wengine huwezi kutana nao misikitini au makanisani Bali tunakutana humu na kuelimishana.

Nashangaa tatizo liko wapi.

Wasio waislamu karibia wote kama sio baadhi Yao wanaamini Uislamu ni Dini ya majini,sasa Mimi nimeonyesha Uislamu wenyewe hauko hivyo Bali watu wake ndio wako hivyo,je nimefanya vibaya kusema haki?

Uongo ukiachwa uendelee'' mwisho wa siku unakubalika kuwa kweli,ni juu yetu kusema hii kweli na hii ni Uongo.

Shukrani.
 
Hao Masharifu mala kadhaa tunaona ndio waalimu wazuri wa dini.

Akizaliwa mtoto Sharifu anatembezwa sehemu mbali mbali kutoa mihadhara ya dini na kuombea waislamu wenye madhaifu mbali mbali.

Wewe bado hujaufamu Uislamu kwa usahihi.

ni wewe ambae hujaufahamu, hao watoto wanaitwa Masharifu hutumiwa na wajanja wajanja kwa ajili ya kupigia pesa tu.
 
hakuna cha kushirkiana na majini sema watu wanashobokea majini na majinamiz
af yenyew ayanag time ndoman tukijichanganya yanatubetua
 
Kwa hivyo hoja nzima haitufikishi popote, na haikufikiriwa kwa kina.
Inategemea kiwango cha uelewa wa mtu.
Nadharia yangu ni kuwa.

"Kitu chochote kinakufikisha mahala pengine"

Hivyo kujifunza hoja yoyote kunafaa.

Na sio kukanusha kanusha kitu chochote.
 
Hata mimi sioni kosa lako hapo Sheikh labda ungekuwa umepotosha kwenye mada na kuweka vitu vya uwongo hapo ingekuwa kweli hata mimi kuna rafiki yangu mkiristo ambaye nimesoma nae miaka mingi alikuwa anaamini muislamu ukishika dini lazima uwe na majibu na Qu'ran ina majini baada miaka mingi tulikutana siku za karibuni aliniona nipo kisheikh aliniona kuhusu majini nikamuelimisha akajiona alikuwa gizani sana kuamini dhana potofu..

Sasa dhana hizo zipo sana na ni vizuri kubainisha wazi na kuweka sawa inapopatikana nafasi ,kuhusu watu kutukana kwa trend yao ya matusi mbona huu uzi haujachafuliwa kabisa kwa jinsi ninavyoona mimi swala hilo haliwezi kuwa sababu ya kutobainishwa ukweli na upotofu na nakupa kongole kwa kufuata kanuni nzuri ya majadiliano hauna jazba wala hakuna uliowatukana wala kuwajibu vibaya hata wale wazee wa lugha chafu umeenda nao kwa busara na kuwapuuza kwani kwenye uzi wake Akhi wa nasahau kwa waislamu wa hapa kuna watu wengi walikuja kutukana dini na kukazuka vita vikali mule na mabishano ukilinganisha na huu hapa kumetulia kabisa.

Vilevile kuna mtu kama Atufigwegwe god yeye ametoa ushuhuda kuhusu yeye binafsi kushirikiana na jini na akapewa nasahau humu pengine huenda uzi huu ukamfanya abadilike kwani katika wema hakuna kudharau jambo haswa jambo na kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia naamini nia yako ilikuwa na ni njema kabisa..
 
Inategemea kiwango cha uelewa wa mtu.
Nadharia yangu ni kuwa.

"Kitu chochote kinakufikisha mahala pengine"

Hivyo kujifunza hoja yoyote kunafaa.

Na sio kukanusha kanusha kitu chochote.
Nikikujibu 42, jibu langu linatufikisha wapi katika mjadala huu?
 
Sisi hatuelimishani mitandaoni sisi tunaenda kukaa chini kusomeshwa hatufichi kitu sisi

Sio kama nyie pastor akisema hakuna kuuliza ndo imepita iyo

Sasa kati yetu na sisi nani kuna walakini mkubwa mno?
Naomba unielimishe jua linazama bipi kwenye matope na kwenda kumsujudia Mungu?
 
Nikikujibu 42, jibu langu linatufikisha wapi katika mjadala huu?
Nitafurahi kwa jibu jipya na nitalifanyia kazi ya kulielewa vizuri zaidi.

Kumbuka kila jibu ni jibu sahihi kwa mjibuji.
 
Jazakallahu kheir Al akhy adriz hakika umetoa maelezo mazuri sana binafsi nimefurahi Sana Kwa maoni yako na Busara zako.

Shukrani sana
 
Dini hahiitaji elimu yoyote, unachosoma kilichoandikiwa ndicho hicho.
Shida ipo sehemu moja tu wakristo wengi hawana elimu juu ya uislam kwaiyo wanamezeshana propaganda sana juu ya uislam.

Lakini bado sioni tatizo kuitwa wafuga majini kama ufugi uwezi chukia kitu ukiona unakasilika ujue unayafuga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…